Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Ni dawa zipi zilizopigwa marufuku Tanzania na nini hutokea pale mwingizaji anapokamatwa?

Hapa Tanzania matumizi, umilikaji, usafirishaji na kuhusika katika dawa za kulevya kama vile bangi, hiroini, kokaini na mirungi yamepigwa marufuku. Hii ni pamoja na dawa ambazo zimethibitishwa na daktari kuwa zisitumike kwa matibabu. Kwa Tanzania β€œgongo”pia ni haramu.
Polisi akimkamata mtu anayekwenda kinyume na sheria, humpeleka mtu huyo mbele ya vyombo vya sheria na atahukumiwa ikithibitika kuwa ana hatia. Sheria i inatoa adhabu kali kwa makosa yanayohusiana na dawa za kulevya. Faini ya shilingi milioni 10 za Kitanzania au kifungo cha maisha au vyote kwa pamoja.

Kwa nini watu wanaotumia dawa za kulevya hukonda?

Dawa za kulevya huharibu ufanyaji kaza wa kawaida wa mfumo wa mwili hasa tumbo na utumbo wa watumiaji
hushindwa kufyonza virutubisho vidogo kama vile
vitamini, madini kutoka kwenye chakula na kwenda kwenye mfumo wa damu. Hiki ndicho kinachowafanya wakonde. Isitoshe, hupunguza uwezo wa mwili kujikinga na maradhi na hivyo huuweka mwili katika hatari ya kuambukizwa na magonjwa likiwemo gonjwa hatari la UKIMWI.

Shopping Cart