Meseji ya kumuaminisha mpenzi wako kuwa unampenda
upendo wa moyoni ndiyo dhati niliyoamini amini kwa haya
nisemayo nakupenda wewe ndiyo kaburi nitakalozikwa nalo
upendo wa moyoni ndiyo dhati niliyoamini amini kwa haya
nisemayo nakupenda wewe ndiyo kaburi nitakalozikwa nalo
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
Imara hautikisiki,kakamavu halishikiki penzi langu kwako
ni nuru daima halizimiki.upo juu katika mapenzi.
Moyo wangu umehifadhi hisia zako, nakuahidi kamwe
sintopunguza upendo kwako, tunza sms hii ya
ahadi kwenye simu yako, iwe kumbukumbu kila uisomapo!
“NAKUPENDA MALAIKA WANGU”
USikimbie nyuki ukakosa asali, utamu wa samaki ni kula na
wali,
usizidishe siki akawa mkali.
Ni
mimi niliye na dhiki nakujulia tu hali.
Bongo zenye fikra kali huwa na mawazo, suluhu na sababu;
ubongo wa kisayansi huwa na kanuni, nadharia na takwimu;
wangu una wewe tu!
Mapigo yangu ya moyo huongezeka pindi nisipokuona japo kwa
dakika plz mpenzi kaa karibu yangu utulize mapigo
Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu, kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi?
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
“Japokuwa” “Kuku” “Haogi” “Yai” “Lake” “Litabaki” “Kuwa” “Jeupe” “Tu” “Namaanisha” “Kuwa” “Hata” “Kama” “Ukiona” “Nipo” “”KIMYA”” Muda”
“Mrefu” “”UPENDO”” “Wangu” “Kwako” “””Bado””” “Uko” Pale pale!!!!! Usijali
“Tupo Pamoja” “Kwa” “Asilimia 100%”.
Recent Comments