Mahusiano: Vijana na Ujana

Ujumbe kwa mabinti kuhusu uvaaji

Familia Kwanza: Wasichana wawili waliwasili kwenye Kikao huku wamevaa nguo ambazo zilikuwa zikionyesha miili yao.

Hiki ndo kitu ambacho Mwenyekiti wa kikao alichowaambia, aliwatazama kwa muonekano mzuri kisha akawataka wakae, kisha akawaambia jambo ambalo hawatoweza kusahau katika Maisha yao.

Aliwaangalia moja kwa moja katika macho yao, kisha akasema;

“Wasichana, kila kitu ambacho MUNGU amekiumba chenye thamani katika Dunia hii kimesitiriwa, na ni vigumu kukiona au kukipata.

1.Wapi unapoipata Almasi?
Ni chini kabisa ndani zaidi katika ardhi, na yamefunikwa na kuhifadhiwa humo

2. Wapi mnapoweza kuipata Lulu? Pia ni ndani zaidi kwenye kina kirefu zaidi katika Bahari, na yamehifadhiwa humo na kujificha ndani ya Sanamu zuri la Baharini

3. Wapi mnapoweza kuipata Dhahabu? napo pia ni ndani zaidi katika Migodi, na yamefunikwa juu na Ardhi za Miamba na ndio uyapate hapo. Yatupasa tufanye kazi ya ziada zaidi na tulime kwa undani zaidi ndipo tuyapate.

Kisha Mwenyekiti akawaangalia wale Mabinti kwa Jicho kali zaidi na kisha akawaambia;
“Miili yenu ni ya kuogopwa na ina thamani sana, na inazidi sana hata thamani ya Dhahabu, Almasi au Lulu. Na yawapasa muihifadhi zaidii.

Kama mtatunza Madini yenu kama ilivyotunzwa Almasi, Dhahabu na Lulu basi Makampuni yenye sifa nzur katika Jamii, Makampuni ya uhakika, Makampuni ya kuaminika yenye Mitambo mizuri yatatenga Muda wa miaka kadhaa katika kufanikisha kuyapata Madini hayo.

Kwanza itawapasa wawasiliane na Serikali (ambayo ndio familia yako) pia kusahihisha Mikatabata muhimu (ndoa) na mwisho ni Mgodi wenye dhana kubwa (ambayo ndiyo ndoa) lakini kama ukiacha madini yako yenye thamani nje hayajahifadhiwa katika uso wa Dunia basi utamvutia kila Mmoja (Mwanaume) na hasa wale ambao ni Wachimbaji haramu watakuja na kuchimba kiharamu (Zinaa), kwa hiyo kila mmoja atachukua kwa vifaa vilivyo na Makali na hivyo ndio watakavyokulima kirahisi.

Hivyo basi nawashauri hifadhini Miili yenu vizuri ili iwavutie wachimbaji wa halali (Waoaji) ndio wakukaribie upate kuheshimika

Read and Write Comments

Maisha ya Wasichana Wa facebook na instagram

Wiki ya kwanza
Status:”Location flani amazing”
“Having fun”
“I love my life”
“sijali mnayosema nafanya nachotaka”

BAADA YA MIEZI MIWILI
STATUS:”Binadamu wengi ni wasaliti”
“trust nobody”
“Na hili nalo litapita”
BAADA YA MIEZI SITA
Status:”Yesu wewe ndio rafiki wa kweli”
“Bwana ndiye mchungaji wangu”
BAADA YA MIEZI TISA NA KIDOGO
STATUS: “Nakupenda mwanangu😅😅😀😆😆😆😂😂😂😂😄

Kama Mwanamme Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
Read and Write Comments

Ushauri kwa vijana wenye miaka 22 nakuendelea

Ikiwa wewe ni kijana na Una umri wa kuanzia miaka 22 na Kuendelea
Soma hapa ujifunze maisha ya hekima na namna bora ya kuishi na kufanikiwa ungali kijana

1. Kama uko shule au chuo soma na usicheze ukifeli unajipotezea muda. Soma sana utafanikiwa…

2. Jifunze kuweka akiba ya pesa. Pia jifunze kuwa na matumizi mazuri ya pesa,bajeti vizuri na jiwekee akiba bank au popte unapoona panafaa.

3. Jitengenezee good character yaani tabia yako njema ili uwe tofauti na wengine.. Jitofautishe na wengine, uwe mfano bora

4. Jifunze kufanya kazi tofauti tofauti. Fanya hiki ama kile ili angalau uweze kuishi popote kwani dunia inabadilikaa na huwezi jua kesho yako

5. Anza kununua na kumiliki vitu kama kitanda godoro vyombo na ardhi au kiwanja. Kumbuka msingi mzuri wa maisha ni fikra za ujana na kujiwekea mali

6. Kama utaweza kapange ujifunze maisha. Anza kujitegemea ili kujipa confidenece na maisha.

7. Weka falsafa yako katika maisha na uiishi. Falsafa ni dira ya kukuongoza. Mfano unataka kumiliki nini katika maisha? Unataka mke au mume wa aina gani? Aina gani ya maisha unaipenda? Hiyo ndiyo falsafa…

8. Tengeneza mahusiano yaliyotulia na weka malengo. (Kwa wale wa ndoa) Jichagulie kijana au binti aliyemzuri katika wengi, kijana au binti wa moyo wako, mpende… Kipindi hiki ni cha kuwa na mwenza aliyetulia kama unafikiri kuoa au kuolewa. Ukicheza ukafikisha 30 bila kuwa na mtu maaalumu basi utaoa au kuolewa bora mradi ila siyo na mtu wa ndoto yako..

9. Kuwa na marafiki imara, jichagulie katika wengi marafiki kadhaa waliotulia wenye nidhamu ya maisha na wanaopenda uende mbele. Kijana chunga marafiki ulionao wengi leo wanajuta kwaa urafiki m’baya uliowapoteza… a

10. Kumbuka ibada na kumshukuru Mungu. Kipindi hiki ni cha misukosuko na mihemko mingi. Usiache mafundisho ya imani yako, usimsahau Mungu. Mshukuru Mungu kwa uhai na kila jema au baya likupatalo.

11. Jitume katika kazi, watu waliofanikiwa wanajua thamani ya juhudi na kujituma. Usikate tamaa hata kama unapata kidogo. Fanya kazi kama vile kesho haipo. Matunda utayaona

12. Zingatia kujiweka safi. Kuwa msafi na mtanashati huanza na ubongo, muonekano wako ndivyo watu watakavyo kuchukulia. Jiweke safi na jitunze..

13. Kula kwa afya, wengi wanachukia miili yao. Wanauchukia aidha unene au wembamba, ila ukila kwa afya, ukafanya mazoezi unatengeneza afya bora ya sasa na baaadae..

14. Vaa kwa heshima, usivae kama mcheza disko au teja. Kumbuka thamani yako kwa Mungu. Kwanini uvae nguo za machukizo mbele yake! Kwanini ukubali kuwa wakala na kutumiwa na shetani kuwaaangamiza wengine kwa kuvaa ovyo? Vaa kwa heshima..

15. Pendelea kusafiri maeneo tofauti na ujifunze! Asafiriye hupata maarifa na hujifunza mengi. Penda kusafiri, tembelea maeneo tofauti utakuwa na mengi ya kujifunza.

16. Kumbuka kupumzisha mwili. Kuishi kwetu kupo katika chembe ya uhai iliyopo mwilini. Upe mwili na ubongo chakula chake cha kupumzika. Nenda maeneo yatakayofanya mwili na akili vipumzike angalau kila baada ya miezi kadhaa..

17. Jifunze kuamua mwenyewe. Usisubiri kila kitu kumshirikisha mtu ndio uamue. Jifunze kuwa mwamuzi wa mambo yako mwenyewe haijalishi kwa gharama ipi. Watu wawe washauri ila ubaki kuwa mwamuzi mwenyewe.

18. Kuwa mtu wa kutunza siri. Jitahidi kuwa na shingo nzito na akili yenye kuweka siri. Usiwe mtu wa kusema kila uonacho au uambiwacho.

19. Jfunze na zitawale hisia zako. Hisia ziwe za hasira, mapenzi au ugomovi zitawale na utaishi miaka mingi. Asiye tawala hisia zake hata awe mkubwa bado ni mdogo…

20. Jitolee kwaajili ya wengine, fundisha kemea saidia. Unaweza kufundisha kupitia facebook wasap nk. Kemea ukiona mtu anafanya kitu kibaya, saidia wenye shida wakumbuke wagonjwa yatima wazee na wenye mahitaji. Wewe ni yatima, mzee, au muhitaji wa kesho.. Weka akiba ya wema

21 Jenga mazingira ya kuishi na watu vizuri. Usijione mzuri au HB sana ukadharau wengine. Ishi na kila mtu kwa upendo hata kama wanakuchukia..

22. Tunza muda, muda ni mali huwezi kuurudisha, kuusimamisha au kuuzuia. Ukishapotea ndio basi tena. Tambua thamani ya muda na fanya vitu kwa wakati..

23. Pendelea kusoma hasa vitabu vya dini, kuhusu mali, elimu, mchumba, afya, maisha, uongozi, hekima, busara, utu, uchaji, utii, maarifa, utajiri, heshima, uvumilivu, matumaini, upendo, na kila kitu vimo katika Biblia na Qur’an ..soma uchote hekimaa…

24. Acha kujifunza matumizi ya pombe, sigara , dawa za kulevya. Kama unatumia jitahidi uache, kama unajifunza acha na kama kuna mtu anakushawishi kataa. Afya ni mali na mtaji usichoshe na kuumiza uhai wako kwa pombe sigara na madawa ya kulevya…

Inafaa ukishare kwa wengine wajifunze maarifa haya..
*Maisha ni maamuzi yako wewe*
Kuamua kufanikiwa au kushindwa,
kuamua utajiri au umasikini yote ni mipango na hutokana na fikra zako..

Read and Write Comments

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?

Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO

Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
Read and Write Comments
Shopping Cart
0
    0
    Your Cart
    Your cart is emptyReturn to Shop
    🏠 Home 🔒 Login 📝 Register 💡 Tools