Author name: SW - Melkisedeck Shine

Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu

Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimu….kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamakeπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Sitasahau mwaka huu

Sitasahau mwaka ule ambapo nilipeleka barua ya maombi yangu ya kazi kwenye kampuni moja maarufu. Wakati nasubiri majibu siku moja nikaenda kwa mama ntilie kununua maandazi akanifungia vizuri, kufika nyumbani hamu yote ya maandazi iliniishia pale nilipogundua karatasi iliyofungiwa maandazi ni barua yangu ya kuombea kaziπŸ˜‚πŸ˜‚

Wazo la asubuh – penzi la kuku

Wazo la asubui

πŸ™ˆPenzi la kuku sekunde 2 ila vifaranga kibao.Lakini binadamu masaa kibao mtoto 1 au 2. Sasa binadam na kuku nani JEMBE? Ukimwona JOGOO popote piga SALUTI!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ukinuna poa tu!!!!!πŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒ

Eti wanadamu walikuja vipi duniani

Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake:
MTOTO: Baa, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa.
Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto
wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika
akamfuta mamake)
MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na
manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi
kwa baba)
MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa
manyani mwanzo?Au wanidanganya?
BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo
wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo waoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸšΆπŸΌπŸšΆπŸΌπŸšΆπŸΌ

Ameniomba nimfungulie akaunt facebook cheki nilichomjibu

Leo nimechoka zangu alafu shangazi amekuja anataka nimuunganishe facebook. Imebidi nimwambie
lazima awe na picha passport size 4 kwaajili ya kuweka profile picture, barua kutoka kwa afisa mtendaji na Atm card ya nmb bank. Alafu awe na marefa wanne ambao wamekuwa facebook for more than 3 years. Amesema
hataki tena kujiunga fb!

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Saa ivi niko zangu nimelala naendelea kupunguza uchovu

Huyu mwanamke kazidi sasa

Jamaa: Mambo honey, upo ok?
Mrembo: Sipo ok my dear
Jamaa: Una tatizo gani baby?
Mrembo: Nimetoka hospitali kupima, nna mimba.
Jamaa: Weeh usiniletee balaa hiyo mimba imeingiaje wakati huwa tunatumia kinga?
MremboΒ Kwani nani kakwambia mimba ni yako, hebu tuliza mshono huo.

πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
MTATUUA

Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti

Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenzi…

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Shopping Cart