Ujumbe wa kimahaba kwa umpendaye sana
Kama ningeweza kubadili herufi, ningeweka yangu na yako
kuwa pamoja
Kama ningeweza kubadili herufi, ningeweka yangu na yako
kuwa pamoja
Hakika wewe ndiye wangu mahabuba unayejua kunipa huba,
napenda unavyoniganda mithili ya ruba, nahahidi kukupa
mahaba yanayozidi shaba. Nakupenda.
Fungua macho yako uone kopa za mahaba ninazokumwagia,
fungua mikono yako na upokee mapenzi yangu,
fungua simu yako uone ni jinsi gani ninavyokukumbuka japo
kwa kukutumia sms mpenzi wangu,
Nakutakia usiku mwema
Wewe pekee upo moyoni mwangu, nitaendelea kukupenda siku
zote za maisha yangu! Katika siku hii ya wapendanao, wewe
ndiyo ua la moyo wangu!
nimetuma ndege wangu auzunguke ”moyo” wako kwa ” upendo
” auguse ”uso” wako kwa ”faraja” na mwisho
akunong’oneze sikioni taratibu kuwa nakupenda.
Penzi, maisha yangu yote nimesoma juu ya neno hili,
nimeota juu yake, nimelilia, nimelihitaji. Sasa pamoja
nawe nimelipata.
, – .(. – .
‘. .’
‘ . . . ‘ Napenda tunda hili likupoze makali uliyo nayo moyoni, Nimeliosha kwa maji safi na salama kwa ajili yako lipo tayari kuliwa.
“APPLE” Ni tunda lenye ishara ya UPENDO, AMANI & FURAHA. napenda liwe zawadi kwako siku hii ya leo.
Pokea sms yangu iliyojaa utamu, nimeipamba kwa maneno
laini yenye ladha adimu, utamu wake ni kama
apple haufanani na ndimu, nimeituma kwako sms hii ikuletee
salamu “UHALI GANI MPENZI?”
Mungu akupe umri wa mnazi uishi mingi miaka.
Akupe thamani ya mnazi kila kitu chatumika.
Kuanzia kuti lake mpaka kwenye kidaka.
Kitale katikati yake ukila utaridhika.
Matamu na maji yake hukata kiu haraka.
Weupe watui lake lina ladha ukipika.
Kupaka mafuta yake mwili hulainika.
Na kwenye machicha yake kazi nying hufanyika.
Hata na upepo wake uvumapo utacheka.
Sikijui kitu chake kipi kisichotumika.usiku mwema
Recent Comments