Ujumbe wa Kimahaba wa kumwambia mpenzi wako upo tayari hata kumpa maisha yako
Kama busu ni maji ningekupatia bahari, kukumbatia ni
majani, ningekupa msitu. Mapenzi ni maisha ningekupa yangu
bure.
Kama busu ni maji ningekupatia bahari, kukumbatia ni
majani, ningekupa msitu. Mapenzi ni maisha ningekupa yangu
bure.
Njoo pendo langu nikutembeze
katika milango ya furaha
Nikuwakilishe mbele ya majamaa zangu
Nikuonjeshe asali ya pendo langu
Mpenzi kwa mara ya kwanza nilipokuana niliogopa kukuambia,
hata nilipokuambia niliogopa kukupenda, nilipokupenda sasa
naogopa mno kukupoteza. Kusema kweli siko tayari kukukosa
katika maisha yangu.
Uamkapo nitakupa langu tabasamu
Ukweli wa moyo utawale roho yako
Kwani macho yako ndo uzuri kwangu
Nakupenda sasa na milele kipenzi change
Maneno huanza na ABC. Namba 123. Muziki na do re mi na
mapenzi huanza na mimi na wewe.
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
sura yako haifutiki usoni mwangu kirahic,ingawa upo mbal
nami lkn penzi lako bado nalikumbuka,hakuna anayeweza
kukata kiu yangu zaidi yako,nakupenda mpenzi wangu!
Ni ngumu kwa watu wawili kupendana wanapoishi Dunia
tofauti, lakini Dunia hizo zikutanapo na kuwa kitu kimoja,
hiyo ndiyo maana ya kuitwa wewe na mimi.
tazama, nimezama
ndani ya bahari
la penzi lako
siwezi
kusonga mbele
kurudi nyuma
sijielewi
haya mapenzi ya fujo hayafai
kama wanipenda
jaribu kunipa raha
Recent Comments