Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Sabau za ubakaji

Ni vigumu kuelewa nini kinamfanya mtu aweze kubaka mwingine.
Ubakaji ni aina nyingine ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia
ambao utaleta madhara mengi kwa muhusika kwa hiyo hakuna
msamaha kwa ubakaji.
Ubakaji mara zote ni kosa la mbakaji. Hakuna maelezo
mazuri ya kuwaelezea watu ambao ni, au wanajihusisha na
ubakaji. Ubakaji unatendeka kwa sababu mbalimbali. Baadhi
ya wabakaji ni wagonjwa wa akili, wanaume wengine wanabaka
kwa sababu wanafikiri wanawake wako pale ili kuwaridhisha
wao katika masuala ya kujamiiana, na kumwadhibu msichana au
wameshawishiwa na wengine.
Hii ni kosa maana hauheshimu haki ya binadamu na thamani ya
muhusika. Dawa za kulevya na pombe yanaweza vinashawishi
tabia ya ubakaji maana vinawafanya watu kushindwa kujizuia
kuhusu tabia zao.

Ubakaji ni nini?

Ubakaji ni tendo la kutumia nguvu katika ngono ambapo mbakaji anatumia nguvu kuonyesha ubabe wake. Ubakaji ni kosa la jinai i na huadhibiwa kisheria.
Kama mtu hayuko tayari kufanya ngono na analazimishwa kukubali kufanya hivyo hii , i inahesabiwa kama ubakaji, hata kama anayekulazimisha ni rafiki, ndugu, jirani, mume au mtu usiyefahamiana naye.

Utumiaji nguvu katika mahusiano ya ujinsia kama sehemu ya utamaduni

Utumiaji wa nguvu
katika mahusiano ya
ujinsia unavunja haki
za uzazi na haki za
binadamu. Uhusiano
wa ujinsia ni muhimu
uwe katika misingi ya
maelewano, kuheshimiana,
na Huwezi kunikataa
mapenzi kwa
kila mmoja wenu.

Katika baadhi ya
tamaduni , mwanamume
ndiye mwenye mamlaka
na anakubalika kwamba anaweza kutumia nguvu. Ingawaje utamaduni
unatakiwa kujenga na kutia moyo uhusiano mzuri katika jamii.
Utamaduni wetu hauna budi kuimarisha thamani ambayo
itaheshimu hadhi ya utu na usiruhusu utumiaji wa nguvu. Kila
jambo ambalo linavunja haki ya mtu na kumdhalilisha hadhi ya
utu haliwezi kukubalika na kupokelewa.

Iwapo mtu mzima amejamiiana na mtoto na wote wawili wamekubaliana

Ni kweli hiyo ni dhuluma na inaitwa unyanyasaji wa kijinsia kwa
mtoto. Watoto wanaweza kushawishiwa kwa kutumia hila kwa
mtu mzima anayejaribu kuwavuta ili waweze kujamiiana naye. Na
zaidi wanaweza wasielewe matatizo au madhara watakayopata
kutokana na kujamiiana kwa afya zao pia wanaweza wasiweze
kufanya maamuzi sahihi kwa vile hawana habari.
Mtoto hana uwezo wa kuchunguza mambo katika akili yake
kabla ya kujamiiana.
Uhusiano unaweza pia usiwe sawa kwa vile yule mtu mzima ana
uwezo na nguvu juu ya yule mtoto. Kwa hiyo itakuwa vigumu
kwa mtoto kujadiliana juu ya matumizi ya kondomu .Hizi ndiyo
sababu kwa nini watoto wanahitaji ulinzi maalum. Ni kosa
kujamiiana na msichana wa umri chini ya miaka 18.
Iwapo mtu anajamiiana na msichana chini ya miaka 18 mtu
huyo anawajibika kisheria, katenda kosa hata kama msichana
amempa ridhaa yake.

Utoaji wa zawadi kwa kubadilishana na kujamiiana

Kutoa zawadi kwa mtu kwa kubadilishana ili kujamiiana
ni unyanyasaji mbaya. Iwapo mpokeaji wa zawadi hajakubali
kujamiiana na unamlazimisha, mwanamume au mwanamke
kujamiiana hapo hiyo ni unyanyasaji na unamwonea kwa sababu
jambo hilo la kujamiiana lilikuwa halikubaliki kwa mtu yule.
Hapa Tanzania kosa la namna hii hujulikana kama unyanyasaji/
unyonyaji wa ujinsia10 ambapo mtu hufikiria kutumia fedha,
mali au msaada kwa mtoto au wazazi kwa kusudi la kumpata ili
ajamiiane naye.

Uwe mwangalifu unapopewa zawadi, alama za juu shuleni, au
kuajiriwa kwa ajili ya kubadilishana na ngono. Kila mara uliza na
jaribu kuelewa kwa nini zawadi inatolewa kwako.
Usikubali zawadi yoyote au pesa, kama unafikiri kuwa huyo mtu
anayekupa hongo kama zawadi, anakutegemea wewe kujamiiana
naye kwa kubadilishana na hiyo zawadi aliyokupa. Ni jambo
la majaribu kukubali
zawadi au pesa, hasa pale
unapohitaji, lakini fikiri
hatari itakayokupata kwa
kujamiiana kama vile mimba
usiyoitarajia, magonjwa
yaenezwayo kwa njia ya
kujamiiana hata Virusi na
Ukimwi.

Shopping Cart