Ujumbe wa kuasa kuhusu upendo wa kweli
Rafiki wa kweli hudhaminiwa kama familia
Pendo la kweli humaanisha, kupenda kweli
Kumlinda, kumjali, kuvumilia na kusameana
Rafiki wa kweli hudhaminiwa kama familia
Pendo la kweli humaanisha, kupenda kweli
Kumlinda, kumjali, kuvumilia na kusameana
Kulikuwa na vipepeo wawili waliokuwa wanapendana sana, siku 1 waliamua kucheza mchezo wa mahaba. Waliweka ua na walipanga kesho ambaye atakuja mapema na kukaa juu ya UA, atakuwa anampenda mwenzake zaidi. Asubuhi kipepeo dume alienda mapema sana na kukaa juu ya UA. Masikini kumbe jike alifika tangu jana kumwonesha mpenzi wake ni jinsi gani anavyompendaโฆ!! Jeeโฆ!! wewe, utamuonesha nini umpendaye ili aone ni kiac gani โฆโฆโฆโฆโฆโฆโฆโฆ.
Mawingu yametanda napanda kwenye kitanda, macho nayaangaza, taratibu navuta shuka na kujitanda, mishumaa pembezoni inaniangaza, mziki laini wanibembeleza kitu pekee nilichokikosa ni joto lako na vijimambo vyako kunako kitanda!
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
chekecho la huba ,toka uvunguni mwa moyo wangu
navika moyo wako taji la upendo,na kupulizia marashi ya hubaa ,usimpe mwingine mi ndiye ninayejua kulea.
Imani hufanya mambo yote yawezekane, Matumaini hufufua
yaliyopoteza uhai, lakini mapenzi hufanya mambo yote
yaonekane mazuri. Sina linalonihuzunisha maishani mwangu
kwa kuwa tunapendana!
naukunjua moyo wangu huishi milele maishani ,nafungua
nafsi nikupende wewe pekee,nafunga milango ya moyo wangu
ili
kutokupokea ugeni wowote wa moyo zaidi yako
mpenzi.nakupenda sana laazizi
tazama, nimezama
ndani ya bahari
la penzi lako
siwezi
kusonga mbele
kurudi nyuma
sijielewi
haya mapenzi ya fujo hayafai
kama wanipenda
jaribu kunipa raha
Unaweza usione kamwe ni kwa kiasi gani ninavyokujali.
Unaweza usisikie ni kwa kiasi gani nilivyokushiba, unaweza
usihisi namna gani ninavyokukumbuka. Sababu ni moyo wangu
tu uliyoyaficha hayo.
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
Recent Comments