Meseji ya kumtumia mpenzi wako wakati unaenda kwake
nipe niridhike,nionjeshe usinilambishe,nikigonga
nikaribishe na penzi le2 2listawishe.
nipe niridhike,nionjeshe usinilambishe,nikigonga
nikaribishe na penzi le2 2listawishe.
Ni vigumu kumpata mwenye mapenzi ya kweli na zaidi yule
atakayekuwa tayari kukupenda zaidi, hivyo nafasi
inapopatika si busara kuichezea tudumishe penzi letu
laazizi wangu.
Ni ngumu kwa watu wawili kupendana wanapoishi Dunia
tofauti, lakini Dunia hizo zikutanapo na kuwa kitu kimoja,
hiyo ndiyo maana ya kuitwa wewe na mimi.
Unaonekana kung’ara leo nilijuaje…….ni kwasababu
unaonekana hivyo kila siku. Nakupenda sana Mpenzi wangu vile ulivyo kila siku kwangu wewe ni mpya.
Nina habari nzuri nataka kukuambia kuna mgeni leo kaja
kunitembelea,nguo nyekundu amevalia yaani!utamu wako kwa
sasa siwezi kukupatia
kwa maana mgeni kashakuharibia
nakupenda dear
Penzi lako ndiyo pumzi yangu nawezaje kukuacha laazizi,
ina maana nife??? Siwezi kukuacha nakupenda. Nitakupenda
mpaka mwisho wa uhai wangu.
Mapigo yangu ya moyo huongezeka pindi nisipokuona japo kwa
dakika plz mpenzi kaa karibu yangu utulize mapigo
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
Kumjali mtu ni rahisi, lakini kumfanya mtu akujali ni
vigumu, nashangaa umewezaje kunifanya nikujali?
Recent Comments