Ee Moyo Mtakatifu sana wa Yesu, chemchemi ya kila baraka, ninakuabudu, ninakupenda, na kwa majuto halisi ya dhambi zangu, nakutolea moyo wangu dhaifu. Nifanye mnyenyekevu, mvumilivu na safi, nikikubali na kuyatii kabisa mapenzi yako. Ee Yesu mwema, unijalie niishi nawe na kwa ajili yako. Unilinde niwapo katikati ya hatari, unifariji katika mateso, unipe afya ya mwili na msaada katika mahitaji ya mwili, Baraka yako juu ya kila nilifanyalo, na neema ya kifo chema. Amina.
Ee Yesu uliyesema “Kweli nawaambieni, ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, gongeni nanyi mtafunguliwaâ€, tazama ninagonga, ninatafuta na kuomba …….. (Taja ombi lako)
Baba Yetu….., Salamu Maria …….., Atukuzwe Baba……..
Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninakutumainia kwa moyo wote!
Ee Yesu uliyesema “Kweli nawaambieni, chochote mtakachomwomba Baba kwa jina langu mtapewaâ€, tazama kwa jina lako ninaomba ……. (Taja ombi lako)
Baba Yetu….., Salamu Maria …….., Atukuzwe Baba……..
Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninakutumainia kwa moyo wote!
Ee Yesu uliyesema “Kweli nawaambieni, mbingu na dunia zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamweâ€, tazama, nikitiwa nguvu na maneno yako ya kweli ninaomba …….. (Taja ombi lako)
Baba Yetu….., Salamu Maria …….., Atukuzwe Baba……..
Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninakutumainia kwa moyo wote!
Ee Moyo Mtakatifu wa Yesu, ambaye kwako ni kitu kimoja tu kisichowezekana, ambacho ni kutoacha kutowaonea huruma wenye huzuni, utuhurumie sisi wakosefu maskini na utujalie neema tukuombayo kwa njia ya Moyo Imakulata wa Maria, Mama yetu mpole.
Sali ‘Salamu Malkia’ na kuongezea, ‘Mtakatifu Yosefu Baba Mlishi wa Yesu, utuombee’.
P.S. – Sala hii ya Novena ilisaliwa kila siku na PADRE PIO kwa ajili ya kuwaombea wale wote waliomwomba msaada wa sala zake. Unaweza kuisali kwa namna tofauti tofauti. Mfano, kama Novena ya siku tisa, ambapo unasali sala hii mara moja au zaidi kila siku kwa siku tisa, au unaweza kuifanya kama Novena ya masaa, ambapo unasali sala hii kila baada ya saa moja kwa masaa tisa kwa siku hiyo hiyo, hasa kama kitu unachokiomba ni cha haraka au umesongwa moyoni. Vilevile unaweza kuifanya sala hii kama sehemu ya sala zako za kila siku katika mwezi Juni ambao ni mwezi uliotengwa na Kanisa kwa ajili ya kuuheshimu Moyo Mtakatifu wa Yesu, na hapo utaitumia kuwaombea watu waliokuomba msaada wa sala zako kama alivyofanya Mtakatifu Padre Pio. Pia unaweza kuitumia kama sala yako ya siku zote au ya mara kwa mara kwa ajili ya mahitaji mbalimbali.
Jackson Makori (Guest) on June 18, 2024
ðŸ™âœ¨â¤ï¸ Neema za Mungu zikufunike
Joseph Kitine (Guest) on March 31, 2024
ðŸ™â¤ï¸ðŸ’– Tumshukuru Mungu kwa yote
Grace Njuguna (Guest) on March 19, 2024
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Nora Kidata (Guest) on September 18, 2023
ðŸ™ðŸ’– Asante kwa neema zako Mungu
Mercy Atieno (Guest) on March 25, 2023
Baraka kwako na familia yako.
Catherine Mkumbo (Guest) on March 24, 2023
ðŸ™â¤ï¸ðŸ’– Bwana akujalie baraka
Hellen Nduta (Guest) on March 20, 2023
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Andrew Odhiambo (Guest) on February 16, 2023
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Alex Nyamweya (Guest) on January 26, 2023
ðŸ™ðŸŒŸâ¤ï¸ Nakuombea heri
Mary Njeri (Guest) on January 18, 2023
Tembea kwa imani, si kwa kuona
John Mushi (Guest) on January 16, 2023
ðŸ™ðŸŒŸ Neema za Mungu zisikose
David Chacha (Guest) on November 26, 2022
ðŸ™ðŸ’– Nakusihi Mungu
Edward Lowassa (Guest) on September 26, 2022
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Betty Kimaro (Guest) on September 4, 2022
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Nancy Kawawa (Guest) on September 2, 2022
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Joseph Kitine (Guest) on August 13, 2022
Rehema zake hudumu milele
George Mallya (Guest) on July 24, 2022
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Anna Mchome (Guest) on March 25, 2022
ðŸ™âœ¨ Mungu atakuinua
Joseph Njoroge (Guest) on March 13, 2022
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Faith Kariuki (Guest) on January 8, 2022
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
Josephine Nduta (Guest) on January 3, 2022
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
Peter Mbise (Guest) on December 7, 2021
Nguvu hutoka kwa Bwana
Joy Wacera (Guest) on October 25, 2021
Katika imani, yote yanawezekana
Mary Njeri (Guest) on October 5, 2021
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Patrick Kidata (Guest) on October 3, 2021
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Andrew Mahiga (Guest) on August 5, 2021
ðŸ™ðŸ’– Mungu wetu asifiwe
Rose Waithera (Guest) on July 12, 2021
Mungu akubariki!
Moses Mwita (Guest) on February 24, 2021
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Nora Kidata (Guest) on November 15, 2020
Neema ya Mungu inatosha kwako
Edwin Ndambuki (Guest) on October 6, 2020
ðŸ™âœ¨ðŸ’– Mungu atajibu maombi yako
Michael Onyango (Guest) on September 22, 2020
Neema na amani iwe nawe.
Mariam Kawawa (Guest) on September 20, 2020
ðŸ™âœ¨ Neema ya Mungu iwe nawe
Joseph Njoroge (Guest) on September 19, 2020
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Andrew Mahiga (Guest) on September 18, 2020
ðŸ™â¤ï¸ Mungu ni mkombozi
Carol Nyakio (Guest) on September 14, 2020
Mwamini katika mpango wake.
Dorothy Mwakalindile (Guest) on August 12, 2020
ðŸ™â¤ï¸ Mungu ni mlinzi wetu
Lucy Mushi (Guest) on August 8, 2020
ðŸ™â¤ï¸âœ¨ Mungu akujalie furaha
Monica Nyalandu (Guest) on June 11, 2020
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Anna Sumari (Guest) on May 14, 2020
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
John Lissu (Guest) on April 17, 2020
Tumaini ni nanga ya roho
Jane Muthui (Guest) on April 1, 2020
ðŸ™â¤ï¸ðŸŒŸ Asante Mungu kwa uhai
Edith Cherotich (Guest) on March 16, 2020
ðŸ™â¤ï¸âœ¨ Asante Mungu kwa kila kitu
Sarah Mbise (Guest) on February 9, 2020
ðŸ™âœ¨ Mungu atupe nguvu
Rose Kiwanga (Guest) on December 2, 2019
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
John Kamande (Guest) on October 1, 2019
Mungu ni mwema, wakati wote!
Hellen Nduta (Guest) on June 17, 2019
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Bernard Oduor (Guest) on June 3, 2019
Amina
Anna Sumari (Guest) on May 15, 2019
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
Charles Mrope (Guest) on May 5, 2019
ðŸ™â¤ï¸ Mungu akubariki
Rose Lowassa (Guest) on March 13, 2019
ðŸ™ðŸ’–✨ Neema yako ni ya kutosha
Janet Mbithe (Guest) on December 25, 2018
ðŸ™ðŸŒŸ Mungu akujalie amani
Linda Karimi (Guest) on December 19, 2018
Sifa kwa Bwana!
Michael Mboya (Guest) on December 3, 2018
Imani inaweza kusogeza milima
Janet Sumari (Guest) on October 26, 2018
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
Betty Kimaro (Guest) on April 29, 2018
ðŸ™ðŸŒŸ Mungu alete amani
Wilson Ombati (Guest) on February 7, 2018
Mwamini Bwana; anajua njia
Henry Mollel (Guest) on December 14, 2017
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Andrew Mahiga (Guest) on November 30, 2017
Endelea kuwa na imani!
John Kamande (Guest) on November 19, 2017
ðŸ™â¤ï¸ðŸ’– Baraka za Mungu ziwe nawe
Lucy Mushi (Guest) on October 3, 2017
ðŸ™ðŸ™ðŸ™