Mambo ya msingi kujua kuhusu ugonjwa wa ngiri

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni: Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha au kuvimbiwa (Constipation). Vitu hivyo pamoja na mtu kuwa na misuli au tishu zilizopoteza uimara au uwazi (opening or hole) humfanya mtu apate ngiri (hernia).

Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama uvimbe au kujaa katika eneo husika (baadhi ya maeneo yametajwa hapo juu) na pia kwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara na daktari huwezesha kugundua tatizo hili.

Njia inayoweza kutatua tatizo hili ni kwa mtu mwenye ngiri kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea. Pia kutegemeana na kihatarishi cha tatizo hili, mtu unaweza kuwa unafanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii itasaidia pia mmeng’enyo (digestion) wa chakula tumboni na kuepusha kuvimbiwa. Matunda (Vitamin C) husaidia kuunganisha tishu zilizolegea na pia husaidia kupona haraka kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji (operesheni). Na kama tatizo lako ni la kukohoa kwa muda mrefu kunakosababishwa na uvutaji wa sigara, ni vyema ukasitisha uvutaji ili kupunguza madhara au makali ya ngiri lakini pia kusitisha sigara kwa ajili ya usalama wa afya yako.

Vyakula visivyotakiwa kipindi cha ujauzito

Ili mtoto azaliwe akiwa na afya njema pamoja na akili timamu, akiwa tumboni lazima alishwe lishe bora na mlo sahihi. Mwenye jukumu la kutoa lishe bora na sahihi kwa kiumbe kilichomo tumboni ni mama. Anatakiwa kujua aina ya vyakula anavyopaswa kula. Vivyo hivyo, anatakiwa kujua aina ya vyakula vya kuviepuka.

Katika makala ya leo, tunaangalia orodha ya vyakula vilivyokatazwa. Mama mjamzito haruhusiwi kuvila vyakula vifuatavyo kwa faida ya kiumbe kilichomo tumboni na kwa faida yake mwenyewe:

Mayai Mabichi

Ulaji wa mayai mabichi au vyakula vilivyochanganywa na mayai mabichi, mjamzito haruhusiwi kuvila. Kuna baadhi ya β€˜Ice Cream’ na β€˜mayonaizi’ hutengenezwa kwa kuchanganywa na mayai mabichi. Mjamzito amekatazwa kuvila vyakula hivyo.

Maini

Maini yana kiwango kikubwa cha madini aina ya chuma. Hata hivyo, yana kiasi kikubwa cha Vitamin A ambacho huweza kuwa na madhara kwa mtoto kikizidi.

Maziwa mabichi

Maziwa mabichi huweza kuwa na bakteria ajulikanae kama β€˜Listeria’, ambaye huweza kusababisha kuharibika kwa mimba. Unapokunywa maziwa, hakikisha yamechemshwa au kama ni ya paketi hakikisha ni yale yaliyoandikwaβ€˜Pasteurized’ na siyo β€˜Unpasteurized’.

Kafeini (Caffeine)

Ingawa baadhi ya utafiti unaonesha kuwa unywaji wa kiasi kidogo cha kafeini hauna madhara, lakini kuna utafiti mwingine unaonesha kuwa unywaji wa kafeini una uhusiano na kuharibika kwa mimba. Kafeini ni aina ya kirutubisho kinachopatikana ndani ya kahawa.

Iwapo mjamzito atakunywa kahawa, basi anywe kiasi kidogo sana kisichozidi kikombe kimoja kwa siku. Kwa kawaida kahawa hukausha maji mwilini, hivyo unywaji wake husaidia kukauka maji mwilini ambayo ni muhimu sana kwa mjamzito.

Utafiti mwingine unaonesha kuwa kafeini inahusishwa pia na uharibikaji wa mimba, uzaaji wa watoto β€˜njiti’ na watoto wenye uzito mdogo. Ni vizuri kunywa maji ya kutosha, maziwa na juisi na kuepuka kunywa vinywaji vyenye kahawa.

Pombe

Hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa unywaji wa pombe kiasi kidogo wakati wa ujauzito hauna madhara, kwa maana hiyo matumizi ya pombe hayaruhusiwi kabisa wakati wa ujauzito, hata kama ni kidogo.
Unywaji wa pombe wakati wa ujauzito huweza kuathiri ukuaji mzuri wa mtoto. Kutegemeana na kiasi atakachokunywa mjamzito, pombe inaweza kumsababishia mtoto ugonjwa hatari utokanao na pombe (Fetal Alcohol Syndrome).

Nyama mbichi

Epuka kula samaki au nyama mbichi au iliyopikwa lakini haikuiva vizuri. Utajiepusha na uwezekano wa kula bakteria na vijidudu vingine hatari kwa afya ya mtoto tumboni. Mjamzito anapokula nyama, anatakiwa kuhakikisha imeiva sawasawa.

β€˜Soseji” na β€œSandwich”

Mjamzito haruhusiwi kula β€˜soseji’, β€˜sandwichi’ za nyama na vyakula vingine vilivyotengenezwa kwa nyama. Inaaminika kuwa nyama zinazoandaliwa kwa ajili ya kutengenezea vyakula kama hivyo, huwa vimewekewa vihifadhi vyakula (preservatives) ambavyo vinaweza visiwe vizuri kwa afya ya mtoto.

Samaki wenye zebaki (Mercury)

Wajawazito wamekatazwa kula samaki wenye kiasi kingi cha madini ya zebaki. Ulaji wa zebaji kwa wajawazito umehusishwa na uzaaji wa watoto taahira. Mfano wa samaki hao ni pamoja na Papa, Chuchunge na dagaa wakubwa.

Vyakula vinavyosaidia kuongeza kinga ya mwili

Watu wengi tumekuwa tukijali kazi zetu za kila siku bila kujali hali ya afya zetu matokeo yake kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya ghafla. Suala la kula pengine ndilo nguzo ya kwanza ya afya ya binadamu. Mwili ukiwa sawia bila shaka utaweza kufanya mambo yako yote, na usipokuwa sawa basi hutaweza kutimiza lengo lako lolote! Hivi ni vyakula kadhaa vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga ya mwili wako

Uyoga

Usishangae! Ndiyo hiki ni moja ya vyakula muhimu zaidi kuimarisha afya yako kwani huchangia kiasi kikubwa kuimarisha seli nyeupe za damu zinazofanya kazi ya kupambana na magonjwa mbalimbali!

Supu ya kuku

Wengi watahisi ni gharama lakini si kubwa kuzidi gharama ya kumuona daktari! Unywaji wa supu ya kuku ya moto husaidia kuzuia kupungua kwa seli nyeupe za damu vilevile hupunguza uwezekano wa kupata matatizo yanayohusiana na mapafu na mfumo wa hewa kiujumla!

Yogurt (yogati)

Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe na kimea, hupatikana kwa ladha mbalimbali kulingana na matakwa yako, yogati pengine ndio chakula kinachoongoza kwa kuogeza Kinga ya mwili wako

Matunda

Yanapatikana sehemu yoyote duniani kwa bei unazozimudu, katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, matunda asiyekula matunda anahatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda .

Vitunguu saumu

Hupatikana Kila soko Tanzania! Japokuwa vitunguu saumu vimekuwa vikitumika sana kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali toka enzi za mababu, wataalamu wameshauri pia vitunguu hivi ni chanzo muhimu kwa kinga ya binadamu. Vitumie kwa kutafuna (kama unaweza) au weka kwenye chakula!

Viazi vitamu (mbatata)

Unaweza kuhisi ngozi sio sehemu ya muhimu katika kinga ya binadamu lakini ukweli ni kwamba ngozi ni sehemu ya muhimu sana kwa mwili wa binadamu. Kwa kinga kamili ya mwili wa binadamu tunahitaji Vitamin A ambayo hupatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu.

Karoti

Karoti zina ziada kubwa ya vitamin pengine kuliko tunda lolote lile hivyo jitahidi kujumuisha karoti kama kiungo kwenye chakula au unaweza kuitafuna ikiwa mbichi.

Samaki

Husaidia seli nyeupe kuzalisha ctokins zinatohusika kuzuia baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na virusi hasa yale yanayohusiana na mfumo wa hewa nk.

Matikiti

Wengi Hudharau lakini tunda hili ni muhimu sana katika afya ya kila siku ya binadamu kwani husaidia kuongeza kiasi cha maji mwilin, madini chuma na kuimarisha seli nyeupe za damu

Sababu ya meno kubadilika rangi

Wapo baadhi ya watu wanashindwa hata kuachia kicheko chenye bashasha hii ni kwa sababu meno yao yamekuwa na rangi, hivyo kuwafanya watu hao kuona aiabu. Pia watu wengi wakiona meno yana rangi ya njano hudhani ni machafu, meusi yanahitaji kusafishwa ili yawe meupe.

Meno kubadilika rangi huweza kuwa ni sababu moja au muunganiko wa sababu mbalimbali kama ifuatavyo;

Matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye kaboni, sigara na mvinyo (wine) kwa muda mrefu husababisha kubadilika kwa rangi ya meno kwa juu (extrinsic staining).

Utumiaji wa maji yenye madini mengi ya fluoride katika kipindi cha utoto (dental fluorosis).

Matumizi ya dawa aina ya tetracycline kwa mama mjamzito ambaye tayari meno ya mtoto aliye tumboni yameanza kuumbwa lakini hayapata madini ya kutosha.

Maumbile yasiyo sahihi ya sehemu ya juu ya jino (amelogenesis imperfecta). Iwapo sehemu hii imeumbwa ikiwa laini kuliko inavyotakiwa huwa rahisi kufyonza rangi na jino huota likiwa limebadilika rangi au hubadilika baada ya muda.

Kufa kwa sehemu hai ya jino hasa kutokana na kuumia kwa jino au ajali (pulp necrosis), hali hii huweza huchukua miaka mingi mpaka kutokea kubalika rangi ya jino..

Jino liliozibwa kwa kutumia material aina ya amalgam huweza kubadilika rangi na kuwa nyeusi.

Mara nyingne jino lililotibiwa kwenye mzizi wa jino (root canal treatment ) huweza kubadilika rangi baada ya miaka mingi.

Kuna njia mbalimbali ambazo hutumika kuyafanya meno yaliyo na rangi isiyo ya kawaida kuwa meupe.

Njia hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu kutokana na jinsi alivyoathirika. Kuna njia nyingi ambazo huweza kuyang’arisha kwa ndani (internal bleaching) au kuyangarisha kwa nje (external bleaching).

Endapo una tatizo la meno yaliyobadilika rangi, muone daktari wa kinywa na meno kwaajili ya ushauri na matibabu kwani kinywa kizuri na chenye afya huongeza kujiamini.

Umuhimu wa kupata chanjo

Siku zote sisi wanadamu huwa tunaambizana kuwa, kinga ni bora kuliko tiba, tukiwa na maana kwamba, ni vyema mtu ukachukua tahadhari mapema kabla haujafikwa na jambo au tatizo fulani.

Vivyo hivyo katika chanjo, hii ni kinga ambayo hutolewa kwa binadamu na katika umri tofauti tofauti ili kuuwezesha mwili kutengeneza ulinzi asilia (antibodies) ambao utauwezesha mwili uwe na nguvu zaidi za kupambana na magonjwa au visababishi vya matatizo mbalimbali ya kiafya ambavyo siku zote vimekuwa ni sehemu ya maisha ya mwanadamu.

Mpenzi msomaji, ni vyema ukafahamu kuwa chanjo SIYO tiba, na siku zote hutolewa kwa watu ambao hawana ugonjwa au tatizo husika linaloendana na chanjo hiyo, mfano, kama mtoto anao ugonjwa wa surua, basi itabidi apate matibabu ya surua na siyo chanjo ya surua. (Ila kumbuka kuwa matatizo mengine ya kiafya kama vile kukohoa, kuharisha au mafua, havimzuii mtu kupata chanjo).

Pengine utajihoji ni kwa nini inakuwa hivi?, hii ni kutokana na kwamba, chanjo siku zote dozi za dawa zake huwa ni kidogo ukilinganisha na dozi endapo hiyo dawa itatumika kutibu ugonjwa husika mfano surua au kifua kikuu, hivyo kwa kuwa dozi ni ndogo, basi haitakuwa rahisi kutibu mtu ambaye tayari anao ugonjwa.

Kitu kingine katika chanjo ni kwamba, baadhi ya chanjo huwa ni chembe chembe maalumu ambazo hufanana na aina ya ugonjwa ambao umekusudiwa kuzuiliwa au kukingwa, hivyo chembe chembe hizi huwa katika kiwango kidogo sana ambacho hakiwezi kukusababishia matatizo yoyote ya kiafya, ila mwili wako utaamshwa utengeneze kinga za kutosha ili endapo mazingira uliyopo yatakuwa na ugonjwa huo husika, wewe mwili wako utakuwa tayari kupambana ila chembe chembe hizi maalumu hazitaweza kukutibu endapo tayari unao ugonjwa husika.

Mambo ambayo huweza kujitokeza baada ya mtu kupata chanjo ni pamoja na hali ya joto la mwili kupanda au homa, ingawaje siyo lazima mtu apatwe na hali hiyo cha kufanya ni kutumia dawa za kushusha homa na baada ya muda mwili wako utarejea katika hali yake ya kawaida, hivyo endapo hali hiyo itajitokeza kwako usiwe na shaka.

Chanjo itakuwezesha kujikinga dhidi ya magonjwa, kukupunguzia gharama za matibabu na utapata muda ya kuendelea na shughuli zako za kila siku, kwani wewe au familia yako mtakuwa na afya bora.

Mambo ya kufanya ili kupona majeraha mapema

Hakuna mtu anayependa kupata majeraha au kuchelewa kupona majeraha. Kwa kuwa uhai na uzima wetu haupo mikononi mwetu, ni vyema tukafahamu kuwa kuna wakati tunaweza kuumia.

Kwa kutambua hili karibu nikufahamishe mambo matano unayoweza kuyafanya ili kuharakisha kupona majeraha.

1. Kula vizuri

Lishe bora ni muhimu wakati wote, lakini ni muhimu zaidi mara unapokuwa na majeraha. Ili uweze kupona majeraha mapema unahitaji ule matunda na vyakula vyenye protini, vitamini C, B12 pamoja na madini ya chuma kwa wingi.

Vyakula na matunda hayo ni kama vile machungwa, mapapai, mayai, maziwa, samaki, maharage, n.k. Kwa kula vyakula hivi mwili utaweza kutibu majeraha kwa haraka zaidi.

2. Pumzika vya kutosha

Kupumzika ni njia ya kuupa mwili nafasi ya kujijenga na kujitibu wakati wa majeraha. Kutokana na mtindo wa maisha au changamoto za kiuchumi, baadhi ya watu hawapati muda wa kupumzika wapatapo majeraha.

Hivi leo utamkuta mtu akiendelea na shughuli zake huku akiwa na plasta, au bandeji bila hata kujali. Ili uweze kupona mapema unahitaji kuupumzisha mwili kwa kiasi cha kutosha ili upone vyema.

3. Fuata maelekezo

Kutokana na majeraha uliyoyapata daktari anaweza kukataza usile au sifanye kitu fulani lakini wewe hutaki; je unafikiri utaweza kupona mapema?

Watu wengi hukatazwa vitu kama vile pombe au kazi ngumu mara wapatapo majeraha, lakini ni wachache ndiyo wanaoheshimu hili.

Ni lazima ufuate ushauri wa daktari ikiwa unataka kupona mapema.

4. Kunywa maji mengi

Maji huchukua takriban asilimia 70 ya mwili wa binadamu. Kunywa maji mengi uwapo na majeraha kutakuwezesha kupona majeraha yako mapema.

Maji huboresha kinga mwili, huboresha misuli pamoja na viungio (joints) mbalimbali hivyo kukuwezesha kupona majeraha mapema.

5. Ogea maji ya baridi

Tafiti mbalimbali zilizofanywa zimeonyesha kuwa kuna manufaa makubwa ya kuogea maji ya baridi. Manufaa haya pia yapo kwa mtu aliyepata majeraha.

Kuogea maji ya baridi kutasababisha mzunguko mzuri wa damu, hivyo viini lishe na tiba vitasafirishwa vyema kwenda kuponya majeraha; pia maji baridi hupunguza maumivu ya vidonda au majeraha.

Kwa hakika lishe bora ni tiba ya maradhi takriban yote. Katika makala hii umeona jinsi lishe bora pamoja na kuzingatia kanuni chache za msingi za afya kunaweza kukusaidia kupona majeraha mapema.

Mambo Mubimu kujua Kuhusu Tatizo la Shinikizo la damu (Tatizo la presha)

Ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa uchafu. Shinikizo la damu hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa Sphygmomanometer

Shinikizo la damu husababishwa na nini?

Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu:

  1. Uvutaji sigara
  2. Unene na uzito kupita kiasi
  3. Unywaji wa pombe
  4. Upungufu wa madini ya potassium
  5. Upungufu wa vitamin D
  6. Umri mkubwa
  7. Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
  8. Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin

Uanishaji wa shinikizo la damu

Presha ya kawaida <120 <80
Presha inayoelekea kupanda 120-139 80-89
Presha hatua ya 1 140-159 90-99
Presha hatua ya 2 160-179 100-109
Presha hatua ya 3 β‰₯180 β‰₯110

Shinikizo la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi sana duniani na hii ni kutokana na kutokujuwa ni nini hasa husababisha ugonjwa huu mwilini. Shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata masharti.

Katika makala hii tutaona uhusiano mkubwa uliopo kati ya upungufu wa maji mwilini na ugonjwa huu, mwishoni utakuwa umeelewa sasa ni jinsi gani ilivyo rahisi kabisa kujiepusha na kujiponya ugonjwa huu. Endelea kusoma.

Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku likisababisha mshtuko wa moyo (Heart Attacks), kupooza na kiharusi (Strokes).

Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.

Dalili zitakazokutokea unapokuwa na ugonjwa huu ni pamoja na;

  1. Maumivu ya kichwa (Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi nyakati za asubuhi),
  2. Kuchanganyikiwa,
  3. Kizunguzungu,
  4. Kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni),
  5. Kutoweza kuona vizuri au
  6. Matukio ya kuzirai.
  7. Uchovu/kujisikia kuchokachoka
  8. Mapigo ya moyo kwenda haraka
  9. Kutokuweza kuona vizuri
  10. Damu kutoka puani
  11. Uonapo dalili hizi unapaswa kuwahi hospitali kupata vipimo.

Shinikizo la damu (hasa la juu) ni kiashiria cha mwili kupungukiwa maji kwa kiwango kikubwa, ni wakati ambapo mwili unajaribu kujizoesha na upungufu wa jumla wa maji wakati kunapokuwa hakuna maji ya kutosha kuijaza mishipa ya damu yenye kazi ya kusambaza maji kwenye seli mhimu.

Mishipa ya damu imebuniwa maalumu kuendana na mtiririko uliosawa wa ujazo wake wa damu na mahitaji mbalimbali ya tishu kwa kufunga na kufungua mishipa mbalimbali ya damu ndani ya mwili.

Figo hushtuka upesi kulingana na mtiririko wa damu. Hili linaposhindikana, yaani iwapo mtiririko au ujazo wa damu utapungua, basi Figo huitoa homoni iitwayo β€˜renini’ ambayo yenyewe huzarisha kitu kiitwacho β€˜angiotensini’ ambayo huwa na matokeo mawili; kwanza huzibana ateri na kupandisha shinikizo la damu, pili huisababisha tezi ya β€˜adreno’ kutoa homoni iitwayo β€˜aldosteroni’ ambayo huzifanya figo kuishikilia chumvi na hivyo kusababisha kupanda kwa shinikizo la damu.

Asilimia 94 ya damu ni maji. Kwa ujumla kila seli ndani ya miili yetu ina bahari ya maji baridi ndani yake na bahari ya maji chumvi nje yake. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa maji ya bahari hizo mbili.

Chumvi inayashikilia na kuyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli (osmotic retention) na potasiamu inayashikilia maji ndani ya seli.

Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji (yaani haunywi maji ya kutosha kila siku) mwili utaongeza ujazo wa maji chumvi kwenye bahari ya nje ya seli.

Kupitia mfumo maalumu, homoni iitwayo β€˜vasopressini’ hutolewa ambayo inaweza kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli na kuyachoma maji hayo baridi (baada ya kuwa yamechujwa) ndani katikati ya bahari ya ndani ya seli kama yanavyohitajika ili kuutunza uwiano sawa wa maji ndani na nje ya seli.

Lakini ili mbinu hii ifanikiwe, mbinu gani, mbinu ya kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli, vasopressini husababisha kapilari na mishipa ya damu kujikaza au kupunguza vipenyo vyake na kukupatia wewe shinikizo la juu la damu (BP) ambalo ni mhimu ili kuyachuja na kuyachoma maji baridi ndani ya seli toka katika bahari ya maji chumvi iliyopo nje ya seli.

Kama mishipa ya damu haitapunguza vipenyo vyake, baadhi ya gesi itaachana na damu ili kuziba nafasi zilizowazi kutokana na kupungua kwa umajimaji mwilini na hatimaye kukusababishia msongamano wa Gesi (Gas locks).

Sifa hii ya vipenyo vya mishipa ya damu kujirekebisha kwa ajili ya mzunguko wa damu, ndiyo mtindo unaotumika zaidi katika kanuni za kihaidroliki wakati ambapo mzunguko wa damu mwilini umejirekebisha kuendana na kiasi cha umajimaji kinachopatikana.

Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji kwa mfano kutokana na kutokunywa maji ya kutosha; asilimia 66 ya kuishiwa maji inajionesha kwa kupungua kwa ujazo wa seli, asilimia 26 inapotea toka ujazo wa umajimaji uliopo sehemu ya nje ya seli na asilimia 8 tu inapotea toka katika ujazo wa damu.

Shinikizo la juu la damu ni kiashirio cha mwili kupungukiwa maji kwa asilimia 8 tu, lakini madhara yanajitokeza sababu ya asilimia 66 ya kupunguwa kwa ujazo wa seli.

Maji na chumvi vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida.

Hii ndiyo sababu shinikizo la damu linapaswa kutibiwa kwa kuongeza unywaji wa maji pekee. Dr.Batmanghelidj anasema; Maji peke yake, ni dawa bora ya kukojosha, pekee ya asili tuwezayo kuiendea.

Kama watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu wangeongeza kiasi cha uchukuaji maji, hawatazihitaji dawa za kukojosha, watazarisha mkojo wa kutosha na hivyo kuiondoa chumvi iliyokuwa imezidi!. Watatakiwa pia kuacha kula vyakula visivyo na chumvi na hivyo kuepukana na mikakamao ya mishipa (cramps) kwenye miguu yao.

Madhara yanayoweza kuletwa na shinikizo la damu:

Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, kutokulielewa shinikizo la damu kama moja ya ishara za mwili kupungukiwa maji na kulitibu kwa dawa za kukojosha ambazo zinaukausha mwili zaidi, baada ya muda zitasababisha;

  1. Kuzibika kwa ateri za moyo na ateri ziendazo kwenye ubongo
  2. Shambulio la moyo (heart attack)
  3. Mishtuko midogo midogo au mikubwa inayopelekea kuzimia
  4. Ugonjwa wa kibofu cha mkojo
  5. Kiharusi
  6. Kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wanaume
  7. Kuharibiwa kwa ubongo na matatizo ya akili kama vile kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Daktari mwingine, Dr.David Brownstein katika kitabu chake kiitwacho; β€œSalt Your Way to Live”, anasema kwamba alifundishwa katika vyuo vya kiganga kuwa chumvi husababisha shinikizo la damu na kuwa kila mmoja lazima ale vyakula vyenye chumvi kidogo. Na hili watu wengi wamekuwa wakiamini hivi.

Wakati akiwatibu wagonjwa wake, anasema; alianza kuona kuwa wale wanaotumia vyakula vyenye chumvi kidogo wanapata matokeo ya chini au wanapata nafuu ndogo sana kutoka katika vyakula hivyo vyenye chumvi kidogo au bila chumvi kabisa na wengi wao walitokewa kuwa na uhaba mkubwa wa madini katika miili yao.

Katika utafiti wake ili kuwasaidia wagonjwa wake, ndipo akaja na jibu la chumvi ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ambayo huwa na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake, alianza kuona kitu kigeni kinaanza kutokea. Wagonjwa wake hao wakaanza kuona mashinikizo yao ya damu yanaanza kushuka katika kiwango ambacho wanaweza kuachana kabisa na matumizi ya dawa.

Dr.Batmanghelidj anasema, ikiwa watu watajishughulisha na mazoezi hasa mazoezi ya kutembea kwa miguu, watakunywa maji halisi zaidi na kuongeza chumvi (siyo sodiamu) kidogo ya ziada kwenye vyakula vyao, mashinikizo yao ya damu yatarudi katika hali yake ya kawaida.

Swali la kujiuliza; Ni zaidi ya miongo minne sasa tangu tulipoambiwa kula vyakula vyenye chumvi kidogo ili kuepukana na shinikizo la damu, kwanini sasa Idadi ya watu wanaopatwa na ugonjwa huu inazidi kuongezeka?.

Narudia tena, mwili unapoanza kuishikilia chumvi, hufanya hivyo ili kuhifadhi maji, toka katika bahari chumvi hiyo ya nje ya seli, maji huchujwa na kutumika wakati wa mahitaji ya dharura.

Maji na chumvi kwa pamoja vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida. Kuikimbia chumvi kunasababisha shinikizo la damu (BP) kuwa sehemu ya maisha yetu, tutapata nafuu, lakini baada ya muda mfupi hali hurudi ileile na pengine kuwa watumwa wa kuchagua kula hiki au kile.

Tofauti na zamani ambapo shinikizo la juu la damu lilipokuwa ni ugonjwa wa watu wanene au wenye uzito uliozidi pekee, siku hizi wanene kwa wembamba, watoto kwa wakubwa wanaugua BP.

Madhara ya kuwa mnene kupindukia

Unene(obesity), ni ugonjwa unaokua kwa kasi kipindi hiki ukiambatana na madhara makubwa kiafya hata vifo.

Unene hupimwa kwa kutumia kipimo kinachotambulika kitaalamu kama BMI (yaani uzito kwa Kilogram kugawa kwa urefu kwa mita mara mbili).

Tatizo la unene uliopindukia huweza kusababisha mhusika kutengwa katika jamii, kubaguliwa, kudhihakiwa hata kunyanyapaliwa hivyo kuleta madhara kisaikologia kwa mgonjwa.

Sababu za unene uliopindukia ni pamoja na kurithi. Mtoto aliyezaliwa na wazazi wanene, ana asilimia 80 ya kuwa mnene, aliyezaliwa na wazazi wembamba, ana asilimia 10 ya kuwa mnene.

Utamaduni na ukosefu wa nidhamu katika vyakula, pia unachangia unene uliopindukia.

Mfano; kuna ongezeko kubwa la watoto na vijana wanene kwa sasa mijini kuliko vijijini.

Madhara yaletwayo na unene uliopindukia ni mengi, lakini kwa uchache ni pamoja na kulika kwa jointi hasa za miguu, maumivu kiunoni na katika nyonga, shinikizo la damu, kisukari, pia kukosa usingizi kutokana na kubanwa kwa hewa.

Mengine ni athma, kiungulia, mafuta mengi mwilini, magonjwa ya moyo na moyo kushidwa kufanya kazi na mawe katika kibofu cha nyongo.

Wagonjwa hujikuta wakishindwa kufanyakazi vyema ili kujipatia kipato, hivyo kuwa tegemezi, kunyanyapaliwa pia huleta matatizo ya kisaikologia kama nilivyoeleza awali.

Matibabu ya ugonjwa huu ni pamoja na kubadili mfumo na aina ya maisha. Hii ni pamoja na kuwa na nidhamu katika chakula na kufanya mazoezi.

Ni wazi kwamba wazazi na watoto wanaoishi mjini, wanakabiliwa na tatizo hili, kutokana na maisha ya mfumo mgando ( kula kazi bila jasho-kulala, au kula-kusoma-kulala).

Matibabu ya muda mrefu ya tatizo hili na ambayo husaidia mgonjwa kwa kiwango kikubwa ni kufanyiwa upasuaji. Upasuaji katika tumbo ndiyo tiba mwafaka kwa unene uliopindukia.

Mambo ya Msingi kujua kuhusu rangi ya mkojo wako

Je unafahamu ya kwamba rangi ya mkoja inakupa matokea sahihi kuhusu afya yako? Kama jibu ni hapana basi makala haya yanakusu wewe, kwani rangi ya mkoja kwa mujibu wa watalamu wa afya unauwezo mkubwa wa kukuoa ukweli juu ya afya yako.

1. Mweupe kabisa (Usio na Rangi):
Unakunywa maji mengi.

2. Manjano iliyochanganyika na Kijani kidogo. Ni kawaida, una afya na Mwili wako una maji ya kutosha.

3. Manjano iliyo pauka.Upo kawaida tu. Endelea kunywa maji ya kutosha

4. Njano iliyo kolea. Upo kawaida lakini unashauriwa kunywa maji ya kutosha.

5. Njano inayokaribia kufanana na Kahawia au Rangi kama ya Asali. Mwili wako hauna maji ya kutosha. Kunywa maji kwa wingi sasa.

6. Rangi ya Kahawia. Huwenda una Matatizo kwenye Ini lako au Upungufu mkubwa wa Maji mwilini. Kunywa maji ya kutosha na umwone daktari kamali hii ikiendelea.

7. Rangi ya Pinki inayokaribia kuwa kama Nyekundu. Kama hujala matunda yoyote yenye asili ya uwekundu, basi huwenda una famu kwenye kibofu chako cha mkojo. Inaweza ikawa sio ishara mbaya. Lakini inaweza ikawa ishara ya ugojwa wa Figo, uvimbe, matatizo kwenye njia ya mkojo, au matatizo kwenye kibofu. Muone daktari haraka iwezekanavyo.

Madhara ya kutumia dawa bila ushauri wa Dakitari

Mara nyingi watu wanaugua maradhi mbalimbali, lakini wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya vipimo au kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari. Kutokana na uwepo wa maduka ya dawa baridi, watu wengi wanapojisikia kuwa wagonjwa, hununua dawa kwenye maduka hayo na kuanza kuzitumia.

Ni ukweli usiopingika kuwa dawa zimetengenezwa ili kutibu maradhi fulani ambayo yatabainika kwa mgonjwa baada ya uchunguzi wa kitaalamu.

Hivyo matumizi ya dawa bila kufanya uchunguzi wa kitaalamu yanaweza kuwa na madhara makubwa kwenye afya yako

Yafuatayo ni madhara yatokanayo na kutumia dawa bila ushauri wa dactari:

1. Huweza kusababbisha kifo.

Kama nilivyoeleza kwenye hoja zilizotangulia, dawa ni sumu zinazokabili vimelea vya magonjwa. Hivyo kutumia dawa vibaya kunaweza kusababisha kifo.

Ikumbukwe pia watu wenye matatizo maalumu kama vile maradhi ya moyo pamoja na shinikizo la damu, wanapaswa kuwa makini na dawa wanazozitumia kwani zinaweza kuchochea matatizo yao na hatimaye kifo

2. Huweza kusababisha saratani.

Dawa zinapoingia mwilini mwako kimakosa na kushindwa kufanya kazi yake, zinaweza kuharibu baadhi ya seli za mwili na kuzifanya kugeuka seli za saratani. Hivyo hakikisha dawa unayoitumia ni sahihi na inalenga ugonjwa husika.

3. Husababisha usugu wa maradhi

Mtaalamu wa afya hukupa kiwango (dosage) cha dawa kulingana na vipimo alivyovifanya; hivyo kutumia dawa bila vipimo vya kitaalamu kunaweza kusababisha vimelea vya ugonjwa vizoee dawa husika na kusababisha ugonjwa huo usitibike tena.

Hili ndilo linalosababisha maradhi kama vile malaria sugu au UTI sugu. Hivyo kabla ya kutumia dawa ni vyema ukafanya uchunguzi wa kitaalamu

4. Husababisha tatizo la mzio. Allegy.

Kuna watu wenye tatizo la mzio au wengi huita β€œaleji” kwa lugha isiyo sanifu, watu hawa wanapaswa kuwa makini na kuepuka kutumia dawa bila ushauri wa kitaalamu.

Hili ni kutokana na baadhi ya dawa kutokuendana na afya zao, hivyo kusababisha tatizo lao la mzio kuibuka. Ni vyema ukamwona mtaalamu wa afya na umweleze aina ya mzio uliyo nayo ili akupe dawa stahiki.

5. Huongeza sumu mwilini.

Dawa zimetengenezwa kwa kutumia kemikali mbalimbali ambazo kimsingi ni sumu zinazoua vimelea vya magonjwa.

Hivyo kutumia dawa bila vipimo kunakusababishia kuongeza sumu za dawa hizo mwilini mwako kwani umetumia dawa ambazo mwili hauzihitaji kukabili ugonjwa husika.

Sumu hizi zinapokusanyika mwilini mwako zinaweza kukuletea athari mbalimbali za muda mfupi au hata mrefu.

Ni muhimu ukumbuke kuwa dalili za ugonjwa mmoja zinaweza kuwa dalili za ugonjwa mwingine pia. Hivyo ni muhimu kufanya uchunguzi pamoja na kutafuta ushauri wa kitabibu kabla ya kutumia dawa zozote kutibu maradhi yanayokukabili.

Umuhimu wa kula fenesi kiafya

Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee huku likiwa na ladha tamu isiyomithilika. Licha ya sifa hii, tunda hili linatajwa kuwa na faida lukuki endapo litaliwa na mwanadamu.

Kwanza, linatajwa kuwa na virutubisho kadha wa kadha vyenye kazi mbalimbali mwilini. Baadhi ya virutub
isho hivyo ni pamoja na vitamini za aina mbalimbali, madini, protini, mafuta, uwanga na nyuzinyuzi.

Fenesi pia linatajwa kuwa chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na lehemu. Si hivyo tu, bali pia ni chakula chenye virutubisho vya kuondosha sumu mwilini vinavyoweza kuukinga mwili dhidi ya saratani na magonjwa mengine kadha wa kadha.

Uwepo wa viondosha sumu ndani ya tunda hili kunasaidia pia kuongeza uwezo wa kuona. Tunda hili pia linatajwa kuwa na kiasi kikubwa cha madini ya potassium yanayosaidia kuimarisha mifupa na afya ya ngozi.

Wataalamu wa mambo ya afya wamezitaja faida nyingine za tunda hili kuwa ni pamoja na:

Kinga:

Fenesi ni chanzo kizuri cha vitamini C. Uwepo wa kiasi kikubwa cha vitamini hiyo pamoja na viondosha sumu kunaongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini. Husaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi.

Nishati:

Ni tunda salama kiafya, halina lehemu licha ya kuwa na kiasi kikubwa cha mafuta. Pia, lina wanga na kalori kwa kiasi kikubwa. Sukari iliyomo ndani yake huchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mwili.

Hurekebisha msukumo wa damu na pia husaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula tumboni pamoja na kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na kupooza.

Asthma:

Inasadikika pia kuwa tunda hili lina uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa pumu.
Si hivyo tu, fenesi lina vitamini muhimu katika utengenezaji wa damu mwilini.

Mwanamke kuamka mapema asubuhi kunapunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti

Kuamka asubuhi na mapema hupunguza uwezekano wa mwanamke kupata saratani ya matiti.

Kulingana na shirika la habari la BBC,wataalamu wa chuo kikuu cha Bristol nchini Uingereza wamewafanyia tathmini wanawake 400,000 na kutambua kuwa sio rahisi kwa mwanamke anaeamka asubuhi na mapema kupata saratani ya matiti.

Utafiti huo umeoneysha kuwa wanawake wanaoamka wamechelewa wana hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo ukilinganisha na wale wanaoamka wamechelewa.

Utafiti wa hapo awali ulionyesha kuwa kufanya kazi mpaka usiku wa manane kunaongeza hatari ya kupata saratani.

Matokeo ya utafiti huo yatawasilishwa kwenye Mkutano wa Taifa wa Taasisi ya Utafiti wa Saratani huko Glasgow.

Vyakula vya kukusaidia kupunguza uzito

Kuchagua vyakula sahihi kwa mlo wako inaweza kuwa changamoto na tungependa kuamini kwamba kupungua uzito ni jambo tu la kula kalori chache na kufanya mazoezi zaidi. Hata hivyo, si mara zote zoezi hili linakuwa rahisi. Kama ni lengo lako kupunguza uzito, kuchagua chakula gani ule ni muhimu kama kuchagua kiasi gani cha chakula ule.

Ukweli ni kwamba , baadhi ya vyakula vinauwezo wakusaidia kupunguza uzito kutokana na tabia zake za kuunguza mafuta mwilini.

Vifuatavyo ndivyo vyakula vinavyosaidia kupunguza uzito:

Mafuta ya Nazi

Mafuta ya nazi yanapanda chati kwa haraka kabisa na kufanya kuwa mojawapo ya vyakula bora kabisa kwa afya ya binadamu.

Mojawapo ya vitu muhimu kabisa katika mafuta haya ni uwezo wake wa kupunguza uzito wa mwili.

Mafuta ya nazi ni yana kemikali yenye mlolongo wa kati wa mafuta (β€œMedium Fatty Chain Acids”) ambayo humeng’enywa tofauti na yale yenye mlolongo mrefu wa mafuta (β€œLong Fatty Chain Acids”)

Kemikali zenye mlolongo mrefu wa mafuta(β€œLong Fatty Chain Acids”) hupatikana kwa wingi katika vyakula vingi vya mafuta kaa vile nyama, chips n.k.

Kemikali zenye mlolongo wa kati wa mafuta hutumiwa na mwili kwa ajili ya nishati badala ya kuhifadhiwa kama mafuta katika mwili.

Hii ndio sababu mafuta ya nazi ni moja ya vyakula vyenye uwezo wa kuchoma mafuta mwilini na kusaidia kupungua uzito.

Siki ya Apple (Apple Cider Vinegar)

Siki ya Apple ina kiwango kikubwa cha kemikali za amino (amino acids) ,kemikali za kumeng’enya chakula na madini na vitamini. Utafiti unaonyesha kwamba kutumia Siki ya Apple kabla ya kula vyakula vya wanga inasaidia kupunguza kupanda kwa insulin hivyo kusaidia kutopata hamu ya kula mara kwa mara.

Ndimu na Limao

Utafiti unaonyesha kuwa kiasi cha vitamini C mwilini kinahusiana na uzito wa mwili.

Watu wenye viwango vya kutosha wa vitamini C wana uwezo wa uwezo wa kuvunja asilimia 30 zaidi ya mafuta wakati wa mwili unapofanya shughuli za nguvu kama kazi za nyumbani,shambani na mazoezi kama kutembea, kuliko wale walio na kiwango cha chini cha vitamini C.

Kama una dhamira ya kupungua uzito, basi fikiria kuanza siku yako kwa kunywa glasi moja ya maji yenye ndimu au limao au anza kutumia siki(vinegar) kwenye kachumbali au saladi unapokula chakula.

Balungi

Balungi yana kiasi kidogo cha kalori , kiwango cha juu cha tindikali za kumeng’enya chakula na inaweza kukufanya usijisikie njaa kwa muda mrefu.

Watafiti wamegundua kwamba kula nusu ya balungi kabla ya mlo ni inachangia sana kupoteza uzito . Pia kula nusu tu ya balungi kabla ya mlo inaweza kusababisha kupungua kwa kiasi cha glucose-insulin katika muda wa masaa mawili tu.

Kama wewe unahitaji kupungua uzito zingatia kula vyakula vinavyo kata mafuta na ongeza vyakula hivi vilivyotajwa katika mlo wako.

Kwa mafanikio ya muda mrefu , kazania kula vyakula kamili (vyakula visivyo kobolewa au kusindikwa) na kufanya mazoezi ya mara kwa mara.

Vyakula 7 vya kuepuka kula ili uwe na afya nzuri

Inasemwa kuwa β€œwewe ni kile unachokula” kwa kumaanisha kuwa mwonekano wetu na afya ya mwili na akili unajengwa na chakula tunachokula. Madhara ya chakula chetu tunachotumia yako pia katika ngozi. Kuna vyakula vinavyozeesha ngozi kwa haraka na ni budi kuvijua na kuviepuka.

Vyakula hivi japo tunavipenda sana lakini vina athari mbaya kwa miili yetu na muhimu kujenga tabia ya kuviacha katika milo yetu. Kama si rahisi kuacha kabisa basi angalau kupunguza matumizi yake.

Vifuatavyo ni vyakula 7 vinavyozeesha ngozi na unashauriwa kuvitoa katika mlo wako:

1. Nyama Nyekundu
Mojawapo ya vyakula vinavyozeesha ngozi ni nyama hasa nyama nyekundu. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa nyama nyekundu inayotokana na wanyama kama ng’ombe,mbuzi,kondoo,nguruwe n.k ni mbaya kwa afya njema ya binadamu na hivyo kwa ngozi pia. Nyama nyekundu ina kemikali aina ya carnitine ambayo inafanya mishipa ya damu kukakamaa na kusababisha kuzeeka kwa ngozi.

Hivyo nyama nyekundu ni mojawapo ya vyakula vibaya kwa afya ya binadamu na vya kuvizuia.

2. Chumvi

Chumvi hasa yenye madini ya iodine ni mbaya sana kwa afya ya ngozi. Inasababisha chembechembe za nyama katika ngozi kuvimba.

3. Sukari

Sukari japo tunaipenda sana ni adui mkubwa wa afya ya binadamu. Inadhoofisha mfumo wa kinga za mwili. Kiasi kingi cha sukari mwilini kinafanya ngozi kuwa kavu na kufanya mwili utengeneze makunyazi kwa sababu inaharibu kemikali ya collagen na elastin ambazo zinafanya kazi ya matengenezo ya ngozi kuifanya isiharibike na kuwa chakavu.

Sukari nyingi inasababisha mwili kukosa nguvu ya kupambana na bacteria wabaya. Ongezeko la bacteria hawa kunafanya utengenezwaji wa kemikali mbaya ambazo husababisha uchakavu wa ngozi.

Watu wanashauriwa kutumia sukari asilia kama ya matunda na asali kuliko zile zinazopatikana katika vinywaji kama soda na pipi , jojo,biskuti au vitafunwa vingine vyenye sukari ya kuongeza.

4. Vyakula vya Kukaangwa

Vyakula vya kukaangwa kama chipsi,nyama za kukaanga vinasababisha uingizaji wa mafuta mengi mwilini. Mafuta haya yenye vitu vinavyoitwa β€œFree Radicals” yanasababisha uzibaji wa vijitundu katika ngozi. Ukiachia ngozi mafuta mengi mwilini yanasababisha madhara mengi mengine yakiwemo magonjwa ya moyo na kisukari.

5. Mkate Mweupe,Tambi na Keki

Vyakula hivi vina kemikali ya glucemic kwa kiwango kikubwa ambayo inaleta madhara ya magonjwa ya ngozi (Ugonjwa wa madoa katika ngozi)

6. Pombe

Unywaji wa pombe unasababhisha kupoteza maji mengi mwilini kwa njia ya mkojo na huleta madhara mabaya kwa ngozi kwa kuifanya iwe kavu.

7. Kahawa (Caffeine)

Kemikali ya caffeine iliyomo katika kahawa na vinywaji vingine inasababisha ukosefu wa maji ya kutosha katika ngozi na kuifanya iwe kavu. Lakini pia caffeine inasababisha utengenezwaji wa kemikali ya cortisol ambayo inachangia uzeekaji wa ngozi.

Badilisha Tabia Yako ya Ulaji

Vyakula hivi ni baadhi ya vingi ambayo vimo katika ulaji wetu wa kila siku na una madhara makubwa kwenye ngozi zetu. Wanawake wanaathirika sana na ngozi ukilinganisha na wanaume. Au niseme wanajali sana ngozi zao kuwa zenye afya na kuvutia kuliko wanaume hivyo wanaweza kufaidika sana kwa kupunguza au kutotumia kabisa hivi vyakula vinavyozeesha ngozi.

Fahamu kuwa afya yako ni mtaji mkubwa hivyo ni kitu muhimu kuipa afya ya mwili wako kipaumbele na hivyo zingatia ulaji wako.

Mambo ya msingi kufahamu kuhusu uotaji wa meno kwa mtoto

Mtoto wako atakapofikisha miezi sita, ataanza kuota meno. Watoto wengi wanapotaka kuota meno humwaga mate sana na hutaka kutafunatafuna vitu. Wakati mwingine watoto hutapika au kuhara wakiota meno.

Kwa kawaida kuota meno hakufanyi mtoto kupandwa na joto. Kama mtoto wako atapata joto, yaweza kuwa jambo lingine. Hakikisha umemwona daktari wa watoto.

Yafuatayo ni mambo ya msingi kujua kuhusu uotaji wa meno.

Β·Wakati wa kulala, weka kitambaa safi chini ya kichwa cha mwanao ambapo ute utamwagika. Unaweza kibadilisha kitambaa hichi kitakapo loweka ute.

Β·Mpatie mtoto kitu cha kutafuna ambacho hakitamdhuru. Usimpatie kitu kidogo sana kwani anaweza kukimeza. Unaweza kumpatia vidunde vya mpira visivyokuwa na majimaji ndani kwani vyaweza kupasuka.

Β·Usifungilie kidunde cha kutafuna kwa shingo ya mwanao. Kinaweza kushikwa na kummyonga.

Β·Kuna dawa nyingi dukani za kupiunguza maumivu wakati mwanao anaota meno. Hata hivyo, mwone daktari wa watoto kabla jujampa mwanao dawa yoyote

Β·Baada ya mwanao kuota meno hakikisha unayatunza vizuri

Mambo 9 ya kuzingatia kuepuka ugonjwa wa saratani au Kansa

Tafiti nyingi zilizolizofanywa zinaonesha kuwa sababu kuu zinazosababisha saratani ni mtindo wa maisha usiofaa kama ulaji usiofaa na kutofanya mazoezi ya mwili.
Ili kuepukana na ugonjwa wa saratani au kupunguza uwezekano wa kupata saratani ni muhimu kuzingatia yafuatayo:

1. Kula zaidi vyakula vya mimea na nafaka zisizokobolewa

Matokeo ya tafiti yanaonesha kuwa vyakula hivi vinapunguza uwezekano wa kupata saratani, Hakikisha unakula mboga mboga za kijani na rangi nyingine kama njano,zambara. Kula nafaka zisizokobolewa kama unga wa dona, mchele wa brauni,unga wa ngano usiokobolewa,mtama na ulezi.

2. Kuwa na Uzito Uliosahihi

Uzito mkubwa uliopitiliza ni hatari na husababisha saratani. Hakikisha uwiano wa urefu na uzito wako (BMI- Body -to-Mass Index) ni sahihi ambayo ni 18 -25 kwa mtu mzima na mwenye afya nzuri unashauriwa kuwa na uwiano wa 21-23.

Punguza vyakula vinavyonenepesha mwili kama vyenye mafuta na sukari kwa wingi. Vyakula vyenye mafuta kwa wingi kama chipsi na vitumbua mfano ni hatari kwa afya yako.Vyakula vyenye sukari ni kama soda,chokoleti,keki,barafu na iskrimu na juisi bandia.

3. Fanya mazoezi ya mwili

Fanya mazozi ya mwili kila siku. Dakika 15-30 tu zinatosha kufanya mazoezi kwa afya njema. Ukikosa muda fanya anagalau mara 3 kwa wiki kwa muda usiopungua dakika 30.
Kukimbia(jogging) ni njia rahisi ya kufanya mazoezi yanayohusisha mwili mzima. Ukiweza jiunge katika timu ya mpira au klabu za mazoezi ya ndani.

Tembea kwa miguu pale inapobidi. Rafiki yangu mmoja ambaye ana gari ameweka ratiba ya kutotumia gari wakati wa mwisho wa juma. Anapanda dalala na kutembea kwa sehemu kubwa. Unaweza ukafanya hivyo pia.

4. Punguza au Acha kula Nyama nyekundu.

Ukiachia mbali saratani, nyama nyekundu imetambulika kusababisha madhara mengi na makubwa kwa binadamu.

Amua sasa kuachana nayo. Hamia katika samaki na kuku kwa kuanzia na baadae huenda ukaachana na hizo nyingine pia.
Nyama ya nguruwe maarufu kam Kitimoto ni nyama nyekundu na ni hatari kwa afya yako . Heri wale ambao hata dini zao zilikataza nyama hii ya Nguruwe kwani wameepuka hatari.

5. Epukana na Nyama za kusindikwa.

Nyama za makopo na soseji zinasababisha saratani kutokana na kemikali za kutunzia zisioze na pia huwekwa chumvi nyingi sana ambayo ni hatari kwa afya.

6. Punguza Matumizi ya Chumvi

Chumvi ya kupita kiasi inaongeza uwezekano wa kupata saratani hivyo ni hatari. Tumia chumvi kwa kiasi kidogo kwa afya njema. Binadamu anahitaji gramu 5 tu kwa siku sawa na kijoko kidogo cha chai.

Usiongeze chumvi wakati wa kula,chumvi isiyoyeyuka nia hatari zaidi.

7. Acha kula Vyakula vyenye Ukungu

Acha kula nafaka na kundekunde zilizootesha ukungu hasa kwa kutohifadhiwa vyema. Vyakula hivi vinatoa sumu ya aflatoxin

8. Usivute Sigara

Uvutaji wa sigara ni hatari na huenda ukakusababishia saratani ya koo,kinywa na mapafu. Acha kuvuta sigara ili kuepukana na ugonjwa wa saratani. Fikiria kidogo,kwanini ufe kwa sababu ya moshi tu?.

9. Punguza au Acha Pombe Kabisa

Ukiacha pombe utapunguza uwezekano wa kupata saratani na hivyo kuwa salama zaidi.
Achana na pombe, kuna madhara mengi sana ya kunywa pombe ukiachia ya saratani.

Badilisha Mtindo wa Maisha na Uwe Salama na Saratani
Namna ya kuishi kunachangia kwa kiasi kikubwa kupata saratani au la. Chagua mtindo ulio bora na salama kama ilivyoshauriwa katika mada hii juu ya kuepukana na ugonjwa wa saratani.

Afya yako ni jukumu lako mwenyewe na kupanga ni kuchagua. Panga kuishi mtindo wa maisha ulio bora na salama chagua kuishi bila saratani.

Mchanganyiko wa asali na mdalasini una faida hizi

Mchanganyiko wa mdalasini na asali unasaidia katika mambo ya aiana tofauti tofauti kama ifutavto:

Kuvu au fungus miguuni

Changanya kijiko kimoja cha asali, vijiko viwili vya mdalasini na upake kwenye sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji fufutende.

Maumivu ya jino

Changanya vijiko viwili vya asali na kijiko kimoja cha mdalasini na utumia kukupunguzia maumivu ya jino.

Mafua

Tumia kijiko kimoja cha asali iliyochanganywa na robo kijiko cha mdalasini, mchanganyiko huu husaidia kuondoa chafya na kuvimba kwa koo.

Tumbo kusokota

Asali imetambuliwa kwa kipindi kirefu kwamba ni dawa ifaayo kuondoa kadhia ya tumbo kuchafuka. Unachohitaji kufanya ni kuongeza kiasi kidogo cha mdalasini kwenye asali na uchanganye kisha uongeze maji kikombe kimoja na unywe mchanganyiko huu.

Ugonjwa wa viungo

Tumia mchanganyiko wa kijiko kimoja cha asali, vijiko viwili vya maji ya ufufutende na kijiko 1 cha mdalasini na upake kwenye sehemu zilizoathirika.

Kukatika kwa nywele

Changanya asali, mdalasini na mafuta ya mizeituni kisha upake mchanganyiko huo kichwani na uache kwa dakika 15 kabla ya kuosha nywele zako.

Mbinu 11 za kufuata ili uweze kuacha pombe

Pombe ni kinywaji kinachotumiwa na watu wengi pasipo hata kufahamu athari zake. Pombe ina athari mbalimbali kiafya na kisaikolojia. Wengi baada ya kuathiriwa na pombe hutamani kuacha matumizi ya pombe lakini ni wachache tu ndiyo hufanikiwa katika hili.

Mwingereza Matt Haig ambaye ameandika kitabu kilichouzika sana cha β€˜Reasons to Stay Alive’ anasema yeye akinywa pombe humletea wasiwasi hofu na uoga anatoa ushauri wa namna ya kufanya ili asinywe pombe.

β€œHata kama watu hawakulazimishi kunywa nafsi yako tu inajisuta ni kama vile watu wasiokula nyama halafu umekaa kati yao unakula unajiona kama unawakosea unaweza ukajiondoa hapo,” anasema Haig.

Jinsi ya Kuacha Pombe Tumia Mbinu hizi

1. Epuka watu watakaokushawishi kunywa pombe

Mara nyingi kama wewe unapenda kunywa pombe utakuwa na marafiki wanaokunywa pombe pia.

Ni wazi kuwa marafiki wanaokunywa pombe watakuhimiza kunywa hata kwa kukununulia au hata pengine kukukebehi na kukubeza juu ya uamuzi wako wa kuacha pombe.

Hivyo ikiwa unataka kuacha kunywa pombe ni lazima uepuke marafiki au watu wanaoweza kukushawishi kunywa pombe. Unaweza kutafuta marafiki wengine au watu wengine ambao hawatakatisha lengo lako la kuacha pombe.

2. Epuka mazingira yatakayokusababisha kunywa pombe

Ikiwa kuna mazingira yanayoshawishi kunywa pombe basi yaepuke. Inawezekana ni nyumbani kwa rafiki zako, hotelini, baa n.k; ikiwa unataka kuacha kunywa pombe basi huna budi kuepuka mazingira haya ambayo yatakushawishi kunywa pombe.

Kwa mfano Unaweza kujizoeza kukaa kwenye migahawa au hoteli ambazo hazina pombe ili usije ukajikuta umeshashawishika kuendelea kutumia pombe.

3. Usiweke pombe nyumbani au sehemu unayokaa

Kama unatabia ya kuweka pombe nyumbani, sasa inakupasa kuacha mara moja. Hata kama kuna mtu huwa analeta pombe nyumbani unaweza kumwomba kuwa wewe umekusudia kuacha pombe hivyo asilete pombe nyumbani. Kwa kufanya hivi utapunguza hatari ya kushawishika kuendelea kunywa pombe.

4. Wajulishe watu unaacha pombe

Unapowajulisha watu kuwa unaacha pombe ni rahisi zaidi wao kukusaidia wewe kuacha kunywa pombe. Tafuta watu ambao unahisi wanaweza kukusaidia na kukutia moyo katika mkakati wako huu wa kuacha pombe. Kuwajulisha watu pia kutakuhimiza kuacha kwani utaona aibu kwani umeshawatangazia watu unaacha, hivyo kuendelea ni kujiaibisha wewe mwenyewe.

5. Tatua matatizo ya kihisia na kiakili.

Mara nyingi wanywaji wa pombe hasa wale waliopindukia, hunywa kutokana na matatizo ya kihisia au kiakili yanayowakabili. Wengi huwa na majeraha kwenye maswala ya kifamilia au mahusiano, kazi, au hata kiuchumi.

Unaweza kutafuta suluhisho la matatizo haya kwa kuomba ushauri na msaada wa utatuzi kwa washauri nasaha ili kuepuka kunywa pombe kwa kisingizio cha kupoteza mawazo.

Kumbuka pombe huwa haiondoi matatizo haya bali hukufanya kuyasahau kwa muda tu; ikumbukwe kuwa hata wakati mwingine pombe hukusababishia kuyaongeza zaidi.

6. Tafuta kitu mbadala cha kufanya

Ikiwa kuna muda fulani ambao huwa unautumia kwa ajili ya kunywa pombe, basi yakupasa kubadili matumizi ya muda huo. Unaweza kujipangia shughuli nyingine yenye tija kwenye maisha yako kama vile, mazoezi, utunzaji wa bustani, kusoma vitabu, kutazama filamu, kusikiliza mziki, kutunza mazingira n.k. Kwa kufanya hivi utaweza kubana muda wako unaoutumia kwenda kunywa pombe.

7. Weka malengo tekelevu ya kuacha

Wengi hushindwa kuacha pombe kwa sababu hawana malengo yanayotekelezeka ya kuacha pombe. Kwa mfano unaweza kujiwekea mpango huu:

Nitaanza kuacha kwa kunywa chupa mbili tu kwa wiki.
Kisha nitapunguza na kunywa chupa moja kwa wiki
Na hatimaye nitaacha kabisa kwa wiki
Tarehe fulani (00/00/0000) ni lazima niwe nimeacha kabisa.

Ukijiwekea malengo kama haya na ukahakikisha unafanya juu chini kuyatimiza, hakika utaweza kuacha pombe kabisa.

8. Jipongeze wewe mwenyewe kwa kipindi ulichoweza kuacha pombe

Kujipongeza wewe mwenyewe kunakupa hamasa ya kufanya jitihada zaidi katika mpango wako wa kuacha pombe. Kwa mfano ikiwa umeweza kukaa wiki moja bila kunywa basi jipongeze kwa hatua hii na ujitahidi sasa kukaa mwezi au hata mwaka bila kunywa.

9. Usikae na pesa za ziada

Mara nyingi watu wengi hununua pombe kwa sababu wana pesa mfukoni; wanapokuwa hawana pesa hawalewi kabisa. Jambo hili linaweza kuzuilika kwa kubadili mfumo wako wa kutunza pesa. Unaweza kufanya mambo yafuatayo:

Ikiwa unalipwa pesa kila siku, omba upokee malipo kwa mwezi badala ya kila siku. Ikiwa hili haliwezekani unaweza kumwomba mtu unayemwamini akutunzie pesa zako.
Tunza pesa zako kwenye mifumo ya kutunza pesa kama vile benki na simu za mkononi. Kwa kufanya hivi kutapunguza pesa ulizo nazo mkononi.
Kumbuka njia bora zaidi ni kumwomba mtu unayemwamini akutunzie pesa zako na akukabidhi tu pale unapokuwa na hitaji muhimu. Ikiwa una mwenzi mwaminifu anaweza kukusaidia sana kwa hili.

10. Jikumbushe na kutafakari madhara ya pombe

Unapotafakari madhara ya pombe kama vile matatizo ya kiafya, kisaikolojia, kijamii na hata kiuchumi ni wazi kuwa hili litakuhimiza zaidi kuacha pombe. Tafakari madhara ya pombe na uone kuwa unapokunywa pombe unayapata. Kwa kufanya hivi utajijengea fikra za kujitahidi kuacha pombe ili uepuke madhara hayo.

11. Tafuta usaidizi na ushauri wa kuacha pombe

Zipo taasisi na watu mbalimbali wanaowashauri watu walioathirika kwa matumizi ya pombe. Inawezekana ni asasi ya kiraia, kituo cha ushauri nasaha au hata taasisi au kiongozi wa kidini; hawa wote wanaweza kukushauri na kukutia moyo katika mkakati mzima wa kuacha kunywa pombe.

Madhara ya kunywa maji baridi na faida za kunywa maji moto na asali

UNYWAJI wa maji baridi, hasa katika joto kali kama la Dar es Salaam, ni kiburudisho kikubwa cha koo na huleta faraja kubwa mwilini. Ni jambo la kawaida pia kwa mtu kuhitaji kunywa maji hayo mara baada ya kula mlo, iwe mchana au usiku.

MADHARA YA KUNYWA MAJI BARIDI

Pamoja na ukweli kwamba maji baridi ni;matamu’, lakini siyo mazuri kwa afya yako na katika makala ya leo tutaangalia ukweli kwa nini maji haya siyo mazuri.

Kwa mujibu wa utafiti uliokwisha fanywa na wataalamu wetu wa masuala ya lishe, mtu anapokunywa maji baridi mara baada ya kula chakula, maji yale yanapopita kwenye utumbo huchangia kugandisha mafuta yaliyomo kwenye chakula.

Kitendo hicho, husababisha usagaji wa chakula kuwa wa taratibu sana na hivyo kuchangia ukosefu wa choo. Mbali na ukosefu wa choo, ambao ni madhara yanayojionesha kwa muda mfupi, lakini pia kuna madhara ya muda mrefu yanayoweza kujitokeza baadaye sana.

Inaelezwa zaidi kuwa, wakati chakula kinapochelewa kusagwa kwa sababu ya kuganda kulikosababishwa na maji baridi, chakula hicho hukutana na ;acid’ iliyoko tumboni ambayo huanza kuyayusha mafuta hayo haraka na kufyonzwa na utumbo kabla ya chakula chenyewe.

Hali hii inapoendelea kwa muda mrefu, tabaka la mafuta (fats) hujijenga kwenye utumbo na baadaye huweza kusababisha saratani ya utumbo. Hali kadhalika, huweza kuwa chanzo kingine cha ugonjwa wa moyo ambao madhara yake ni pamoja na kupatwa na Kiharusi na hatimaye kifo.

Ili kuepuka hatari hii, unachotakiwa kufanya ni kuacha tabia ya kunywa maji baridi na badala yake pendelea kunywa maji ya uvugu-vugu mara baada ya kula chakula. Vile vile zingatia ushauri wa kukaa kwa muda usiopungua nusu saa ndiyo unywe maji.

MAJI MOTO NA ASALI KAMA DAWA

Kujiweka katika mazingira mazuri ya kuhakikisha unasafisha tumbo lako kila siku kabla ya kulala, weka utatartibu wa kunywa maji moto kiasi, yaliyochanganywa na asali.

Chemsha maji moto au chukua maji moto yaliyopo kwenye chupa ya chai, acha yapoe kidogo na kuwa ya uvuguvugu, kisha weka kijiko kimoja cha asali mbichi kunywa kisha lala. Kunywa maji hayo nusu saa au zaidi baada ya kula chakula cha mwisho.

Kitendo hicho kitakuwezesha kuyeyusha mafuta, kusadia usagaji wa chakula tumboni na hivyo kukuwezesha kutoa uchafu na sumu mwilini kwa njia ya haja kubwa. Kwa utaratibu huu, hutakaa na uchafu tumboni wala mrundikano wa mafuta mabaya mwilini.

Ni jambo lisilo shaka kuwa iwapo kila mmoja wetu atazingatia kanuni za ulaji na unywaji sahihi, bila shaka matatizo ya moyo na shinikizo la damu yanaweza kupungua kwa kiwango kikubwa, kama siyo kutoweka kabisa.

Mambo ya kufanya unapostuka usiku ili kulinda afya yako

Kumekuwepo na tatizo la vifo vya ghafla sana tena kwa watu ambao wana afya njema na hii inatokana na kuamka ghafla usiku ambapo ubongo hukisa damu ya kutosha.

Unapoamka katikati ya usiku kwenda kujisaidia haja ndogo mfumo wa damu unakuwa umebadilika. Kwa sababu kuamka ghafla kunakuwa hakuna mzunguko wa kupisha damu kwenye ubongo unaosababisha moyo kushindwa kufanya kazi kutokana na ukosefu wa damu.

Ushauri:tumia dakika 3 na nusu kufanya yafuatayo unapostuka usiku
1. Unapoamka usingizini lala kitandani kwa nusu dakika.
2. Kaa kitandani kwa takribani nusu dakika.
3. Shusha miguu, kaa pembeni ya kitanda takribani nusu dakika.

Baada ya dakika 3 na nusu hutakuwa na tatizo la ukosefu wa damu kwenye ubongo na moyo kushindwa kufanya kaz, kufanya hivi husaidia kupunguza uwezekano wa vifo vya ghafla na kuanguka ghafla.

Ushariwa kuwashirikisha watu wengine somo hili, kwanii Kushare ni kujali na kumsaidia mtu mwingine ili asipate elimu hii .Kama tayari ulikuwa unajua hili lichukulie kama kumbukumbu kwani jambo hili Inatokea bila kujali umri.

Shopping Cart
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About