Yesu, Mungu wangu mpenzi,/ upo hapa katika Altare mbele yangu;/ na mimi napiga magoti mbele yako.// Waniangalia sana,/ siyo kwa kunipeleleza,/ lakini kwa sababu wapenda kuniona hivi karibu na wewe,/ wafurahiwa nikija kukuabudu./ Wayasikiliza maneno yangu yote/ yenye kutoka mdomoni mwangu,/ na zaidi wapokea maneno yangu yanayotoka moyoni./ Nataka kuzungumza na wewe peke yako,/ na kusahau mambo mengine yote/ na watu wengine walioko kanisani pamoja nami./
Yesu wangu,/ nakushukuru/ kwa sababu umekubali kutupa Sakramenti hii kuu kabisa,/ ukitaka kukaa pamoja na sisi,/ na hata ukakubali kuwa chakula chetu/ chenye nguvu ya ajabu./ Mfalme wangu Yesu,/ Sultani wangu Mkuu,/ naamini kabisa kwamba upo katika Altare/ na kwamba umejificha chini ya umbo la mkate./ Ulipokuwapo bado hapa duniani mbele za watu,/ ulikuwa hujifichi kama sasa;/ lakini hata siku zile/ watu hawakuweza kukuona vile ulivyo./ Hawakuweza kuutambua Umungu wako,/ ikalazimu kukuamini tu sawa kama sisi./ Wakainama kichwa wakisema,/ โBwana wangu na Mungu wanguโ./ Na mimi kadhalika naungama/ U Bwana wangu na Mungu wangu/ na Mkombozi wangu/ na salama yangu yote./ U Yesu wangu tu,/ siwezi kusema zaidi./ Nakuabudu ee Yesu./ Najua sana, mimi ni mdogo kabisa,/ sina maana hata kidogo./ Mimi ni dhaifu na maskini mno./ Lakini Wewe katika hruuma yako kubwa/ waniita nije kwako./ Wewe huuangalii umaskini wangu,/ bali wanivuta katika mapendo yako./
Nasikia maneno yako usemayo:/ โNjooni kwangu ninyi nyote mnaoelemewa na mizigo/ nami nitawasaidiaโ./ Kwa ajili ya maneno hayo/ nakuja kwako bila hofu./ Najua kwamba wanipenda,/ najua wataka kunisaidia na kuniponya,/ najua kuwa wataka kunitakasa./
Nahitaji sana msaada wako, hakika./ Unaniona katika mwendo wangu wa kila siku,/ Jinsi ninavyohangaika na vishawishi mara nyingi;/ jinsi nilivyo na lazima ya kushindana kila siku/ nikitaka kukaa mwema na safi katika utumishi wako./ Naungama mbele yako Wewe Mkombozi wangu,/ kwamba sikukaa imara siku zote vile nilivyopaswa./ Naungama kwamba nimeshindwa mara nyingine/ na kwa hivi naomba toba./ Lakini kwa nini nimeshindwa mara nyingine?/ Kwa nini nikakosa?/ Ni kwa sababu nalikuwa nimekwenda mbali nawe;/ nalianza kujitegemea mwenyewe./ Katika majivuno yangu nikajisifu mwenyewe,/ nikajiona mwema,/ nikasahau udhaifu wangu./ Na kwa ajili hiyo nikajitia katika hatari bure,/ sikujilinda tena,/ nikampa shetani nafasi ya kunishambulia kwa hila zake zote./ Unihurumie ee Yesu wangu./
Sasa nafahamu jinsi nilivyokuwa mjinga kwelikweli./ Ndiyo maana nakuabudu kwa moyo wangu wote./ Najiweka mikononi mwako/ ufanye nami vile unavyotaka./ Wewe utanitunza;/ Wewe utanilinda vema;/ Wewe utaniongoza nijue namna ya kuepa hatari zote,/ na jinsi ya kufukuza kila kishawishi./ Chukua moyo wangu kabisa,/ kwa sababu ni mali yako kamili;/ Wewe ndiwe uliyeniumba,/ ndiwe uliyenipeleka katika Ukristo,/ nawe ndiwe utakayenihukumu siku ya mbele./ Ndivyo ninavyojitolea kwako./ Ndivyo ninavyokuabudu,/ wala sijui njia nyingine ya kukusifu zaidi./
Yesu wangu mpenzi,/ naomba upokee kwa uzuri heshima hiyo yangu./ Angalia: naitolea pamoja na heshima yote/ unayopewa daima na watakatifu wako/ na malaika wako./ Nikipiga magoti hapa mbele yako sasa,/ siko peke yangu,/ nakuabudu pamoja na Mama yako Bikira Maria,/ ambaye sala zake zinakupendeza kabisa./ Sala zangu naweka pamoja na sala zake yeye,/ uzipokee zote pamoja,/ zikupendeze zote sawa./ Ee Mama Maria!/ Nifundishe maneno ya kumsifu Mwanao Yesu vizuri./ Nipeleke kwa Yesu tumwabudu pamoja./ Nifunike na utakatifu wako/ kusudi Yesu asiangalie tena umaskini wangu/ na makosa yangu,/ aniponye katika huruma yake./
Sasa najisikia vizuri, Yesu wangu./ Sasa nina moyo wa kuweza kuendelea vema/ katika njia njema./ Sasa ninatumaini kwamba/ nitakaa mkristo mwema,/ nitakuwa mtumishi wako mwaminifu./ Nasikia amani kubwa sana moyoni mwangu,/ kwa kuwa nimo mikononi mwako./ Baada ya dakika chache/ nitaondoka tena kanisani,/ nitarudi nyumbani kwangu,/ lakini hatutaachana,/ hapana./ Mapendo yetu yatatuunganisha pamoja daima./ Wewe utanikumbuka nikiwa kazini,/ nikilala usingizi,/ nikienda njiani,/ kila mahali nilipo,/ Wewe utaniona,/ utafuatana na mimi./ Kadhalika nitakukumbuka tu./ Nitafanya bidii nisikuache kabisa./ Amina.
Raphael Okoth (Guest) on August 1, 2017
๐โค๏ธ๐ Baraka za Mungu ziwe nawe
Elizabeth Mrope (Guest) on June 18, 2017
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Andrew Mahiga (Guest) on April 24, 2017
๐๐ Mungu akujalie amani
Charles Mboje (Guest) on April 18, 2017
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Esther Nyambura (Guest) on April 2, 2017
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Kevin Maina (Guest) on April 1, 2017
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Victor Sokoine (Guest) on February 27, 2017
Neema ya Mungu inatosha kwako
Andrew Mchome (Guest) on February 24, 2017
Mungu akubariki!
Grace Mligo (Guest) on November 19, 2016
Sifa kwa Bwana!
Grace Mushi (Guest) on November 3, 2016
๐โค๏ธ๐ Tumshukuru Mungu kwa yote
Betty Kimaro (Guest) on August 8, 2016
Mwamini Bwana; anajua njia
Mercy Atieno (Guest) on July 16, 2016
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Benjamin Masanja (Guest) on June 16, 2016
๐๐๐ซ Mungu ni mwema
Edward Chepkoech (Guest) on June 16, 2016
Mungu ni mwema, wakati wote!
Francis Mtangi (Guest) on June 7, 2016
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
George Ndungu (Guest) on April 17, 2016
๐โจ Neema ya Mungu iwe nawe
John Kamande (Guest) on March 23, 2016
Neema na amani iwe nawe.
Robert Ndunguru (Guest) on November 15, 2015
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Bernard Oduor (Guest) on November 15, 2015
๐โค๏ธโจ Asante Mungu kwa kila kitu
Betty Akinyi (Guest) on October 31, 2015
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Catherine Mkumbo (Guest) on October 11, 2015
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Violet Mumo (Guest) on June 22, 2015
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Lucy Kimotho (Guest) on June 3, 2015
Kwa Mungu, yote yanawezekana