Vichekesho Vya Jumatano
Hili nalo neno kwa wavulana
Hili nalo neno
Demu wako anakuja kwako kasuka nywele za 30,000 na hujampa hata mia,we unakalia kusema waooo waoooo kama king’ora cha ambulance.
Shauri yako we endelea kusema waoooo waooo na atakuwa wao kweli.
๐๐๐๐๐๐๐
Angalia wadada walivyoumbuka kwenye hii test
Ticha katangaza test , Akatoa Masharti; Ukiandika jibu hamna kufuta au kukata.
Swali la kwanza,
Taja vyakula vi3 ambavyo ukienda hotelini umelipiwa utapenda kula (marks 1)
WAVULANA wakajaza; wali, ugali, mihogo.
WADADA wakajaza; burger, pizza, egg chop. Swali la
2: Eleza jinsi ya kupika kila chakula ulichotaja hapo juu. (marks 99)
wacha wadada waanze kuhangaika kukata majibu ya mwanzo!
SOMA HII! Baba kampaka Sumu mkewe kafa Houseboy
Baba mmoja Juzi alimpaka Sumu Mke wake kwenye Matiti akiwa amelala ili Mtoto akinyonya afe kwani alihisi sio wa kwake, akaondoka kwenda kazini aliporudi akakuta house boy amekufa, usiniulize alikufaje. Mie mambo ya umbea sipendi niliondoka zangu mapemaaa!!๐ ๐ ๐ ๐
๐๐๐๐๐๐
Huyu Jamaa ubahili umezidi kwa hiki anachomwambia huyu dada
Kama ni ubahili hapa umezidi
mdadaย Bby naomba hela nimpeleke mdogo wangu hospital kang’atwa na nyoka
JAmaaย embu mpe huyo nyoka cm niongee nae.. maisha yanakaba..๐๐
Madogo wa sikuizi ni kiboko, cheki huyu alichokifanya akiwa darasani na mwalimu wake
Muda wa kwenda nyumbani ulikuwa umefika, mwalimu
akasema: yeyote atakaye jibu swali langu lolote kwa usahรฌhi ataondoka asiye jibu atabaki.
Dogo mmoja akatupa begi nje ya dirisha.
Mwalimu akauliza nani katupa ilo begi nje?
Dogo akajibu fasta mimi. Akafungua mlango akaenda kwao.
neno moja kwa dogo
Tofauti ya mchaga na mhaya wakipata kazi
Mchaga hata apate kazi bank bado atasema yupoย kibaruani.
Acha sasa mhaya apate kazi katka mashine ya kusaga na kukoboa; utaskiaย i work as a crucial engineer in a monocotyledon finalizing company
๐๐๐
ย
Angalia hawa machizi walichokisema baada ya kuona ndege angani
Machizi wamekaa sehemu mara ghafla ikapita ndege angani.
Chizi wa kwanza akasema:ndege ile itakua imembeba raisi.
Chizi mwenzie akajibu:hapana imebeba wazungu kama ingembeba raisi tungeona pikipiki zimetangulia mbeleโฆ
da!balaaa
Cheki wanachokisema vichaa baada ya kuona ndege inapita angani
Vichaa wawili walikuwa wamekaa sehemu ghafla ikapita ndege angani kichaa mmoja akasema ndege ile hitakua imembeba rais kichaa mwenzake akajibu hapana ile imebeba wazungu kama ingekuwa imembeba rais ungeona mapikipiki mbele
Ndoa zina mambo, cheki haya mambo ya mtu na mke wake
Mke: mume wangu leo 2badilishe stail kwani nimechoka kla siku hiyo hiyo tu
Mme: kwel mke wang hata mimi nilikuwa nataka nikuambie hivyo hivyo
Mke: sasa stail ya leo wewe utaosha vyombo mimo nitaangalia tv
Mme: huna haya wala hujui bayaโฆ!!!
we unadhani ni xtail gani mume aldhani???
Angalia anachojibu huyu babu. Wazee wengine bwana
Babu: Mjukuu wangu ngoja nikusimulie hadithi ya mimi babu yako kwenye vita ya kagera
Mjukuu: Niambie babu
Babu: Kwenye vita ya kagera tulienda sehemu tukakamatwa wote askari na maadui wakatuambia chagueni kuuliwa au kubakwa.
Mjukuu: Sasa babu wewe ulichagua nn?
Babu: Niliuliwa!!!



















I’m so happy you’re here! ๐ฅณ


























































Recent Comments