SMS Tamu Mpya Za Mahaba

SMS ya kuasa na kutakia kila la heri katika mapenzi

Mapenzi ni kitu kisichotabirika, ndio maana kila mwenye KUPENDA au KUPENDWA hana uhakika na PENZI lake kwa yule AMPENDAE, Muda wote huhisi anasalitiwa. PENZI Ni kama JENGO lililokosa NGUZO muda wowote unahisi litadondoka… Usinielewe vibaya sikukatazi KUPENDA au KUPENDWA, ila tazama wapi UMEPENDA au UMEPENDWA.kilalakher kwa umpendae

Read and Write Comments

SMS nzuri ya mapenzi ya kutakia usiku mwema

Mungu akupe umri wa mnazi uishi mingi miaka.
Akupe thamani ya mnazi kila kitu chatumika.
Kuanzia kuti lake mpaka kwenye kidaka.
Kitale katikati yake ukila utaridhika.
Matamu na maji yake hukata kiu haraka.
Weupe watui lake lina ladha ukipika.
Kupaka mafuta yake mwili hulainika.
Na kwenye machicha yake kazi nying hufanyika.
Hata na upepo wake uvumapo utacheka.
Sikijui kitu chake kipi kisichotumika.usiku mwema

Read and Write Comments
Shopping Cart
5448 4103 4714 5871 4104 4099 4101 4434 4275 78672 5872 4290 78491 4386 4076