Serikali i i inatambua kukua kwa tatizo la dawa za kulevya nchini, kwani dawa za kulevya nyingi zinazotumika zinapitishwa na kuingizwa kwa magendo nchini. Kutokana na hali hii serikali imepitisha sheria kuhusu tuhuma za dawa za kulevya yaani Sheria ya Kuzuia Matumizi ya Dawa za Kulevya ya mwaka 1995.
Sheria hii i ii inatoa maelekezo ya kumshughulikia mtuhumiwa wa dawa za kulevya na hutoa adhabu kali kwa waliopatikana na hatia. Katika kusaidia vita dhidi ya dawa za kulevya, Serikali ya Tanzania iliunda tume ya wataalamu mwaka 1996 iitwayo Tume ya Taifa ya Kuzuia na Kuratibu Dawa za Kulevya ili kuendeleza vita hivyo.
Tume hii inawasaidia polisi, polisi wa mipakani na forodha ambao wanazuia uinizaji na usambazaji wa dawa za kulevya kupitia mipakani na kuharibu mashamba ya bangi na mirungi. Wakala hawa kwa sasa wanafanya kazi bega kwa bega na nchi jirani i i ili kuzuia uingizaji wa dawa za kulevya kupitia mipakani. Vilevile inaandaa wataalamu kwa kutumia ASIZE mbalimbali ambazo kazi zao ni kuelimisha jamii kuhusu athari na hatari ya dawa za kulevya na kuwasaidia waathirika.
Tume hii ya wataalamu vilevile inafikiria kuhusu kampeni za kitaifa zinazolenga kuelimisha kuhusu athari za dawa za kulevya. Lakini kazi ya tume hii ni ngumu kutekelezwa kwani vita dhidi ya dawa za kulevya ni jukumu la kila mtu na sio serikali peke yake. Inahitaji msaada kutoka kwa kila mtu na jamii kwa ujumla.
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Recent Comments