Kwa njia ya Maji haya ya Baraka, na kwa njia ya Damu yako azizi, na kwa maombezi ya Moyo Safi wa Maria, unioshe na uovu wangu wote na uwasaidie roho zinazoteseka toharani. Amina.
Updated at: 2024-05-27 07:14:21 (9 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kwa njia ya Maji haya ya Baraka,
na kwa njia ya Damu yako azizi,
na kwa maombezi ya Moyo Safi wa Maria,
unioshe na uovu wangu wote na uwasaidie roho zinazoteseka toharani. Amina.
Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”.
Updated at: 2024-05-27 07:14:15 (9 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mwongozo wa namna ya Kusali Rozari Takatifu ya Mama Bikira Maria
Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”.
Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, “Tusali kuombea amani katika nchi yetu na ulimwenguni kote, na tuunganishe nia hizo na nia zetu sisi wenyewe, nk).
Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na Salamu Maria tatu.
Mojawapo ya maneno yafuatayo huweza kutumika: “Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, …… Mungu Mwana utuongezee matumaini, Salamu Maria, …… Mungu Roho Mtakatifu washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, …..”
Au;
“Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,…. Utuongezee matumaini ee Bwana, Salamu Maria,…. Uwashe nyoyo zetu kwa mapendo yako ee Bwana, Salamu Maria, …..” Au; “Salamu e uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu Maria,….. Salamu e Mama wa Mungu Mwana, Salamu Maria,….. Salamu e Mchumba wa Mungu Roho Mtakatifu, Salamu Maria,……” Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji huruma yako zaidi. Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef.
Kisha endelea na sala zinazofuata kama mpangilio unavyoonyesha hapo juu.
Kila baada ya Tendo moja na makumi ya Salamu Maria…, “Atukuzwe..”, “Ee Yesu wangu…” na “Tuwasifu milele…” kama muda unatosha wimbo ufaao wa Bikira Maria uimbwe (kama muda ni mfupi basi angalau ubeti mmoja mmoja uimbwe kila baada ya makumi hayo). Baada ya Wimbo, Tendo linalofuata litangazwe kwa sauti pamoja na tafakari fupi au ombi linaloambatana na Tendo husika kama inavyoonyeshwa hapa chini.
MATENDO YA ROZARI TAKATIFU
MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
Tendo la nne; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)
Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
Tendo la tano; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)
Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
LITANIA YA BIKIRA MARIA
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumie
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utusikie
Kristo utusikilize
Mungu Baba wa Mbinguni,…… Utuhurumie
Mungu Mwana Mkombozi wa dunia ……… Utuhurumie
Mungu Roho Mtakatifu …….. Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja …….. Utuhurumie
Maria Mtakatifu ………. utuombee
Mzazi Mtakatifu wa Mungu …….. utuombee
Bikira Mtakatifu Mkuu wa Mabikira …….. utuombee
Mama wa Kristo ……… utuombee
Mama wa Neema ya Mungu ………….. utuombee
Mama Mtakatifu sana ……… utuombee
Mama mwenye usafi wa Moyo ……….. utuombee
Mama mwenye ubikira ……….. utuombee
Mama usiye na doa ……….. utuombee
Mama mpendelevu ………. utuombee
Mama mstajabivu ………. utuombee
Mama wa Muumba ………. utuombee
Mama wa Mkombozi ………….. utuombee
Mama wa Kanisa……….. utuombee
Bikira mwenye utaratibu ………….. utuombee
Bikira mwenye heshima ………….. utuombee
Bikira mwenye sifa ………….. utuombee
Bikira mwenye uwezo ………….. utuombee
Bikra mweye huruma ………….. utuombee
Bikra mwaminifu………….. utuombee
Kioo cha haki ………….. utuombee
Kikao cha hekima ………….. utuombee
Sababu ya furaha yetu ………….. utuombee
Chombo cha neema ………….. utuombee
Chombo cha kuheshimiwa ………….. utuombee
Chombo bora cha ibada ………….. utuombee
Waridi lenye fumbo ………….. utuombee
Mnara wa Daudi ………….. utuombee
Mnara wa pembe ………….. utuombee
Nyumba ya dhahabu ………….. utuombee
Sanduku la Agano ………….. utuombee
Mlango wa Mbingu ………….. utuombee
Nyota ya asubuhi ………….. utuombee
Afya ya wagonjwa ………….. utuombee
Kimbilio la wakosefu ………….. utuombee
Mtuliza wenye huzuni ………….. utuombee
Msaada wa waKristo ………….. utuombee
Malkia wa Malaika ………….. utuombee
Malkia wa Mababu ………….. utuombee
Malkia wa Manabii ………….. utuombee
Malkia wa Mitume ………….. utuombee
Malkia wa Mashahidi ………….. utuombee
Malkia wa Waungama dini ………….. utuombee
Malkia wa Mabikira ………….. utuombee
Malkia wa Watakatifu wote ………….. utuombee
Malkia uliyepalizwa Mbinguni ………….. utuombee
Malkia wa Rozari takatifu ………….. utuombee
Malkia wa amani ………….. utuombee
Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusamehe ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusikilize ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utuhurumie.
Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,…………..Tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe
Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote; na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate na furaha za milele. Kwa Kristo Bwana wetu, Amina.
Ee uliye Mkuu, Mt. Yosefu, uliyatii kabisa maongozi ya Roho Mt. Unijalie neema ya kufahamu aina ya maisha ambayo Mungu anapenda mimi niishi. Usiniache nidanganyike katika jambo muhimu kama hili, ambalo furaha yangu hapa duniani inalitegemea, na hata pia wokovu wa roho yangu.
Updated at: 2024-05-27 07:13:54 (9 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee uliye Mkuu, Mt. Yosefu, uliyatii kabisa maongozi ya Roho Mt. Unijalie neema ya kufahamu aina ya maisha ambayo Mungu anapenda mimi niishi. Usiniache nidanganyike katika jambo muhimu kama hili, ambalo furaha yangu hapa duniani inalitegemea, na hata pia wokovu wa roho yangu.
Unijalie, nikiangazwa na matakwa matakatifu na nikiwa mwaminifu katika kuyatimiza, nikumbatie aina ya maisha ambayo Mungu ameniandalia na yatakayoniongoza kwenye furaha ya milele. Amina.
Malkia wa mbingu, furahi, aleluya. Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya. Amefufuka alivyosema, Aleluya. Utuombee kwa Mungu, Aleluya. Furahi shangilia, ee Bikira Maria, Alaluya. Kwani hakika Bwana amefufuka Aleluya.
Updated at: 2024-05-27 07:14:05 (9 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Malkia wa mbingu, furahi, aleluya. Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya. Amefufuka alivyosema, Aleluya. Utuombee kwa Mungu, Aleluya. Furahi shangilia, ee Bikira Maria, Alaluya. Kwani hakika Bwana amefufuka Aleluya. Tuombe. Ee Mungu, uliyependa kuifurahisha dunia kwa kufufuka kwake Bwana wetu Yesu Kristu, Mwanao: fanyiza, twakuomba, kwa ajili ya Bikira Maria, tupate nasi furaha za uzima wa milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.
Ewe Mtakatifu Yuda Tadei,/ mtume mtukufu na shahidi wa Kristo,/ umesifika pote kwa wepesi wako wa kutoa misaada/ kwa wanaokukimbilia katika matatizo yao mazito./ Pia ni mwombezi wa waliopondeka moyo./
Updated at: 2024-05-27 07:14:23 (9 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ewe Mtakatifu Yuda Tadei,/ mtume mtukufu na shahidi wa Kristo,/ umesifika pote kwa wepesi wako wa kutoa misaada/ kwa wanaokukimbilia katika matatizo yao mazito./ Pia ni mwombezi wa waliopondeka moyo./
Mimi ni mmoja wa hao./ Nakujia na moyo uliojaa shida na matatizo./ Nakusihi kwa moyo wote/ unisaidie kwa maombezi yako yenye nguvu/ kufikia utatuzi unaofaa kadiri ya mapenzi ya Mungu./ Maisha yangu yamejaa misalaba,/ siku kwa siku matatizo hayapungui./ Moyo wangu umekuwa bahari ya siki chungu sana./ Mapito yangu nayaona yamejaa miiba mikali./ Roho yangu imezama katika dimbwi la machozi na kite./ Nafsi yangu imezingirwa na giza nene./ Ghasia na kukatishwa tamaa ya kuishi/ hunyemelea roho yangu./ Maongozi ya Mungu na imani naviona vinanitoka kidogo kwa kidogo./
Nikielemewa na mawazo kama hayo/ najikuta sina nguvu za kuishi,/ na maisha kwangu ni msalaba mzito/ ninaouogopa hata kuunyakua./ Wewe unaweza kabisa kunitoa katika balaa hili./ Sitaacha kukusihi/ hadi hapo utakaponisaidia/ au kunijulisha mapenzi ya Mungu kwangu./ Natangulia kutoa shukrani kwa jibu liwalo lote.
Kwa ajili ya Baba Mtakatifu wetu ..(N); Bwana, umpe moyo wako wa uchungaji mwema
Kwa ajili ya makardinali na maaskofu wakuu; Uwape moyo wa kichungaji ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wa majimbo; Uwajaze na Roho wako ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre watawa; Wakamilishe katika wito wao ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre walioko hatarini; Uwaokoe ee Bwana
Updated at: 2024-05-27 07:13:38 (9 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kwa ajili ya Baba Mtakatifu wetu ..(N); Bwana, umpe moyo wako wa uchungaji mwema Kwa ajili ya makardinali na maaskofu wakuu; Uwape moyo wa kichungaji ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wa majimbo; Uwajaze na Roho wako ee Bwana Kwa ajili ya mapadre watawa; Wakamilishe katika wito wao ee Bwana Kwa ajili ya mapadre walioko hatarini; Uwaokoe ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wenye udhaifu; Uwatie nguvu ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wenye hofu; Uwape amani ee Bwana Kwa ajili ya mapadre waliokata tamaa; Uwavuvie upya ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wakaao upweke; Uwasindikize ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wamisionari; Uwalinde ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wanaohubiri; Uwaangazie ee Bwana Kwa ajili ya mapadre na watawa waliokufa; Uwafikishe kwenye utukufu wako ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wote; Wajalie hekima na ufahamu wako ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wote; Uwajalie elimu na shauri lako Kwa ajili ya mapadre wako; wajalie wakuheshimu na wakuogope Kwa ajili ya mapadre wote; Wajalie subira na upendo Kwa ajili ya mapadre wote; wajalie utii na upole Kwa ajili ya mapadre wote; uwajalie hamu kuu ya kuokoa roho za watu Kwa ajili ya mapadre wote; wape fadhila za imani, matumaini na mapendo Kwa ajili ya mapadre wote; Wajalie upendo mkuu kwa Ekaristi Tunakuomba uwajalie mapadre wote; Waheshimu uhai na hadhi ya mtu ee Bwana Tunakuomba uwajalie mapadre wote nguvu na bidii katika kazi zao ee Bwana Tunakuomba uwajalie mapadre wote amani katika mahangaiko yao ee Bwana Tunakuomba uwajalie mapadre wote upendo mkuu kwa Utatu Mtakatifu ee Bwana Tunakuomba uwajalie mapadre wote upendo mkuu kwa Bikira Maria ee Bwana Uwajalie mapadre wote wawe mwanga wa Kristo ee Bwana Uwajalie mapadre wote, wawe chumvi kwa ulimwengu ee Bwana Uwajalie mapadre wote, wajizoeze kujitoa sadaka na kujinyima ee Bwana Uwajalie mapadre wote, wawe watakatifu kimwili, kiakili na kiroho ee Bwana Uwajalie mapadre wote wawe watu wa sala ee Bwana Uwajalie mapadre wote wawe kioo cha imani kwako ee Bwana Uwajalie mapadre wote wajali sana wongofu wetu ee Bwana Uwajalie mapadre wote wawe waaminifu kwa wito wao wa kikuhani ee Bwana Uwajalie mapadre wote, ili mikono yao ibariki na kuponya ee Bwana Uwajalie mapadre wote wawake moto wa mapendo yako ee Bwana Uwajalie mapadre wote hatua zao zote ziwe kwa ajili ya utukufu wa Mungu ee Bwana Uwajalie mapadre wote wajazwe na Roho Mtakatifu na uwajalie karama zake kwa wingi ee Bwana.
Tuombe. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, usikie sala tunazokutolea kwa ajili ya mapadre wetu. Uwajalie wafahamu waziwazi kazi uliyowaitia kuifanya, uwape neema zote wanazohitaji ili waitikie wito wako kwa ushujaa, kwa upendo, na majitoleo yenye udumifu katika mapenzi yako matakatifu. Amina.
Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie Kristo utuhurumie Kristo utuhurumie Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie Kristo utusikie Kristo utusikilize Baba wa mbinguni Mungu Utuhurumie Mwana, Mkombozi wa dunia Mungu Utuhurumie Roho Mtakatifu Mungu Utuhurumie
Updated at: 2024-05-27 07:14:15 (9 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie Kristo utuhurumie Kristo utuhurumie Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie Kristo utusikie Kristo utusikilize Baba wa mbinguni Mungu Utuhurumie Mwana, Mkombozi wa dunia Mungu Utuhurumie Roho Mtakatifu Mungu Utuhurumie Utatu Mtakatifu Mungu mmoja Utuhurumie Moyo wa Yesu Mwana wa Baba wa Milele Utuhurumie Moyo wa Yesu uliotungwa na Roho Mtakatifu mwilini mwa Mama Bikira Maria Utuhurumie Moyo wa Yesu ulioungana na Neno wa Mungu Utuhurumie Moyo wa Yesu ulio na utukufu pasipo mfano Utuhurumie Moyo wa Yesu, hekalu takatifu la Mungu Utuhurumie Moyo wa Yesu, hema la Yule aliye juu Utuhurumie Moyo wa Yesu tanuru lenye kuwaka mapendo Utuhurumie Moyo wa Yesu, nyumba ya Mungu na mlango wa Mbingu Utuhurumie Moyo wa Yesu, tanuru yenye kuwaka mapendo Utuhurumie Moyo wa Yesu, chombo cha haki na upendo Utuhurumie Moyo wa Yesu, unaojaa upendo na wema Utuhurumie Moyo wa Yesu, kilindi cha fadhila zote Utuhurumie Moyo wa Yesu, unaostahili sifa zote Utuhurumie Moyo wa Yesu, unaotawala mioyo yote Utuhurumie Moyo wa Yesu, zinamokaa hazina za hekima na elimu Utuhurumie Moyo wa Yesu, uliopendelewa na Mungu Baba Utuhurumie Moyo wa Yesu, uliotuenezea maziada yake Utuhurumie Moyo wa Yesu, mtamaniwa wa vilima vya milele Utuhurumie Moyo wa Yesu, wenye uvumilivu na huruma nyingi Utuhurumie Moyo wa Yesu, tajiri kwa wote wenye kukuomba Utuhurumie Moyo wa Yesu, chemchemi ya uzima na utakatifu Utuhurumie Moyo wa Yesu, malipo kwa dhambi zetu Utuhurumie Moyo wa Yesu, ulioshibishwa matusi Utuhurumie Moyo wa Yesu, uliovunjika kwa sababu ya ubaya wetu Utuhurumie Moyo wa Yesu, uliotii mpaka kufa Utuhurumie Moyo wa Yesu, uliochomwa kwa mkuki Utuhurumie Moyo wa Yesu, chemchemi ya faraja zote Utuhurumie Moyo wa Yesu, uzima na ufufuo wetu Utuhurumie Moyo wa Yesu, amani na upatanisho wetu Utuhurumie Moyo wa Yesu, sadaka ya wakosefu Utuhurumie Moyo wa Yesu, unamokaa wokovu wao wenye kukutumaini Utuhurumie Moyo wa Yesu, matumaini yao wenye kuzimia kwako Utuhurumie Moyo wa Yesu, sababu ya furaha ya watakatifu wote Utuhurumie Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia Utusamehe Bwana Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia Utusikilize Bwana Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia Utuhurumie
Kiongozi: Yesu mwenye Moyo mpole na mnyenyekevu, Wote: Ufanye mioyo yetu ifanane na Moyo wako
TUOMBE: (W) Ee Mungu Mwenyezi milele, uuangalie Moyo wa mwanao mpendelevu, pia na heshima na malipo aliyokutolea kwa ajili ya wenye dhambi, uridhike, uwaondolee wenye kuomba toba kwako kwa njia ya huyo Mwanao Yesu Kristo anayeishi na kutawala nawe pamoja na Roho Mtakatifu, Mungu milele. Amina.
Ee Mungu Mwenyezi wa milele, mpaji wa mema yote, unayetusamehe na kutulinda. Utujalie sisi tunaokusihi, tufurahie hali njema ya hewa na mvua tunayoitamani na kuhitaji. Tutumie daima vipawa vya wema wako kwa ajili ya utukufu wa jina lako, na kwa ajili ya wokovu watu. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana
Updated at: 2024-05-27 07:14:08 (9 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Mungu Mwenyezi wa milele, mpaji wa mema yote, unayetusamehe na kutulinda. Utujalie sisi tunaokusihi, tufurahie hali njema ya hewa na mvua tunayoitamani na kuhitaji. Tutumie daima vipawa vya wema wako kwa ajili ya utukufu wa jina lako, na kwa ajili ya wokovu watu. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana watu Yesu Kristo Mwanao, anayeishi na kutawala nawe katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu, daima na milele. Amina. `
Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Salamu Maria,….
Ndimi Mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyonena. Salamu Maria, …… Neno wa Bwana akatwaa Mwili, akakaa kwetu. Salamu Maria, …..
Utuombee, ee Mzazi Mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo.
Updated at: 2024-05-27 07:14:10 (9 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Salamu Maria,….
Ndimi Mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyonena. Salamu Maria, …… Neno wa Bwana akatwaa Mwili, akakaa kwetu. Salamu Maria, …..
Utuombee, ee Mzazi Mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe:
Tunakuomba ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika, kwamba, Kristo Mwanao amejifanya mtu: kwa mateso na Msalaba wake, utufikishe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu, Amina.