Dawa za kulevya zenyewe hazisababishi UKIMWI na magonjwa ya zinaa. Lakini utumiaji wa dawa za kulevya hurahisisha kupata na kuenea kwa magonjwa haya. Dawa hizi hudhoofisha mwili na kinga ya mwili. Hivyo basi hurahisisha virusi vya magonjwa kuingia mwilini mwa mtumiaji kiurahisi.
Matumizi ya dawa za kulevya huwafanya watumiaji kusahau hatari za kuwa na wapenzi wengi pamoja na kufanya ngono na watu usiofahamu hali za afya zao. Hujisahau kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu. Vilevile husahau majukumu yao kama vile mke, watoto na familia nzima kwa ujumla.
Dawa za kulevya zinazoingia mwilini kwa njia ya sindano husababisha uwezekano mkubwa wa kuenea kwa virusi vya UKIMWI (VVU) kwa watumiaji pindi wanapochangia sindano kujidungia dawa hizo mwilini. Pia dawa za kulevya huchangia kuenea kwa virusi vya UKIMWI kwa kuwa watumiaji hujii ngiza katika biashara ya ngono i ili kuweza kujipatia fedha za kununulia dawa hizo.
Recent Comments