Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Je, ni kweli matumizi ya dawa za kulevya ni mojawapo ya sababu zinazochangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU)

Dawa za kulevya zenyewe hazisababishi UKIMWI na magonjwa ya zinaa. Lakini utumiaji wa dawa za kulevya hurahisisha kupata na kuenea kwa magonjwa haya. Dawa hizi hudhoofisha mwili na kinga ya mwili. Hivyo basi hurahisisha virusi vya magonjwa kuingia mwilini mwa mtumiaji kiurahisi.

Matumizi ya dawa za kulevya huwafanya watumiaji kusahau hatari za kuwa na wapenzi wengi pamoja na kufanya ngono na watu usiofahamu hali za afya zao. Hujisahau kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu. Vilevile husahau majukumu yao kama vile mke, watoto na familia nzima kwa ujumla.
Dawa za kulevya zinazoingia mwilini kwa njia ya sindano husababisha uwezekano mkubwa wa kuenea kwa virusi vya UKIMWI (VVU) kwa watumiaji pindi wanapochangia sindano kujidungia dawa hizo mwilini. Pia dawa za kulevya huchangia kuenea kwa virusi vya UKIMWI kwa kuwa watumiaji hujii ngiza katika biashara ya ngono i ili kuweza kujipatia fedha za kununulia dawa hizo.

Je, mtu anawezaje kuacha kutumia dawa za kulevya na itamchukua muda gani kurudia hali yake ya kawaida?

Kitu muhimu ni kwamba, kweli uwe umedhamiria kuacha. Hatua ya kwanza ni kujiuliza kwa nini unatumia dawa za kulevya. Pale utakapojua ni nini ulikuwa unahitaji katika dawa za kulevya ni rahisi kutimiza malengo hayo kwa njia za kiafya zaidi. Jaribu kupunguza taratibu kiasi na muda wa kutumia dawa za kulevya. Pia tumia vitamini na madini kuimarisha afya yako. Jitenge na watumiaji wengine wa dawa za kulevya na sehemu ulizokuwa ukienda kupata dawa za kulevya. Kama hutofanikiwa katika hatua ya kwanza usikate tamaa! Watu hushindwa kuacha katika jaribio la kwanza! Jaribu tena!

Kuacha dawa za kulevya ni sawasawa na kupata nafuu ya ugonjwa, ni rahisi zaidi kufanikiwa kama utapata ushirikiano zaidi kutoka kwa marafiki au wanafamilia. Unaweza vilevile kuomba ushauri kutoka kwa watoa nasaha au madaktari. Msaada wa kitabibu ni muhimu kwa wale waliozoea kutumia hiroini na pombe, kwani mara nyingi hupata madhara yatishiayo maisha pale wanapojaribu kuacha dawa za kulevya.
Ni vigumu kusema utachukua muda gani kuacha kutumia dawa za kulevya, kwa sababu i natofautiana kati ya mtu na mtu.

Je, kwa nini watu waanzao kutumia dawa za kulevya hupenda kuendelea kuzitumia?

Hii ndio hasa sababu kwa nini dawa za kulevya ni hatari! Mara unapozizoea unakuwa na ugumu wa kuendesha maisha yako bila dawa za kulevya. Kwa dawa nyingi za kulevya ubongo huzoea kuwepo kwake kwenye damu na dawa zaidi na zaidi huhitajika i ili kuendeleza hali hiyo. Hii i ii ina maana kadri muda unavyoenda ndivyo unavyoongeza kiasi cha dawa za kulevya unachokihitaji.
Pale utakapojaribu kupunguza kiasi cha matumizi ya dawa za kulevya au kuacha kabisa unaweza kupata hali ya kimaumbile au kiakili i i itokeayo kutokana na kuacha kitu ulichozoea. Hali hii inaweza i isiwe ya kufurahisha, yenye kuumiza na pengine hatari kwa maisha yako. Mara mtu anapozizoea dawa za kulevya haiwi tu tabia bali ugonjwa. Watu wengi wanaotegemea dawa za kulevya hawazitumii kwa kujifurahisha bali kuzuia maumivu yasababishwayo na kuacha kitu ulichozoea. Njia nzuri ya kuzuia hali hii ni rahisi: kuwa jasiri na sema HAPANA. Usijaribu dawa za kulevya.

Shopping Cart