Mapishi ya bagia na chatney ya machicha ya nazi

Mahitaji

Kunde (Ila mimi nilitumia Nigerian brown beans 1/2 kilo)
Vitunguu maji (onion 2)
Pilipili (scotch bonnet pepper 2)
Vitunguu swaum (garlic 4 cloves)
Chumvi (salt)
Barking powder (1/2 kijiko cha chai)
Machicha ya nazi (grated coconut 1 kikombe cha chai)
Limao (lemon 1)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Loweka kunde usiku mzima kisha ziondoe maganda na uzitie kwenye blender pamoja na vitunguu maji, vitunguu swaum, pilipili, chumvi,barking powder na maji kiasi. Visage vitu vyote mpaka viwe laini na kisha uutoe na kuweka kwenye chujio ili uchuje maji. baada ya hapo zikaange katika mafuta mpaka ziwe za brown na uzitoe na kuziweka kwenye kitchen towel ili zichuje mafuta.Baada ya hapo saga machicha ya nazi,limao, pilipili chumvi pamoja na maji kidogo na hapo chatney yako itakuwa tayari kwa kuseviwa na bagia.

Mapishi ya Bagia dengu

Mahitaji

Unga wa dengu (gram flour 1/4 kilo)
Kitunguu kilichokatwa (onion 2)
Hoho (green pepper 1/2)
Pilipili iliokatwakatwa (scotch bonnet pepper 1/2)
Barking powder (1/4 ya kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Kitunguu swaum (garlic cloves 2)
Mafuta ya kukaangia (vegetable oil)
Binzari manjano (turmeric 1/4 ya kijiko cha chai)

Matayarisho

Changanya unga, chumvi, binzari, barking powder kwanza kisha weka maji kiasi na vitu vyote vilivyobakia (isipokuwa mafuta) na ukoroge vizuri kuhakikisha unga hauna madonge.Hakikisha unga hauwi mzito wala mwepesi sana. Kisha uache kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo choma bagia katika mafuta. Ukiwa unachoma hakikisha bagia zinakuja juu ya mafuta na hazigandi chini. Ikitokea zinaganda chini hapo itakuwa umekosea kitu. Pika mpaka ziwe za light brown kisha zitowe na uziweke katika kitchen towel ili zikauke mafuta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Mandazi Matamu

Mahitaji

Unga wa ngano (nusu kilo)
Sukari (Kikombe 1 cha chai)
Chumvi (nusu kijiko cha chai)
Hamira (kijiko kimoja cha chai)
Yai (1)
Maziwa ya unga (vijiko 2 vya chakula)
Butter (kijiko 1 cha chakula)
Hiliki (kijiko1 cha chai)
Maji ya uvuguvugu ya kukandia
Mafuta ya kuchomea

Matayarisho

Tia unga kwenye bakuli kisha tia sukari, chumvi, yai, maziwa ya unga, butter na hiliki kisha uchanganye pamoja mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia maji ya uvuguvugu kiasi na uanze kuukanda. Ni vizuri ukaukanda kwa muda wa dakika 15 ili kuhakikisha donge lote la unga limelainika vizuri.
Baada ya hapo Tawanyishaa unga uliokwandwa katika madonge 4. Tia unga wa ngano kidogo katika kibao cha kusukumia na uanze kusukuma donge moja katika shape ya chapati na hakikisha haiwi nyembamba sana wala nene sana yani inatakiwa iwe ya wastani.Ukishamaliza kusukuma unatakiwa ukate shape uipendayo na uyatandaze katika kitu kilichopo flat na kiwe kimenyunyuziwa unga wa ngano ili kuyazuia yasigandie. Rudia hiyo process kwa madonge yote yaliyobakia. Baada ya hapo yaweke mandazi katika sehemu iliyokuwa na joto ili yaweze kuumuka (inaweza kuchukua masaa 3 kuumuka). Yakisha umuka unatakiwa uweke mafuta katika karai la kuchomea. Yakisha pata joto la kiasi unatakiwa utumbukize mandazi na unaze kuyachoma mpaka yawe ya brown. Yakisha iva yaipue na uyaweke kwenye kitchen towel iliyakauke mafuta. Yakisha poa yatakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya Kujaza nywele kwa njia za Asili

Zingatia mambo haya yafuatayo;

  1. Chukua parachichi kubwa moja, asali vijiko vitatu na kiini cha yai.
  2. Osha nywele zako kwa shampoo na uzikaushe.
  3. Ponda ponda parachichi mpaka lilainike kabisa. Chukua vijiko vitatu vya asali na kiini cha yai kisha changanya yote kwa pamoja.
  4. Paka mchanganyiko huo kaa nao kwa muda wa dakika 15 kisha osha.
  5. Fanya hivyo kwa muda wa wiki moja hadi mbili na utaweza kuona matokeo mazuri katika nywele yako

Mapishi ya Viazi vitamu na kachumbari

Mahitaji

Viazi utamu 3
Nyanya 2 kubwa
Kitunguu
Tango
Limao
Chumvi
Pilipili
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Menya viazi na kisha vikate katika vipande. Tia mafuta kwenye chuma cha kukaangia, yakisha pata moto tia viazi nauviache vikaangike mpaka upande mmoja uwe wa brown na kisha geuza upande wa pili na upike mpaka uwe wa brown. Vikisha iva ipua na uweke kwenye kitchen towel ili vikauke mafuta.
Kachumbali: Katakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili tango na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja .Baada ya hapo viazi na kachumbali vitakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kupika Eggchop

Mahitaji

Mayai yaliochemshwa 4
Nyama ya kusaga robo kilo
Kitunguu swaum
Tangawizi
Limao
Chumvi
Pilipili
Breadcrambs
Carry powder
Binzari nyembamba ya unga
Yai moja bichi
Mafuta

Matayarisho

Marinate nyama na pilipili, kitunguu swaum, tangawizi, limao, chumvi, carry powder, binzari nyembamba na breadcrambs pamoja. Kisha vunja yai moja bichi kwenye kibakuli na ulikoroge kisha tia kwenye mchanganyiko wa nyama.Gawanisha matonge manne kwa ajili ya kuzungushia kwenye mayai .Chemsha mayai kwa muda wa dakika 20. Yakisha iva acha yapoe na kisha yamenye maganda na uyaweke pembeni. Baada ya hapo chukua yai moja lililochemshwa na ulizungushie donge moja la mchanganyiko wa nyama. fanya hivyo kwa mayai yote yaliobakia. Baada ya hapo paka mafuta kwa nje ya hizo eggchop na kisha paka mafuta kwenye sinia la kuokea na uziokee kwenye oven kwa moto wa kawaida, kwa muda wa dakika 20.Na eggchop zako zitakuwa tayari kwa kuliwa

Jinsi ya kupika Mitai

VIAMBAUPISHI

Unga wa ngano 1Β 1/2 Kikombe

Baking powder 1 Kijiko cha chai

Baking soda ΒΌ Kijiko cha chai

Chumvi Β½ kijiko cha chai

Sukari 1 kijiko cha supu

Hamira 1/2 Kijiko cha supu

Yai 1

Maziwa Β½ Kikombe

Mafuta ya kukaangia

VIAMBAUPISHI:SHIRA

Sukari 1 Kikombe

Maji Β½ Kikombe

Iliki au Mdalasini ΒΌ kijiko cha chai (ya unga)

MAANDALIZI NA JINSI YA KUPIKA

1. Kwenye bakuli, changanya pamoja unga, baking powder, baking soda, chumvi, sukari na hamira.

2. Katika kibakuli, piga mayai na maziwa pamoja.

3. Changanya mchanganyiko wa mayai na wa unga ; na ukande kama unga wa maandazi.

4. Ikisha fura, sukuma unga kama wa maandazi na ukate mitai .

5. Pasha moto mafuta na uchome hadi iwe rangi ya dhahabu, upande zote mbili.

6. Ipikie shira lakini isiwe nzito .

7. Tia mitai na upepete hadi sukari ienee kote na zitakuwa tayari kuliwa.

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tende Na Ufuta

MAHITAJI

Unga – 3 Vikombe vya chai

Baking powder – 1 Β½ Vijiko vya chai

Sukari – 1 Kikombe cha chai

Siagi – 1 Kikombe cha chai

Mayai – 2

Maji – kiasi ya kuchanganyia

Tende – 1 Kikombe

ufuta – ΒΌkikombe

MAPISHI

  1. Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika bakuli
  2. Tia mayai, na maji kidogo uchanganye vizuri.
  3. Sukuma kiasi kama unavyosukuma chapati duara kubwa.
  4. Tandaza tende juu yake halafu kunja hadi mwisho.
  5. Paka mayai juu yake halafu mwagia ufuta kisha kata kata vipande.
  6. Vipange kwenye treya ya oveni kisha choma(bake)moto wa 350Β°F kwa muda wa nusu saa takriban.
  7. Ziepue katika moto naziache zipowe. Panga katika sahani.

Jinsi ya kutengeneza Visheti Vyeupe Na Vya Kaukau

VIAMBAUPISHI

Unga – 4 Vikombe vya chai

Siagi – 1 Kikombe cha chai

Hiliki Β½ Kijiko cha chai

VIAMBAUPISHI:SHIRA

Sukari – 2 Vikombe vya chai

Maji – 1 Kikombe cha chai

Vanilla Β½ Kijiko cha chai

(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.

JINSI YA KUTENGENEZA

Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.
Changanya vizuri isiwe na madonge.
Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.
Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.
Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .
Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili
Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.
Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai.
Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.

Uvaaji wa Tai na Maana yake

Wachambuzi wa mambo ya saikolojia wanasema kwamba kwa kuchukua tai na kulivaa ile rangi ndiyo itakayoweza kupeleka ujumbe wa wewe unataka nini au unataka watu wakutambue kwa namna gani.
Wakati Joshua Blue, Makamu mkuu wa shule ya Kennedy mjini Hong Kong, anapoendesha baraza la wanafunzi anavaa tai lenye rangi ya light violet ili kumpa mamlaka.

Tai la rangi ya bluish-purple anasema ni β€œcolourful yet muted”, anaamini kwamba rangi ya bluu inawafanya wanafunzi wasiboreke wakatiw anasikiliza, anajizuia kutumia brighter purples na pinks wakati akiwa mbele ya wanafunzi.

β€œHuhitaji kuwa na rangi nyingi zinazong’aa kwani watoto watajivuruga,” anasema Blue mwenye umri wa miaka 35.

Hakika inaweza kuwa kama kichekesho lakini wataalamu wanasema kwamba uchaguzi wa rangi ya tai inasaidia sana kupeleka ujumbe unaotakiwa kwa wahusika. Na hii haijalishi ni mteja, mdau wafanyakazi au watoto.

β€œRangi hutoa aina Fulani ya ishara,” anasema David Zyla, Mwandishi mwenye makao makuu yake New York anayeandika Color Your Style.

β€œSuti ile ile inaweza kubadilishwa kimtindo yaani salamu zake kwa kubadili rangi ya tai, na kila mvao ukawa na ishara na salamu tofauti.”

Baada ya kusoma maelezo yote hayo, nikuulize je sasa unaweza kufikiria unataka kuvaa tai gani katika mkutano wako ujao.Labda nikusaidie kwa namna hii.:

Rangi nyekundu

Ni rangi Inayotawala

Si bahati mbaya au kitendo cha kubahatisha kwa wanasiasa wengi kuvaa tai lenye rangi nyekundi ndani ya suti zilizo dark na mashati mepesi.

β€œTai nyekundu inaonesha mamlaka,” anasema Mark Woodman, mchambuzi wa mambo ambaye amejifunza masuala ya huko Laurel, Maryland, Marekani. β€œKuna kitu Fulani kipo ndani ya rangi nyekundu ambacho mara zote kinajitokeza kumuimarisha mtu na kumpa mvuto wa pekee.”

Ofisa Mtendaji wa JPMorgan, Jamie Dimon huvaa tai nyekundu anapozungumza na wananchi
Hata hivyo wataalamu wanasema kwamba kuna rangi nyekundu na rangi nyekundu.Nyekundu iliyokoza kwa miondoko ambayo wazungu wanasema ni burgundy, husaidia kuleta imani na matumaini wakati ile nyekundu nyepesi na pink inakuwa zaidi onesho la ubunifu na namna ulivyo kistaili.Katika miaka michache iliyopita rangi ya pink inaweza kuonesha mshikamano na wamama anasema Woodman.

Wakati unaendesha mradi au unataka kupeleka ujumbe Fulani kwa kruu yako fikiria kuvaa tai la rangi nyekundu iliyokoza ambayo inashaini.Tai la rangi nyekundi unaweza kuwa njia bora ya kuonesha mamlaka.

Royal purples

Ross Znavor, Mtendaji katika moja ya taasisi za kifedha mjini New York yeye huvaa tai la rangi ya purple na si nyekundu katika mikutano ya kibiashara,Rangi hii huonesha kujiamini na humsaidia watu kuendelea kumkumbuka.

Anasema kuvaa tai hilo kunampatia mtu mwingine kukubali kwamba wewe unaweza kushirikiana naye na kujenga uhusiano wa kudumu.

Lindsay anasema purple, kiasili ni rangi ya utiifu na utajiri na kwa sasa inaaanza kukubalika maeneo ya kazi.

Arnold Schwarzenegger huonesha kujiamini kwa kuvaa tai rangi ya purple.

β€œWanaume wanaovaa mashati ya lighter purple na tai za darker purple, hutaka kutambulika haraka katika kundi bila kuleta ushawishi mwingine wa kipuuzi unaovuruga”.

Rangi nyeusi

Inawezekana huvai kila siku au kila mahali lakini ukivaa tai nyeusi katika mikutano ya watendaji, kwenye dhifa unakupa wewe hali ya muondoko mweroro wenye utanashati mkubwa , anasema Zyla.

Muigizaji sinema Leonardo DiCaprio huvaa tai nyeusi katika mikutano au maeneo ambayo ni ya kikazi zaidi.

Lakini ni kweli kuwa rangi nyeusi inakufanya kuwa na ujeuri wa aina Fulani na wengine wanasema kusema kwamba inakuwa overdressed katika mazingira mengi. β€œRangi hii inafaa kutotumika kama wewe unataka kuendelea kupanda ngazi, wapandisha ngazi wanaweza kufikiria kwamba wewe ni jeuri wa aina Fulani hivi,” anasema Zyla.

Ni vyema sana kama mtu atakuwa amejipatia grey shades, anaongeza Woodman. Tai la rangi ya grey linaweza kukupa mwonekano wenye mvuto mweroro usio na jeuri na usiojinata anasema Woodman.
β€œGrey iko poa, iliyotulia na ya kisasa zaidi,” anasema.Ili kuifanya iwe imetulia zaidi piga tai hili na shati ambalo ni lighter, pastel-coluored. Tafadhali angalia lighter grey shades na malizia na shaini ili kukupa muonekano ambao ni polished.

Rangi ya kijani

Rangi ya kijani ina maana nyingi kuanzia kuzaliwa upya hadi rangi ya fedha kwa mataifa Fulani.Lakini cha ajabu ni rangi yenye β€˜kelele’ nyingi katika maeneo ya kazi.
Wakati mwingine kijani inakuwa too much.

β€œJe unataka kukumbukwa akwa ajili ya tai au kama wewe binafsi?,” anauliza Woodman .Anasema kuchagua rangi ya kijani inayostahili ni kazi kubwa.Kijani inayowaka inavuruga kutokana na mwako wake na pia inakuwa na taabu sana kupata suti inayoambatana nayo au hata shati. Hata hivyo tai la light green likiwa na subtle print linaweza kuwa jema katika shati ambalo rangi yake ni neutral.
Tai ya rangi ya njano, ni tai la kiasili kwa nchi nyingi hata waingereza wanaliheshimu kwa sababu linakupa uhakika, kukuweka mng’avu na mwenye siha hasa ya kufaa.

Ni rangi inayoonesha jua, hivyo watu wengi wanaweza kuwa na kishawishi cha kuzungumza nawe kwa sababu ya ukweli kuwa ni rangi yenye mvuto wa kipekee. Kwa wengi kuvaa tai la rangi ya njano kunaonesha kwamba maisha yeye anayaangalia katika dunia chanya zaidi, anasema Eve Roth Lindsay, mshauri wa masuala ya muonekano wa Hong Kong.

Lakini kiukweli kuwa unapaswa kuwa mwangalifu usije ukafanya kosa la uasili na utamaduni wa eneo lenu inapokuja suala la rangi.

Mathalani rangi ya njano nchini india ina maananisha kwamba wewe ni mfanyabiashara wakati rangi nyeupe nchini China inamaana upo katika kipindi cha maombolezo.

Rangi ya bluu

Unahofu ya kupeleka ujumbe ambao uhuhitaji kwa kutumia tai uliyovaa yaani rangi yake?basi ni vyema ukafikiria kutumia tai ya rangi ya bluu.

Rangi hii hutumika katika matukio yote.
Rangi ya bluu ni rangi bomba kwa kuwa inawakumbusha watu anga na bahari, vitu vyenye kutuliza maisha ya binadamu anasema Lindsay.

β€œRangi ya bluu hakika ni salama zaidi kuivaa,” anasema.

Bluu inaonekana dhahiri ni rangi ya nguvu ya kimataifa

Tai ya Patterned blue hutoa hali ya kutulia na kitaalamu zaidi na inaweza kutumiwa katika mikutano ya kimataifa ya kibiashara na mazingira bila kupeleka ujumbe usiotakiwa.

Tai ya subtle blue inaweza kuwa na mvuto na kujionesha undani wakati cobalt au royal blue hukufanya ujiachie ndani ya kundi kwa namna Fulani. β€œBluu iliyokoza ni rangi ya marubani watukuka. Bluu bahari ni rangi inayoaminika, inayokupa imani na kiburi cha uwezo,” anasema Lindsay .

Kuwa rafiki na asili

β€œKabati lako likiwa na rangi rafiki za asili kama tan, kahawia, earthy colours, salmon na njano hufaa sana kwa watu wanaojishughulisha na wengine kama wafanyabiashara (mauzo), walimu na watu wa huduma mbalimbali,” anasema Lindsay.

Hakikisha kwamba tai la rangi ya kahawia haiku pekee kwani inaweza kuonesha ugoigoi katika wajihi. Hata hivyo tai la beige linaweza kukuonesha kwamba huna matatizo, yuko huru.
Epuka kuvaa tai la rangi ya udongo na shati linalofanana nalo. Na kama unataka kujishebedua na kuonekana kweli katika eneo la kazi rangi hizi za asili achana nazo kabisa.

Mapishi ya visheti vitamu

VIAMBAUPISHI

Unga – Vikombe 2

Samli au shortening ya mboga – 2 Vijiko vya supu

Maziwa ΒΎ Kikombe

Iliki – Kiasi

Mafuta ya kukarangia Kiasi

VIAMBAUPISHI :SHIRA

Sukari – 1 Kikombe

Maji ΒΎ Kikombe

Vanila Β½ Kijiko cha chai

Zafarani (ukipenda) – Kiasi

JINSI YA KUPIKA

Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine.
Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya.
Tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo.
Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi.
Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo lake.
Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta.
Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote.
Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.

Mapishi ya Mitai

VIAMBAUPISHI

Unga wa ngano – magi 2 (vikombe vikubwa)

Hamira kijiko 1 cha chai

Sukari Vijiko 2 vya supu

Maziwa ΒΎ Magi

Siagi Vijiko 2 vya supu

Mafuta ya kukaangia kiasi

VIAMBAUPISHI:SHIRA

Sukari ΒΎ Kikombe

Maji ΒΎ Kikombe

Illiki ya unga kiasi

Zafarani kiasi

JINSI YA KUPIKA

Katika bakuli, changanya vipimo vyote pamoja na ukande unga usiwe mgumu wala laini sana uwe kiasi.
Kisha fanya donge moja na iache pahali penye joto mpaka iimuke.
Halafu weka mafuta ya kukaangia kwenye moto.
Sukuma donge hadi liwe duara sio nyembamba sana, kisha katakata kama maandazi.
Mafuta ya kisha pata moto choma mittai hukuunazigeuza hadi ziwive na kugeuka rangi.
Katika sufuria tia vipimo vya shira na iache ichemke isiwe nzito sana.
Mimina mitai kwenye shira na uzipepete, kisha weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Ufuta Na Jam

VIAMBAUPISHI

Unga vikombe 2

Sukari ya kusaga 1/4 Kikombe

Siagi 250 gms

Jam kisia

Ufuta kisia

Vanilla 1 kijiko cha chai

MAPISHI

Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai, sukari na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri.
Tia baking powder, na unga na changanya kwa mkono vizuri.
Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni.
Tengeneza viduara vidogo vidogo.
Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole, kisha weka jam, halafu juu yake paka mayai na unynyuzie ufuta.
Pika katika moto wa chini 350ΒΊF kwa muda wa dakika 20-25.
Tayari kwa kuliwa.

Dawa za nywele zinazosababisha uvimbe kwenye Kizazi kwa wanawake

Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.
Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.

Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma.

β€œKemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids,” anasema.

Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe kwenye kizazi hutokea katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani kabla hajakoma hedhi.

Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuisha wanawake wa kada tofauti tofauti wanaotumia dawa za nywele na wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili ulibainika.

β€œZipo kemikali tofauti tofauti zinazosababisha uvinbe kwenye kizazi, zipo za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury na hydroquionone,” anasema.

Dk Chipata anasema madhara yanayopatikana katika kemikali za vipodozi ni makubwa siyo tu kwenye kizazi bali nyingine husababisha saratani au kufeli kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya zebaki (mercury).

β€œDawa za nywele zina madhara si lazima zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata jeraha la kuungua bali zinaweza kupenya zenyewe kwenye ngozi kutokana na mfumo wa ngozi,” anasema.

Anashauri kuwa ni vyema watu wakasoma kipodozi kimetengenezwa kwa nini kabla ya kukitumia na kuongeza kuwa ni salama zaidi kubaki na ngozi au nywele halisi badala ya kujibadilisha.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekataza vipodozi vyenye kemikali kama biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl chloride, zirconium na bidhaa zenye aerosol, chloroquionone, steroids, methylene na chloroform.

Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012 na Dk Lauren Wise na wenzake nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la afya la nchini Marekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vina kemikali zenye vichocheo vya estrogen ambavyo kwa kawaida huchochea kasi ya kuota kwa uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na wakati mwingine kwenye mji wa mimba. Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana kama fibroids au myoma.

Dk Wise anasema aliwafanyia uchunguzi wanawake wanaotumia dawa za kulainisha nywele na kuangali umri walioanza kutumia dawa hizo, mara ngapi, waliungua kiasi gani na walikaa na dawa hizo kichwani kwa kipindi gani.

Aliwafuatilia wanawake 23,580 wanaotumia dawa za kulainisha nywele na baada ya kipindi fulani walipimwa. Kati yao, 7146 waligundulika kuwa na uvimbe kwenye kizazi baada ya kupimwa kwa mionzi na wengine kufanyiwa upasuaji.

Kwa nini relaxer ni hatari kwa wanawake?
Dk Wise anasema mchanganyiko ulio kenye dawa za nywele hasa zilizoandikwa β€œLye Relaxer” ni sodium hydroxide wakati makopo ya dawa yaliyoandikwa β€œNo Lye Relaxer” yana calcium hydroxide na guanidine carbonate.

Bidhaa za kulainishwa nywele zilizoandikwa β€˜no lye relaxer’ zinadaiwa kusababisha majeraha kwa kiasi kidogo ukilinganisha na zile zilizoandikwa β€œLye Relaxer”.

Mapishi ya Biskuti Za Mayai

VIAMBAUPISHI

Unga 3 Vikombe

Sukari ya unga (icing sugar) 1 Kikombe

Siagi 250 gm

Mayai 3

Vanilla 2 Vijiko vya chai

Baking powder 1 Kijiko cha chai

JINSI YA KUPIKA

Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
Tia mayai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini.
Tia unga na baking powder changanya na mwiko.
Tengeneza round upange kwenye tray utie nukta ya rangi.
Nyunyuzia sukari juu ya hizo round ulizotengeneza kabla huja choma.
Pika (bake) katika oven moto wa 350Β°F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

Mapishi ya Biskuti Za Kastadi

VIAMBAUPISHI

Unga 6 Vikombe

Sukari ya kusaga 2 vikombe

Siagi 500 gm

Baking powder 1 Kijiko cha chai

Kastadi Β½kikombe

MAPISHI

Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
Mimina mchanganyiko uliopiga kwa mashine kwenye bakuli.
Tia unga na baking powder na Kastadi.
Kata usanifu (design) unaopenda halafu panga kwenye sahani ya kupikia (baking tray).
Pika (bake) katika oven moto wa 350Β° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

Mapishi ya Biskuti Za Jam

VIAMBAUPISHI

Unga 2 Β½ gilasi

Sukari ΒΎ gilasi

Samli 1 gilasi

Mayai 2

Baking powder 2 kijiko vya chai

Vanilla 1 Β½ kijiko cha chai

Maganda ya chungwa 1

MAPISHI

Tia kwenye machine ya kusagia (blender) mayai, sukari, vanilla, samli na maganda ya chungwa, saga vizuri.
Tia unga kwenye bakuli pamoja na baking powder, mimina vitu ulivyosaga kwenye bakuli, changanya.
Punguza unga uliochanganya kidogo weka pembeni.
Unga uliobakia tia kwenya tray ya kuchomeya, utandaze vizuri, tia jam juu yake.
Chukua la kukwaruzia carrot (grater) ukwaruze unga uliuopunguza juu ya jam.
Choma kwa muda dakika 20 moto wa 180Β C.

Acha ipowe kidogo, zikate vipande vya mraba (square) Tayari kwa kula.

Jinsi ya kutengeneza biskuti za Matunda Makavu Na Cornflakes

VIAMBAUPISHI

Unga – 4 Vikombe

Sukari – 1 Kikombe

Baking powder 1 kijiko cha chai mfuto

Siagi – 454 gms

Mayai – 2

Matunda makavu (tende, zabibu, lozi) – 1 Kikombe

Vanilla – 2 Vijiko vya chai

Cornflakes – Β½ kikombe

JINSI YA KUANDAA

Changanya sukari na siagi katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy)
Tia yai moja moja huku unachanganya mpaka iwe laini kama sufi. (fluffy)
Tia unga, baking powder, matunda makavu, changanya na mwiko.
Chota mchanganyiko wa biskuti kwa mkono kama (kiasi cha kijiko kimoja cha supu) fanya duara na uchovye katika cornflakes iliyopondwa kwa mkono (crushed)
Zipange katika treya ya kupikia na zipike (bake) katika moto wa 375Β°F kwa muda wa kiasi dakika 15 huku unazitazama tazama.

Jinsi ya kupika Biskuti Nyembamba (Wafer Bar) Za Chokoleti Na Njugu

MAHITAJI

Wafer Powder/gram wafer (unga wa biskuti uliosagwa wa tayari) – vikombe 2

Maziwa ya Mgando Matamu ya Kopo – 2 vikombe

Nazi iliyokunwa – Β½ Kikombe

Chokoleti vipande vipande – 1 Kikombe

Njugu vipande vipande – Β½ Kikombe

Siagi – 227Β g

MAPISHI

Yeyusha siagi motoni kisha changanya na unga wa wafer acha kidogo motoni
Mimina katika treya unayochomea itandaze vizuri, kisha mimina maziwa juu yake pamoja na njugu vipande , nazi iliyokunwa na vipande vya chokoleti.
Choma (bake) kwenye oveni kwa moto wa 350ΒΊC kwa dakika 20.
Katakata tayari kwa kuliwa

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About