Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Je, ni kweli kwamba kuvuta bangi kunaongeza akili na uwezo wa kufikiri?

Hapana, hii si kweli! Vijana wanaoamini kwamba wana uwezo wa kufikiri baada ya kuvuta bangi kwa sababu inawapa hisia ya kuzoea mihemko ya kusikia vizuri au kufahamu kwa haraka. Lakini ni kawaida kwamba uvutaji wa bangi unaathiri shule, kazi na shughuli nyingine kinyume na matarajio ya mafanikio. Siku zote vijana wavutaji bangi wanapoteza ari shuleni au mafunzoni. Wanashindwa kuweka malengo ya maisha yao ya baadaye.

Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hupunguza mawazo?

Bangi hupunguza mawazo kwa muda mfupi kwani huleta hisia za furaha na utulivu. Lakini hata hivyo matatizo hubakia palepale na mara nyingi huongezeka hapo baadaye. Watu wanaovuta bangi huikimbia dunia halisi na huingia dunia ya ndoto kwa muda mfupi. Mara hisia zilizoletwa na bangi zinapoondoka, aghalabu matatizo huwa mabaya zaidi kuliko mwanzo. Matumizi ya bangi huahirisha na kuchelewesha tu utatuzi wa matatizo.

Nini matokeo ya unusaji/uvutaji wa petroli kwa vijana?

Kama kijana akinusa au kuvuta petroli kupitia puani au mdomoni, petroli hiyo huingia kwenye mapafu na sehemu zote mwilini.
Madhara ya unusaji au uvutaji petroli ni sawa kabisa na pombe. Baada ya kunusa/kuvuta petroli mtuamiaji hujisikia kizunguzungu na kulewa. Wengine huhisi kama kwamba wanaota na kujisikia furaha. Lakini wengine hujisikia kuumwa na kusinzia.
Unusaji/uvutaji wa petroli ni hatari sana na hata huweza kusababisha vifo kwani petroli humfanya mtu apoteze fahamu, huharibu mapafu na wengine hufa kwenye ajali. Hii hutokana na kushindwa kutoa uamuzi ufaao wanapokabiliwa na hali zinazoweza kusababisha ajali, hasa barabarani.
Matumizi ya muda mrefu ya petroli huweza kumsababishia madhara mtumiaji kama kutokwa na damu puani, kupoteza hamu ya kula, kuwa dhaifu, kupata matatizo ya mtindio wa ubongo, kupatwa na magonjwa ya figo, moyo, mapafu na kuharibika maini.

Shopping Cart