Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tangawizi

MAHITAJI

Unga – 2 Vikombe

Cocoa ya unga – 1 Kijiko cha supu

Sukari ya hudhurungi – 1 Kikombe

Siagi – ¾ Kikombe

Yai – 1

Molasses – ¼ Kikombe

Baking soda – 2 vijiko vya chai

Mdalasini wa unga – 1 kijiko cha chai

Tangawizi mbichi – 1 kijiko cha supu

Karafuu ya unga – ½ kijiko cha chai

Chumvi ½ kijiko cha chai

Vanilla ½ kijiko cha chai

MAANDALIZI

Katika bakuli, chunga unga, baking soda, chumvi na cocoa. Weka kando.
Washa oven lipate moto huku unatayarisha biskuti.
Katika bakuli jengine, mimina siagi na sukari upige kwa mashini ya keki hadi mchanganyiko uwe laini kama dakika mbili.
Mimina molasses na yai ndani ya mchanganyiko wa siagi na sukari uchanganye vizuri.
Mimina unga kidogo kidogo huku unachanganya na mwiko hadi unga wote umalizike.
Mimina mdalasini, karafuu na tangawizi, changanya vizuri.
Weka mchanganyiko wako ndani ya friji kama masaa mawili. (Ukipenda unaweza kuhifadhi mchanganyiko wako ndani ya mfuko wa freezer na uoke siku nyengine.)
Tengeneza viduara vidogo vidogo.

Chovya kila kiduara katikati sukari, kisha panga kwenye treya ya kuoka

Rudisha viduara katika friji kama nusu saa.

Oka katika oven 350ºF kwa muda wa dakika 15.

Toa biskuti kwenye oven na uache zipoe kama dakika kumi.
Panga kwenye sahani tayari kuliwa.

Vyakula vya Kukuza nywele na kuzifanya ziwe na Afya

Kuwa na nywele zenye afya nzuri ni muhimu kwa wote bila kujali jinsi, hali hii husababisha wengi kutumia madawa ya aina mbalimbali ya kuhakikisha nywele zao zinastawi na kuwa na muonekano mzuri.
Kwa bahati mbaya, wengi waliotumia madawa yanayotengenezwa kwa kemikali hujikuta katika wakati mgumu siku za usoni wakikabiliwa na matatizo ya nywele kukatika na hata kupata madhara katika ngozi ya kichwa.

Njia bora na salama zaidi ya kustawisha nywele, kuzifanya ziwe na mvuto wa aina yake bila kujali wewe ni mtu wa asili ya bara Asia, Afrika au Marekani, ni kula vyakula vyenye virutubisho muhimu kwa afya ya nywele.

Vifuatavyo ni sehemu ya vyakula ambavyo hupatikana kirahisi barani Afrika na kwa bei nafuu, ambavyo vitakupa afya bora zaidi ya nywele zako.

1. Yai

Nywele za binadamu zina protini ambayo zimeumbiwa. Hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa zina protini ya kutosha, na hilo hufanyika kupitia vyakula. Protini ni nguzo kuu ya nywele za binadamu, na yai ni moja kati ya vyakula vyenye utajiri mkubwa wa protini. Hakikisha unakula yai angalau mara tatu kwa wiki.

2. Spinachi

Nywele zinahitaji madini ya chuma ili ziweze kuwa katika hali nzuri ya afya. Kukosekana kwa madini ya chuma husababisha nywele kunyonyoka. Mwili unapokosa madini ya chuma, hewa ya oxygen na virutubisho hushindwa kufika vizuri kwenye mizizi ya nywele hivyo hufanya nywele kuwa dhaifu na zisizo na muonekano mzuri.

Mboga za majani aina ya spinachi ni suluhisho, kwakuwa zina madini ya chuma kwa wingi ambayo seli za nywele huhitaji.

3. Jamii ya Machungwa, Limao

Mwili wa binadamu huhitaji vitamini C ambayo husaidia kuhuisha utendaji wa madini ya chuma. Hivyo, unapaswa kuongeza matunda ya jamii ya ‘citrus’, kama vile machungwa, chenza, balungi na limao. Pia, unaweza kutumia na asali pamoja.

Vitamini C husaidia katika ukuaji wa nywele kusaidia usambaaji wa virutubisho na ukuaji wa haraka wa nywele.

4. Karoti

Ni muhimu sana kuhakikisha unakunywa juice ya karoti kila siku, kama unataka nywele zako zikue haraka zikiwa na mwonekano mzuri wenye afya. Vitamini A inayopatikana kwenye karoti ni muhimu sana kwa ukuaji wa seli za nywele. Kumbuka nywele zina tishu ambazo hukua haraka zaidi katika mwili.

Karoti ina mafuta asili yanayofahamika kama ‘sebum’ na mizizi ambayo husaidia kukuza nywele kwa haraka.

5. Parachichi

Tunda aina ya parachichi lina kazi nyingi sana mwilini kama matunda mengine, lakini hili ni tunda la kipekee amnbalo lina utajiri wa vitamini E ambayo husaidia mzunguko wa damu na katika hilo husaidia mfumo wa ukuaji wa nywele kwa haraka.

Tunda hili husaidia kuhuisha na kurekebisha mafuta na kiwango cha PH (inayosafisha kemikalii mwilini) ambavyo kama vitazidi kwenye mwili vinaweza kusababisha kusimama kwa ukuaji wa nywele, yaani nywele hudumaa.

Kwa faida zaidi, vitamin E inayopatikana kwenye parachichi kwa wingi husaidia zaidi afya ya moyo wa binadamu na zaidi ngozi. Hakikisha unapata tunda hili kadiri iwezekanavyo.

Hivi ni baadhi tu ya vyakula na matunda kwa ukuaji mzuri wa nywele zako. Kama unatumia vizuri mlo wako, utakuwa adimu sana kutumia mafuta yenye kemikali ambayo yanaweza kukuletea madhara mabaya.

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tende

MAHITAJI

Unga – 4 Vikombe vya chai
Sukari ya laini (icing sugar) – 1 Kikombe cha chai
Baking powder – 2 Vijiko vya chai
Mayai – 2
Siagi au margarine – 1 Kikombe cha chai
Vanilla -1 Kijiko cha chai
Maziwa ya kuchanganyia – kiasi
Tende iliyotolewa koko – 1 Kikombe
ufuta (sasame) kiasi 1/4 kikombe

MAANDALIZI

Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika mashine.
Kisha tia mayai, vanilla na halafu maziwa kidogo kidogo hadi mchanganyiko ushikamane.
Gawanya madonge mawili na usukume kama chapati, lakini sio nyembamba sana.
Tandaza tende robo ya duara na unyunyize ufuta duara zima: kisha kunja hadi mwisho na ukate kate, kisha upange katika trei ya kuvumbika.
Vumbika (bake) moto wa 350°F kwa muda wa dakika 20 au hadi vigeuke rangi na viwive.
Zikisha iiva ziache zipowe na zitakuwa tayari kuliwa.

Thamani ya Neno “Nimekusamehe”

Ni jambo jema kusamehe wale waliotukosea. Neno “Nimekusamehe” ni zuri kusikia masikioni kuliko neno “Ninakupenda”. Maana kusamehewa ni zaidi ya kupendwa kwani Msamaha ni matokeo ya Upendo.

Melkisedeck Leon Shine

Neno “Nimekusamehe”

Neno “Nimekusamehe” ni moja ya maneno yenye nguvu kubwa sana katika lugha yoyote ile. Ni neno ambalo linabeba uzito wa moyo mzito uliojaa maumivu na hatimaye kuachilia mzigo huo. Ni jambo jema kusamehe wale waliotukosea, kwani msamaha unafungua milango ya amani na upatanisho.

“Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.” (Mathayo 6:14)
“Basi, vaeni kama wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu; mkichukuliana na kusameheana, mtu akiwa na neno juu ya mwenzake. Kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.” (Wakolosai 3:12-13)
“Msameheane, na kwa maana hiyo msisahau jinsi Yesu Kristo alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi msameheane.” (Waefeso 4:32)

Uzuri wa Kusamehewa

Neno “Nimekusamehe” ni zuri kusikia masikioni kuliko neno “Ninakupenda”. Maana yake ni kwamba, msamaha unaleta uzima wa moyo na uhuru wa ndani. Kila mtu anahitaji kusamehewa, na wakati mwingine msamaha una nguvu zaidi ya upendo wenyewe. Kwa maana kusamehewa ni zaidi ya kupendwa kwani msamaha ni matokeo ya upendo. Ni kupitia msamaha tunapata nafasi ya kuanza upya na kujenga mahusiano mapya yaliyojaa matumaini.

“Kwa maana nitatubia uovu wao, na dhambi yao sitaikumbuka tena.” (Yeremia 31:34)
“Naye asema, ‘Dhambi zao na uovu wao sitaukumbuka tena.'” (Waebrania 8:12) “Nanyi msifanye mambo ambayo mimi nimewaambia msifanye, bali ninyi pia msisahau kwamba, ikiwa ninyi mna uovu na msamaha, mimi pia ninasamehe na kuponya.”_ (Zaburi 103:3)

Msamaha: Daraja ya Upendo wa Kweli

Msamaha ni daraja inayoelekea kwenye upendo wa kweli. Bila msamaha, upendo hawezi kuwa kamili. Wakati tunapowapenda wengine, tunahitaji pia kujifunza kusamehe. Upendo usio na msamaha ni kama mti usio na mizizi, hauwezi kustawi na kuzaa matunda mazuri. Msamaha hufungua milango ya mawasiliano na kurejesha amani kati ya watu. Ni ishara ya kukubali udhaifu wa kibinadamu na kutambua kuwa sisi sote tunahitaji neema na rehema ya Mungu.

“Upendo hufunika wingi wa dhambi.” (1 Petro 4:8)
“Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.” (1 Wakorintho 13:7)
“Kwa maana nimekasirika kiasi gani, kwamba nilipotaka huruma, ndipo nilipokasirika; lakini nikaachilia mbali upendo wangu, na hivyo nimesamehe.” (Mika 7:18)

Ukomavu Katika Imani na Msamaha

Kusamehe ni ishara ya ukomavu katika imani. Ni kuonyesha kwamba tumeelewa maana ya kweli ya upendo wa Kristo. Yesu alitufundisha umuhimu wa kusamehe kupitia maisha yake na kifo chake msalabani. Alisema, “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui walitendalo.” (Luka 23:34). Huu ni mfano wa hali ya juu kabisa ya msamaha na upendo. Tunapomwiga Kristo kwa kusamehe wengine, tunaonyesha kwamba tumezama katika upendo wake na tumeamua kufuata njia yake.

“Wakati Petro alipomwambia Yesu, ‘Bwana, nikisamehe ndugu yangu mara ngapi? Hata mara saba?’ Yesu akamjibu, ‘Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.'” (Mathayo 18:21-22) “Nanyi mtasameheani bure kama Bwana alivyosameheani ninyi, pia nanyi msameheani kwa bure.”_ (Wakolosai 3:13)
“Tafuteni amani na kila mtu, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao.” (Waebrania 12:14)

Kusamehe ni zawadi ya kipekee ambayo tunaweza kupeana sisi kwa sisi. Inahitaji unyenyekevu, uvumilivu, na upendo wa kweli. Tukumbuke kila siku kuwa na moyo wa kusamehe na kujenga mahusiano yenye msingi wa upendo na msamaha. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuishi maisha yenye amani na furaha, tukifuata nyayo za Kristo ambaye alitufundisha maana ya kweli ya msamaha na upendo.

Shopping Cart