Jinsi ya kutumia mashonanguo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea
Mashonanguo kwa kiingereza ni Blackjack au kwa kisayansi yanajulikana kama (Bidens
pilosa)
Mashona nguo yanazuia wadudukama vile Vidukari, Siafu, bungo, katapila, chenene (crickets), nyenyere, siafu na inzi weupe.
Jinsi ya Kutayarisha na kutumia mashonanguo
- Jaza kikombe kilichojaa mbegu ambazo zimekomaa na maji;
- Chemsha kwa dakika kumi au loweka kwenye maji kwa saa ishirini na nne, kisha upooze.
- Ongeza lita moja ya maji na kijiko kimoja kidogo cha sabuni;
- Kisha unyunyizie mimea.
Matumizi mengine
- Mbegu zinaweza kutawanyishwa karibu na vichaka kuvutia mchwa.
- Mmea waweza kupondwa au kufikichwa kisha maji yake yatumike kunyunyizia mimea.
Angalizo: Kiasi kingi cha dawa hii chaweza kudhuru baadhi ya maua ya mimea.
Read and Write Comments
Recent Comments