Ujumbe wa kutuma kwa mpenzi wako ajione mwenye thamani kubwa
Wewe ni mngβarao machoni mwangu;
Tabasamu la midomo yangu;
Furaha ya uso wangu;
Kwa sababu bila wewe, mimi sinajipya.
Wewe ni mngβarao machoni mwangu;
Tabasamu la midomo yangu;
Furaha ya uso wangu;
Kwa sababu bila wewe, mimi sinajipya.
Natamani ningekuwa chozi jichoni mwako ambapo ningetelemka
na kuishia midomoni mwako, lakini kamwe sitamani uwe chozi
jichoni mwangu nitakupoteza kila muda niliapo.
Furaha yangu kubwa ni kuliona tabasamu lako, kujua uko na
furaha, na kuhisi upendo wako. Najua kuwa maisha mara
nyingine huwa ni makatili, na hiyo ni sababu niko hapa
kukuonyesha kuwa maisha yanaweza kuwa mazuri kama kuna mtu
anayekujali.
sura yako haifutiki usoni mwangu kirahic,ingawa upo mbal
nami lkn penzi lako bado nalikumbuka,hakuna anayeweza
kukata kiu yangu zaidi yako,nakupenda mpenzi wangu!
Happy birthday mpenzi, nakuombea kwa mwenyezi
akupe maisha marefu na kukuepusha na maradhi,
pongezi kwa wako wazazi kwa kukuzaa mpenzi,
nakupenda la azizi.
naukunjua moyo wangu huishi milele maishani ,nafungua
nafsi nikupende wewe pekee,nafunga milango ya moyo wangu
ili
kutokupokea ugeni wowote wa moyo zaidi yako
mpenzi.nakupenda sana laazizi
Ningependa siku moja utamani sana kuwa na mimi, na
uhangaike sana kunitafuta, ili ujue ni kwa kiasi
ninavyotamani kuwa nawe sasa.
Kila niamkapo mawazo yangu huwa kwako na upepo uvumapo
huhitaji uwepo wako na hasa nikumbukapo kumbato lako,
nakupenda mpenzi
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako, naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
tunda langu laangaliwa hawajui nilipoli chuma,
utamu wake maridhawa,hakika utalipenda.si mpi tunda langu mwingine na lila mwenyewe.
Mawingu yametanda napanda kwenye kitanda,
macho nayaangaza,
taratibu navuta shuka na kujitanda,
mishumaa pembezoni inaniangaza,
mziki laini wanibembeleza kitu pekee nilichokikosa
ni joto lako na vijimambo vyako kunako kitanda!
Ni ngumu kwa watu wawili kupendana wanapoishi Dunia
tofauti, lakini Dunia hizo zikutanapo na kuwa kitu kimoja,
hiyo ndiyo maana ya kuitwa wewe na mimi.
Kama busu ni maji ningekupatia bahari, kukumbatia ni
majani, ningekupa msitu. Mapenzi ni maisha ningekupa yangu
bure.
Niliumbwa kwa ajili yako, mbele yako nitakushika mkono, nikuonyesha sayari yangu, pendo langu la undani, na NITAKUHESHIMU milele mpenzi wangu.
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Kama ningeweza kubadili herufi, ningeweka yangu na yako
kuwa pamoja
Kulikuwa na vipepeo wawili waliokuwa wanapendana sana, siku 1 waliamua kucheza mchezo wa mahaba. Waliweka ua na walipanga kesho ambaye atakuja mapema na kukaa juu ya UA, atakuwa anampenda mwenzake zaidi. Asubuhi kipepeo dume alienda mapema sana na kukaa juu ya UA. Masikini kumbe jike alifika tangu jana kumwonesha mpenzi wake ni jinsi gani anavyompendaβ¦!! Jeeβ¦!! wewe, utamuonesha nini umpendaye ili aone ni kiac gani β¦β¦β¦β¦β¦β¦β¦β¦.
Kila nikuonapo napata weweseko, yako miondoko si ya kitoto
na zaidi wajua kuweka mikogo, umeumbika si kitoto,
nahitaji uwe wangu mama watoto!
Swt ulivyoumbika wengi wanateseka juu yako ,najua
wanakusumbua ni vema usiwakubalie, ukweli umebarikiwa
uzuri umeshushiwa na dhati ya penzi umetunukiwa nakupenda
Ucku ulalapo jua kuna m2 akupendaye,mchana uwajibikapo
tambua yupo anayekuwaza ,jioni uwapo mazoezini jua yupo
anayekuonea wivu,hata uwapo kwenye kumbi za burudani
tambua mwenzio nakulilia,usitoe penzi kangu akilini hata
km upo mbali nami!moyoni mwangu hutafutika milele!
Si vibaya mimi kukusifia kwani wewe ni wangu, nivingi umejaaliwa, vinavyouvutia moyo wangu, ama hakika uzuri wako umedhibiti matamanio yangu “SINTOMPENDA MWINGINE ZAIDI YAKO”
Recent Comments