SMS nzuri kwa mpenzi wako kumwambia kuwa ameitibu akili yako
Chuki huharibu akili; mapenzi huitibu. Umeitibu akili
yangu.
Chuki huharibu akili; mapenzi huitibu. Umeitibu akili
yangu.
Siku zote kwangu ni sherehe ni wewe unishereheshaye,ukweli
usio na kejeli mapenzi yako yanatii kiu yangu,moyoni
mwangu nimeridhia… .nakupenda daima mpenzi!
Ni ngumu kwa watu wawili kupendana wanapoishi Dunia
tofauti, lakini Dunia hizo zikutanapo na kuwa kitu kimoja,
hiyo ndiyo maana ya kuitwa wewe na mimi.
Pokea sms yangu iliyojaa utamu, nimeipamba kwa maneno
laini yenye ladha adimu, utamu wake ni kama
apple haufanani na ndimu, nimeituma kwako sms hii ikuletee
salamu “UHALI GANI MPENZI?”
Pokea sms yangu iliyojaa utamu, nimeipamba kwa maneno laini yenye ladha adimu, utamu wake ni kama apple haufanani na ndimu, nimeituma kwako sms hii ikuletee salamu “UHALI GANI MPENZI?”
»–——»>
Mshale huu unamtafuta mtu muhimu sana ktk
maisha yangu na kama umekutana nao
usiukwepe uache
uchome Moyo wako gharama
za matibabu juu yangu.
utamu wa penzi hunogeshwa na pendo la dhati pia utamu wa
penzi ni uwepo wangu na wako,ladha yake ni zaidi ya nazi
kwenye wali au royco kwenye mchuzi au pilipili kwenye
kachumbari, utamu wake ni zaidi ya asali au jam kwenye
mkate ,blueband kwenye uji.penzi tamu halina kifani
Naweza kuishiwa ujumbe wa kukutumia. Naweza kuishiwa utani
pia. Naweza kuishiwa chaji lakini moyo wangu hauwezi
kukosa nafasi ya kukuweka.
Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu, kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi?
Recent Comments