Ukeketaji au tohara ya wanawake ni hatari sana kwa msichana
anayetahiriwa. Wasichana hufa kutokana na madhara yake
makubwa zaidi kwa vile:
- Hutokwa na damu nyingi.
- Uambukizo unatokea iwapo vifaa vilivyotumiwa
- havikuwa safi. Uambukizo unaweza kuenea mpaka katika
viungo vya ndani vya uzazi na kusababisha ugumba na
hata vifo.
- Hatari ya kuambukizwa Virusi vya UKIMWI wakati wa
ukeketaji.
- Kuziba kwa mkojo na damu ya mwezi (hedhi) ndani ya
mwili wa mwanamke na kusababisha uambukizo.
- Matatizo na maumivu makali wakati wa kujamiiana na
wakati wa kujifungua kutokana na kupungua ukubwa wa
uke. Ukeketaji wa wanawake mara nyingi una madhara
ya kisaikologia ambapo wasichana hupoteza tumaini
na imani kwa walezi au wazazi na wanaweza wakapata
mateso ya kujisikia waoga, kufadhaika, kutojiweza na
kutokuwa kamilifu kimwili.
Zaidi ya hayo, ukeketaji unampunguzia mwanamke hamu ya
kujamiiana. Kufanikisha hamu ya ngono inategemea kwa kiasi
kikubwa viungo vya uzazi vya nje. Ukeketaji hata hivyo unaharibu
umbile na kazi za viungo vya uzazi vya nje vya mwanamke.
Ina madhara kimwili na kisaikologia ambapo mara nyingi
huleta matatizo ya mahusiano ya kimwili kati ya mwanamume
na mwanamke. Kisimi ni sehemu ya mwili wa msichana chenye
ashiki na hisia kali ya viungo vya uzazi. Kinasisimua ashiki kwa
mwanamke anaposhikwa. Sehemu ya ndani ya mashavu na kisimi
kwa kiasi kikubwa vinahusika na hali kiwango cha raha ya na
kufikia mshindo wakati wa kujamiiana. Wakati kisimi na viungo
vingine vya uzazi vimeondolewa, ashiki na raha hupungua kwa
kiasi kikubwa. Endapo mwanamke amekatwa vibaya sana au uke
umeshonwa, kuna uwezekano wa kupata maumivu na matatizo
wakati wa kujamiiana na wa kujifungua.
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Recent Comments