SMS Tamu Sana Za Mahaba

SMS nzuri ya mapenzi ya kimahaba ya kutuma kwa mpenzi wako umpendaye

Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.

Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa

Read and Write Comments

SMS nzuriiii ya kumpa mtu hai

Nakupa HAI, kwa sababu uko HAI, usingekuwa HAI, ni vigumu kupewa HAI, basi nawe wape HAI, walio HAI, maana ni bahati kuwa HAI, wengi walitamani kuwa HAI, lakini wamepoteza UHAI, Usione najidai, ila mimi naringia UHAI, Haya basi pokea HAI, ili moyo wako ufurahi. HAIIIIIIIIIIIII!!!

 

Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa

Read and Write Comments
Shopping Cart