Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.
Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?
Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.
Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.
Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.
Share kwa wengine ili nao wazinduke.
Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
-
Familia, Mapenzi na Mahusiano
πKitabu cha SIRI ZA MWANAMKEπ§ππ
Original price was: Sh7,500.Sh3,000Current price is: Sh3,000. Download Now
Editor: Melkisedeck Leon Shine. About Me | Contact Me | LinkedIn | TikTok | WhatsApp
Read and Write Comments
Recommended Posts
Kutumia Vifaa vya Kufanya Mapenzi: Kuingiza Burudani katika Uhusiano wako
Je, ngono/kufanya mapenzi ni jambo la faragha au unajisikia huru kuzungumzia kuhusu hilo?
Kuimarisha Uzoefu wa Kufanya Mapenzi: Jinsi Mawasiliano yanavyosaidia
Mwanamme: Jinsi ya Kuwa na Ushirikiano na Jamii na Wanaume Wenzako
Je, kuna umuhimu wa kujadili maoni na mitazamo yako kuhusu ngono/kufanya mapenzi?
Je, kuna umuhimu wa kujadili kuhusu upendeleo wako wa ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?
Kuvunja Vizuizi vya Aibu katika Kufanya Mapenzi: Njia za Kuweka Urahisi na Utulivu
Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya elimu na mafunzo