SMS nzuri ya kimahaba kueleza kuhusu penzi
penzi linaweza kuelezewa kwa namna nyingi. Namna moja
niijuayo nikumtumia mapenzi hayo mtu asomaye meseji hii
penzi linaweza kuelezewa kwa namna nyingi. Namna moja
niijuayo nikumtumia mapenzi hayo mtu asomaye meseji hii
Nakupa HAI, kwa sababu uko HAI, usingekuwa HAI, ni vigumu kupewa HAI, basi nawe wape HAI, walio HAI, maana ni bahati kuwa HAI, wengi walitamani kuwa HAI, lakini wamepoteza UHAI, Usione najidai, ila mimi naringia UHAI, Haya basi pokea HAI, ili moyo wako ufurahi. HAIIIIIIIIIIIII!!!
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Naweza kukuazima mabega yangu upande, masikio yangu usikilizie mikono yangu ushikie, miguu yangu, utembelee, lakini si moyo wangu kwani tayari unao wewe.
Nitaenda mbali Zaidi ya maono yako
Safarini nitajenga hekalu la pendo letu
Nitapuliza filimbi kama ishara ya utambulisho wako
Na mwanzo wa sherehe ya ndoa yetu
Natamani ningekuwa chozi jichoni mwako ambapo ningetelemka
na kuishia midomoni mwako, lakini kamwe sitamani uwe chozi
jichoni mwangu nitakupoteza kila muda niliapo.
Hata kama nitajidanganya kwamba sikupendi, moyo wangu
umeganda kwako na hakuna dalili za kukuacha, wewe ni wangu
peke yako dear…
Baadhi ya watu huzaliwa na vipaji. Huweza kufanya mambo
mazuri kwa ujuzi wao, lakini hamna anayekufikia wewe,
kwani ukinisogelea tu kila kitu huwa kizuri.
Njoo pendo langu nikutembeze
katika milango ya furaha
Nikuwakilishe mbele ya majamaa zangu
Nikuonjeshe asali ya pendo langu
Naweza kuishiwa ujumbe wa kukutumia. Naweza kuishiwa utani
pia. Naweza kuishiwa chaji lakini moyo wangu hauwezi
kukosa nafasi ya kukuweka.
Recent Comments