Kilimo cha Organic

Matumizi ya mihogo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea

Muhogo Inazuia Minyoo na vidukari.

Hatua za Kutayarisha dawa

  • Toa maji ya matunda kwa kuponda mizizi;
  • Pima k i w a n g o kimoja cha maji ya m a t u n d a sawa na maji ya kawaida (1:1).
  • Nyunyiza haraka ukitumia lita nne kwa mita moja za mraba, inasemekana kuwa na athari kubwa.
  • Subiri kwa siku ishirini kabla ya kupanda.

Angalizo: Tafuta ushauri wa mtaalamu wa kilimo kabla ya kutumia dawa yoyote ya asili

Read and Write Comments

Jinsi ya kuandaa mbangimwitu kama Dawa ya magonjwa na ya kuulia wadudu shambani

Mbangi mwitu au kwa kisayansi ni African marigold / (Tagetes erecta) Unazuia Bakteria, fungusi na wadudu kama vile Siafu, bungo pamoja na aina nyingine za wadudu.

Hatua za Maandalizi ya dawa na kutumia

  1. Ponda gramu 100-200 za matawi, mizizi na maua;
  2. Weka lita moja ya maji yaliyochemka;
  3. Loweka kwa masaa ishirini na nne;
  4. Ongeza lita moja ya maji baridi,
  5. Nyunyiza kwenye mimea au mchanga.
Read and Write Comments

Mambo makubwa yanayosababisha kulazimika kulima au kutifua udongo

Kutifua udongo ni jambo la muhimu sana ili kuufanya udongo kuwa bora.

Umuhimu wa kutifua udongo ni kama ifuatavyo
1. Hulainisha udongo ili kuruhusu mizizi ya mimea kupenya kwa urahisi.
2. Kutifua kunaboresha uwezekano wa kupenya kwa nitrogen na oxygen kutoka kwenye hewa.
3. Kunawawezesha viumbe hai waliopo kwenye udongo kufanya kazi zao ipasavyo.
4. Kunasaidia Kuandaa sehemu ya kuwekea mbegu.
5. Kutifua kunauongeza uwezekano wa maji kupenya kwenye udongo na kupunguza uyeyukaji wa maji.
6. Kuchanganya mabaki ya mimea na samadi kwenye udongo

Read and Write Comments

Faida ya kupanda maharagwe katikati ya kabichi

Maharagwe yanapandwa kwenye kabichi yanafanya kazi zifuatazo;

Kudhibiti wadudu (mtego).

Maharage yanaweza kupandwa kati ya mistari ya kabichi yakiwa kama mitego kwani yanasaidia kulinda kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Kuboresha udongo.

Maharagwe yanaongeza nitrojeni kwenye udongo

Chakula cha mifugo.

Maharagwe yanaweza kutumika kulishia mifugo kama ng’ombe mbuzi na kondoo.

Matandazo.

Maharage yanaweza yakatumika kama matandazo kwenye shamba kusaidia kulinda unyevu.

Kutengenezea mbolea.

Maharagwe yakioza yanaweza kuwa mbolea nzuri ya shamba lako

Read and Write Comments

Jinsi ya kutumia mashonanguo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea

Mashonanguo kwa kiingereza ni Blackjack au kwa kisayansi yanajulikana kama (Bidens
pilosa)
Mashona nguo yanazuia wadudukama vile Vidukari, Siafu, bungo, katapila, chenene (crickets), nyenyere, siafu na inzi weupe.

Jinsi ya Kutayarisha na kutumia mashonanguo

  1. Jaza kikombe kilichojaa mbegu ambazo zimekomaa na maji;
  2. Chemsha kwa dakika kumi au loweka kwenye maji kwa saa ishirini na nne, kisha upooze.
  3. Ongeza lita moja ya maji na kijiko kimoja kidogo cha sabuni;
  4. Kisha unyunyizie mimea.

Matumizi mengine

  1. Mbegu zinaweza kutawanyishwa karibu na vichaka kuvutia mchwa.
  2. Mmea waweza kupondwa au kufikichwa kisha maji yake yatumike kunyunyizia mimea.

Angalizo: Kiasi kingi cha dawa hii chaweza kudhuru baadhi ya maua ya mimea.

Read and Write Comments

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Wigo wa mimea ni kinga nzuri ya mazao shambani. Mimea ya wigo inaweza kutumika kama kizuizi cha wadudu kuhama hama.

Wigo hutatiza vidukari kuhama na kuingia bustanini. Kwa mfano, mimea kama tithonia ni kizuizi kwa aina nyingi sana za wadudu.

Safu za mbaazi zimekuwa zikitumika kulinda nyanya, viazi, kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Maharage yanaweza kupandwa kati ya mistari ya kabichi yakiwa kama mitego kwani yanasaidia kulinda kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Maharagwe yanapandwa kama mtego kwenye kabichi lakini yanafanya kazi ya kudhibiti wadudu (mtego), kuboresha udongo, chakula cha mifugo, matandazo au kutengenezea mbolea.

Vile vile wigo wa mimea ni makazi ya wanyama/wadudu wanaowinda.

Read and Write Comments

Shopping Cart
0
    0
    Your Cart
    Your cart is emptyReturn to Shop
    🏠 Home 🔒 Login 📝 Register 💡 Tools