Jambo la kwanza jaribu kumwondoa hofu mwathiriwa na
muliwaze maana amepata jambo la kutisha. Na iwapo mtu
amejeruhiwa sana mpeleke katika kituo cha huduma za afya
kilicho karibu mara moja. Vinginevyo ongozana na rafiki
yako kwenda kituo cha Polisi na kutoa taarifa kuhusu jambo
lililotokea. Polisi watampa fomu ambayo ataipeleka kwa mtoa
huduma. Ni muhimu usijioshe kwa maji kabla hujachunguzwa na
mtaalamu wa afya kwani kufanya hivyo kutaondoa ushahidi wa
kubakwa.
Kwa kuwa kupitia utaratibu huu
inakuwa vigumu mwathiriwa
anahitaji msaada wa karibu
na uangalizi. Mzazi au rafiki
anahitajiwa aongozane naye
na kumsaidia, kwa mfano
kuhakikisha kuwa katika kituo
cha polisi msichana ahojiwe na
polisi wa kike.
Mtu aliyebakwa anahitaji
kusaidiwa kihisia ili aweze
kusahau mawazo na jambo
liliomtokea. Kwa mwathirika, ni
muhimu apewe ushauri nasaha
ili aendelee kujihisi kwamba yeye bado yupo kama mtu wa
kawaida. Ni muhimu pia kuzishughulikia habari za mwathiriwa
kwa siri. Usimweleze kila mtu kilichotokea. Waeleze wale tu
ambao unafikiri wanaweza kusaidia kama daktari, mwalimu au
mzazi. Usiulize maswali ya kwa nini maana inaweza ikaonekana
ni kosa la mwathiriwa. Badala yake zungumza na huyo mtu kwa
utaratibu, polepole, peke yake na mpe uangalifu wa kutosha.
Hakikisha kwamba hutoi lawama yoyote kwa mwathiriwa.
Kubakwa kamwe siyo kosa la mwathiriwa.
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Recent Comments