Hatari inategemea na mazingira ambapo mimba inatolewa. Kama ni hospitalini na i inatolewa na mtaalamu aliyesomea na kama mazingira na vifaa ni safi, uwezekano wa kutoa mimba salama ni mkubwa. Lakini, hata katika mazingira hayo, shida zinaweza kutokea.
Msingi wa kukumbuka ni kwamba kutoa mimba mwenyewe au hata kwa mtu asiyesomea ni hatari sana. Kwa wanawake wanaojaribu kutoa mimba kuna uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi katika via vya uzazi na baadhi yao hutoboa mfuko wa uzazi. Matatizo haya ni hatari sana. Matatizo yanayohusiana na kutoa mimba ni mazito, kama mfuko wa uzazi kuharibika, maambukizi yasiyotibiwa katika via vya uzazi, kutoa damu nyingi, ugumba au hata kifo kwa mwanamke aliyehusika.
Kwa hiyo ni vizuri zaidi na tena salama kuacha kutoa mimba. Unaweza kuzuia kupata mimba i isiyotarajiwa, ama kwa kuacha kujamii ana au kwa kutumia njia za uzazi wa mpango kujikinga. Pia kumbuka kuwa utoaji mimba hauruhusiwi hapa Tanzania.
Read and Write CommentsReferences:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Recent Comments