Tambi za mayai ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kuandaa pale ninapokua ninaharaka au sina muda mrefu wakukaa jikoni.pishi hili huchukuca muda mfupi sana na nimlo uliokamilika.
Mahitaji
- Tambi Β½ paketi
- Vitunguu maji 2 vikubwa
- Karoti 1
- Hoho 1
- Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
- Carry powder kijiko 1 cha chai
- Njegere zilizochemshwa Β½ kikombe
- Mafuta kwa kiasi upendacho
- Mayai 2
- Chumvi kwa ladha upendayo
Njia
1.Chemsha maji yamoto yanayotokota,ongeza chumvi na mafuta kidogo,weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive.Chuja maji yote ili kupata tambi kavu
2.Katika bakuli piga mayai kisha weka pembeni
3.Katika kikaango,weka mafuta,vitunguu maji ,vitunguu swaumu,hoho, karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva.
4.Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya .
5.Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi ziwe kavu.Tayari kwa kula