Author name: DIN - Melkisedeck Leon Shine

SALA YA KUUABUDU MOYO MTAKATIFU WA YESU KATIKA EKARISTI TAKATIFU

Kwa nguvu zangu zote za moyo wangu/ ninakuabudu ee Moyo Mtakatifu/ na Mwabudiwa sana,/ Moyo Mtakatifu wa Bwana wetu Yesu Kristu/ ambao ninataka kumpenda/ na kukusalimu kwa usikivu unaoendelea./ Kamwe nisikuudhi tena/ kwa sababu Wewe ni Mwema sana;/ Ee Mwema sana./ Ee Moyo Mtakatifu sana/ ninakupenda/ na ninataka kukupenda zaidi ya vitu vyote,/ kwa nguvu zangu zote/ na kwa uwezo wangu wote,/ ninatamani kuwa mali yako/ Wewe uliyejitoa Msalabani kwa ajili yangu/ kwa mateso makali./ Unionee huruma na udhaifu wangu/ na usiniruhusu kupotea./

Ninajitoa kabisa kwako/ ee moyo wa mapendo,/ kwa makusudi kuwa utu wangu,/ maisha na mateso yangu/ yalipie kukupenda,/ kukuheshimu/ na kukutukuza Wewe sasa na milele./ Ninakupenda ee Moyo Mwabudiwa wa Mwokozi wangu,/ ninakuomba kwako/ uamuru moyo wangu na kila kitu ndani yangu/ kikutukuze sasa na milele./ Amina.

(Na Mt Margareta Maria Alakoki)

Hadithi: Mkasa wa kusisimua, Jifunze kitu hapa

Watu wawili๐Ÿ‘ฌ walikuwa wanakunywa pombe๐Ÿบ๐Ÿป baa. Wakati wanakunywa wakaanza kubishana๐Ÿ™…๐Ÿพโ€โ™‚ na baadaye ule ubishi ukawa ugomvi.

Mmoja akamrukia mwenzake akaanza kumpiga. Baada ya kumpiga kwa muda mrefu akagundua kuwa mwenzake hapumui tena.

Kumbe amemwua mwenzie.๐Ÿ˜ฐ

Ndipo alipoanza kukimbia๐Ÿƒ๐Ÿพ huku shati laki likiwa limechafuka sana na damu. Wale waliyokuwa wanauangalia ule ugomvi wakaanza kumfukuza.
๐Ÿƒ๐Ÿพ ๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™€๐Ÿƒ๐Ÿพ๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™€๐Ÿƒ๐Ÿพ๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™€๐Ÿƒ๐Ÿพ

Huyu mwuaji akakimbilia kwenye ๐Ÿก๐Ÿƒ๐Ÿพnyumba ya mtu mmoja mcha Mungu na akamwomba yule mtu amfiche maana ameua mtu na watu walikuwa wanamfukuza.

Yule mcha Mungu akasema nitakuficha wapi wakati mimi nina chumba kimoja tu?๐Ÿ˜จ

Yule mwuaji akamjibu akamwambia acha kuendelea kupoteza wakati fikiria tu mahali pa kunificha. Yule mcha Mungu akavua shati๐Ÿ‘” lake safi akampa yule mwuaji alafu yeye akachukua lile shati la muaji lililojaa damu akalivaa.

Akampa sharti yule mwuaji na kumwambia tunza shati langu usilichafue. Yule mcha Mungu alipofungua mlango wa chumba chake wale watu wakamvamia๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™€๐Ÿƒ๐Ÿพ๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™€๐Ÿƒ๐Ÿพ๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™€๐Ÿƒ๐Ÿพ๐Ÿƒ๐Ÿพ๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™€๐Ÿƒ๐Ÿพ๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™€๐Ÿƒ๐Ÿพ na kumpiga sana wakijua yeye ndo mwuaji huku mwuaji akiondoka salama na kurudi kwake.

Baada ya kumpiga sana yule ndugu akapelekwa polisi๐Ÿ‘ฎ๐Ÿพ๐Ÿ‘ฎ๐Ÿฝโ€โ™€ na baadaye akapelekwa mahakamani na akahukumiwa kunyongwa๐Ÿ‘ด๐Ÿผ kwa kumwua mtu mwingine.

Yule mwuaji halisi akiwa kule nyumbani alijisikia vibaya sana๐Ÿ˜ž akaenda mahakamani akajisalimisha akasema yeye ndiye aliyeua, yule ndugu aachiwe huru.

Hakimuโš– akamwambia umechelewa, yule ndugu kesha nyongwa.

Alilia๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ฉ sana na kujiambia kuwa yule mtu amekufa kwa kosa ambalo sio lake.๐Ÿ˜ฐ

Akakumbuka maneno ya mwisho ya yule ndugu _*”LITUNZE SHATI LANGU USILICHAFUE.”*_

Wapendwa,
YESU alikufa kwa ajili ya dhambi zako na zangu. Alichukua vazi letu lililochafuliwa na uchafu wa dhambi zetu akatupa vazi Lake takatifu la haki. YESU aliuawa kwa kosa lako na langu. Akatupa haki Yake na kutuambia tusichafue tena maisha yetu.

Kuendelea kutenda dhambi baada ya yale ambayo Yesu ametufanyia ni kuidharau sana kazi ya msalaba na kuikanyagia chini Damu Yake ambayo tumesafishwa kwayo.

Ni kushindwa kuthamini kuwa kuna mtu alishakufa kwa ajili yetu. Ni kushindwa kutambua uthamani wa wokovu ambao tumeupokea.

Wapendwa,
*Tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii?*

T A F A K A R I

Mambo ya kutafakari unapokuwa katika shida kubwa, unapoelekea kukata tamaa

Tafakari Kuhusu Wakati wa Shida

Leo tunatafakari kuhusu wakati wa shida. Maisha ya mtu yanabadilika wakati wowote kwa namna yoyote. Yanaweza yakawa mazuri mpaka ukashangaa au yanaweza yasiwe mazuri kama unavyotarajia. Yote hayo ni sehemu ya maisha.

“Nimejifunza kuwa na kuridhika na hali yoyote niliyo nayo. Najua jinsi ya kuwa na hali duni, najua jinsi ya kuwa na hali ya wingi. Katika hali zote na mambo yote, nimefundishwa jinsi ya kushiba na jinsi ya kuwa na njaa, jinsi ya kuwa na wingi na jinsi ya kupungukiwa.” (Wafilipi 4:11-12)

Kumbuka Wakati wa Matatizo

Unapokua na matatizo makubwa katika maisha, kumbuka haya yafuatayo:

1. Mungu Yupo na Anakuona

Mungu yupo na anakuona. Mwambie matatizo yako, huo ndio wakati wake wa kuonyesha uwepo wake na nguvu zake. Wewe tu kusema na Mungu kwa utayari na uwazi, hivyo utakao kuwezesha kupata au kutatua tatizo lako.

“Naomba BWANA akujibu siku ya dhiki, jina la Mungu wa Yakobo likuinue.” (Zaburi 20:1)
“Mchungueni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote.” (1 Mambo ya Nyakati 16:11)
“Bwana ni ngome yao katika wakati wa shida.” (Zaburi 37:39)

2. Matendo na Maamuzi Yako

Maneno, vitendo, na maamuzi yako ndiyo yanaweza yakawa njia ya kutatua matatizo yako. Usiogope kuchukua hatua zinazohitajika. Tafuta hekima na uongozi kutoka kwa Mungu katika kila hatua unayochukua.

“Yehova atakuelekeza siku zote, na kukusibisha katika nchi yenye ukame, na kukuimarisha mifupa yako. Utakuwa kama bustani iliyomwagiliwa, na kama chemchemi ya maji ambayo maji yake hayatapungua.” (Isaya 58:11)
“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako.” (Mithali 3:5-6)
“Nawafundisha njia iliyo njema na adili; msiiachilie sheria yangu.” (Mithali 4:11-13)

3. Matatizo Hayako Sio Mwisho wa Maisha

Tatizo lako sio mwisho wa maisha yako, sio mwisho wa yote mazuri ya jana, leo, na kesho. Bado unayo mambo mengi mazuri yanakungojea. Mungu anapanga mambo mazuri kwa ajili ya wale wanaompenda na kumtumainia.

“Maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu, asema Bwana, ni mipango ya amani na si ya mabaya, ili niwape tumaini katika siku zenu za usoni.” (Yeremia 29:11)
“Na tusiache kutenda mema, kwa maana tutavuna kwa wakati wake tusipozimia roho.” (Wagalatia 6:9)
“Bwana atakamilisha mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; usiache kazi ya mikono yako.” (Zaburi 138:8)

4. Uangalizi wa Tatizo

Kumbuka tatizo lako linaweza likawa sio kubwa ila wewe ndio unaliona kubwa. Wewe sio wa kwanza kuwa na tatizo kama hilo, wengine hayo ndo maisha yao. Angalia kwa mtazamo wa matumaini na uombe hekima ya Mungu ili uweze kuona njia ya kutoka kwenye tatizo lako.

“Mkipungukiwa na hekima, na aombe kwa Mungu, naye atampa kwa ukarimu wala hachukii.” (Yakobo 1:5)
“Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.” (2 Wakorintho 4:16)
“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” (Wafilipi 4:13)

Kwa hivyo, wakati wa shida, ni muhimu kujikumbusha kwamba Mungu yupo, anakusikiliza, na yupo tayari kukusaidia. Usiache matumaini, endelea kuamini na kutenda kwa hekima na imani, ukijua kwamba matatizo yako ni sehemu ya safari yako ya kiroho na Mungu anapanga mazuri mbele yako.

Mafundisho kuhusu Toharani

Toharani ni mahali gani?

Toharani ni mahali pa mateso zinakosafishwa roho ambazo hazikutimiza kitubio vizuri baada ya kuungama dhambi. (1Kor 3:15, 1Pet 1:7).

 


 

Je, hatuwezi kupunguza mateso ya roho za marehemu waliokwenda toharani?

Ndiyo: twaweza kupunguza hata kuyamaliza kwa kuwasalia na kuwapatia rehema na hasa kwa kuadhimisha Misa kwa ajili yao. (2Mik 12:38-46)

 


 

Toharani maana yake nini?

Toharani maana yake kuna hali ya muda ambayo huruma ya Mungu inawatakasa marehemu waliofariki dunia katika urafiki naye lakini bila ya usafi kamili unaotakiwa kwa kuingia mbinguni. Sisi tunaweza kuharakisha utakaso wao kwa kumtolea Mungu sala na sadaka, hasa ekaristi. Yuda Mmakabayo โ€œalichanga fedha kwa kila mtu jumla drakma elfu mbili, akazipeleka Yerusalemu kutoa sadaka ya dhambi.
Kwa kufanya hivi alitenda vema na kwa haki, kwa kuwa aliukumbuka ufufuo wa wafu. Maana kama asingalitumaini ya kuwa wale waliokufa watafufuka, ingalikuwa kazi bure isiyo na maana kuwaombea wafu. Lakini kwa kuwa aliufikiri utukufu wa thawabu waliowekewa wale wafao katika utauwa, wazo lake lilikuwa takatifu na la kicho. Ndiyo sababu alifanya upatanisho kwa wafu ili wafunguliwe dhambi zaoโ€ (2Mak 12:43-46). Imani hiyohiyo iliongoza Wakristo wa kwanza kuwafanyia marehemu ibada ambayo haieleweki vizuri, lakini hailaumiwi na Mtume Paulo: โ€œKama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?โ€ (1Kor 15:29).

Maswali na Majibu kuhusu Rehema

Rehema ni nini?
Rehema ni msamaha au ondoleo la adhabu ya dhambi tulizostahili sababu ya dhambi zilizokwisha ondolewa

Rehema hutolewa na nani?
Rehema hutolewa na Kanisa Katoliki kwa kutugawia mastahili ya Yesu Kristo, Bikira Maria na Ya Watakatifu

Kuna Rehema za namna ngapi?
Rehema za namna mbili
1. Rehema kamili
2. Rehema pungufu (Rehema isiyo kamili)

Rehema kamili ni nini?
Rehema kamili ni msamaha wa kufutiwa adhabu zote za muda za dhambi

Rehema isiyo kamili (pungufu) ni nini?
Rehema isiyo kamili (pungufu) ni msamaha wa kupunguziwa adhabu ya dhambi

Adhabu za dhambi huondolewa kwa namna gani? Jinsi ya kupata rehema
Adhabu za dhambi huondolewa kwa;
1. Kufanya malipizi au majuto kamili
2. Kuvumilia taabu na mateso katika maisha
3. Kuvishinda vishawishi na majaribu
4. Kusali sala mbalimbali
5. Kuomba Misa kwa ajili hiyo.
6. Kusoma neno la Mungu na kulitafakari na kulinganisha na maisha yetu ya kila siku
7. Utakaso wa Toharani kama adhabu hizi hazikuondolewa duniani

Kipimo cha Rehema ni nini?
Kipimo cha Rehema hutegemea uzito wa majuto na mapendo mtu aliyonayo kwa Mungu Muumba wake. (1Kor 9:11)

Mtu akitaka kupata Rehema za Kanisa Katoliki yampasa nini?
Mtu akitaka kupata Rehema za Kanisa Katoliki yampasa;
1. Kujua na kufuata utaratibu unaotolewa na Kanisa Katoliki wa kupata Rehema
2. Awe katika hali ya neema ya Utakaso
3. Kufanya matendo yote yanayotakiwa kwa kupata rehema hiyo, kwa mfano;
a). Hija au Kuhiji katika mwaka wa Jubilei katika Kanisa lililo teuliwa na Askofu
b). Kufanya mafungo – Kama vyama vya kitume
c). Kuzuru makaburi (Kutembelea) yaliyobarikiwa
d). Katika hatari ya kufa padri hutoa rehema pamoja na Sakramenti ya wagonjwa
e). Kusali kwa nia za Baba Mtakatifu
Shopping Cart