Hii ndiyo Ladha ya bia zote usiyoijua
Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..
Kwa wanywaji wazuri wa bia,
chupa ya kwanza ๐บ huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza kooโฆ Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.
chupa ya pili ๐บ๐บ kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihiโฆ.
Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.
Bia ya tatu ๐บ๐บ๐บ huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sanaโฆ. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokezaโฆ..
Bia ya nne ๐บ๐บ๐บ๐บ huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikiaโฆ.. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.
Bia ya tano ๐บ๐บ๐บ๐บ๐บ ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipuโฆโฆna kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; โMi sipendwi mpaka leo sijaolewaโ au โ Mume wangu sijui yukoje hanijaliโ
Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.
Kuanzia bia ya sita ๐บ๐บ๐บ๐บ๐บ๐บ na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. โฆโฆ. โฆKuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.
Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjikaโฆโฆ.
Recent Comments