Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Jinsi ya kujikinga na ubakaji

Hata kama utafanya kila kitu usibakwe bado inaweza ikatokea.
Ubakaji na unyanyasaji wa ujinsia unaweza kutokea kwa kila mtu.
Hata hivyo kuna baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kupunguza
hatari ya kubakwa.
Jizuie usiwe peke yako kwenye giza, kutembea peke yako
katika misitu au sehemu ambazo zina watu wachache, kuchota
maji sehemu ya mbali. Hakikisha kuwa kuna watu karibuni wa
kukusaidia iwapo kuna hatari. Pia jihadhari na watu walevi na
sehemu ya kunywea pombe maana watu walevi wanaweza wakawa
hatari. Iwapo umelazimika kufanya kazi katika mazingira
ya hatari, jaribu kujadili tatizo hili na wazazi wako au mtu
unayemwamini na muulize huyu mwanamume au mwanamke
azungumze na wazazi wako.
Usikubali zawadi au upendeleo, kama unafikiri unapewa wewe
kwa kubadilishana na ngono. Kama unajisikia unatishwa jaribu
kukimbia na piga kelele kwa kutafuta msaada mara moja.
Utafiti umeonyesha kuwa wasichana au wanawake ambao kwa
ushupavu wanasema hapana na ambao wanathubutu kupiga
kelele na kuvutia hisia za wengine wakati wanaposhambuliwa
wana hatari kidogo ya kubakwa. Unapokuwa unajitetea kwa
uhakika unapoanza unachopenda na usichopenda, ni sehemu
muhimu ya kujilinda.

Mwanamume au mvulana anaweza kubakwa?

Ndiyo, mtu yoyote anayelazimishwa
kujamiina atakuwa
amebakwa, haijalishi kama
mtu huyu ni mwanamke/
msichana, mwanaume au
mvulana.

Wavulana na wanaume
wanaweza kubakwa na
wanaume wenzao au wanaweza
kulazimishwa na mwanamke
kujihusisha na tendo la
kujamiiana. Wanaume wanaweza
kulazimisha wavulana
kujamiiana kwa njia ya mdomo
au njia ya haja kubwa. Kisheria hapa Tanzania tukio kama
hili linajulikana kama kulawiti.
Matatizo/matokeo ya kulawiti kwa wavulana ni sawa na yale
yanayopatikana kwa wasichana. Wavulana wanaweza kuumizwa
vibaya zaidi wakati wa kujamiiana na pia kuchanganyikiwa,
kiwewe, na kwa wavulana wanapata madhara zaidi.
Sheria hapa Tanzania12 haziko wazi juu ya ubakaji kwa wavulana
hata hivyo wanatambua mahusiano ya ushoga/ubasha kuwa ni
kosa la jinai.

Madhara yanayotokea kwa unyanyasaji wa jinsia kwa mtu

Unyanyasaji wa ujinsia una matatizo mabaya ya kimwili na
yanayochukua muda mrefu kwa mwathiriwa kupona. Unyanyasaji
wa jinsia mara nyingi humuumiza mwathiriwa, matendo ya
ubakaji, majaribio ya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia kwa mtoto,
na ukeketaji kwa wanawake yanamhusu moja kwa moja mwili
wa mwathiriwa. Mwathiriwa anaweza kupata maumivu makali
wakati wa kitendo, viungo vyake vya uzazi akiwa mwanamume
au mwanamke kuna uwezekano ukapata majeraha wakati wa
ubakaji. Zaidi ya hayo mbakaji anaweza kumuumiza mwathiriwa
katika sehemu nyingie za mwili. Na jambo baya zaidi ukatili
wa kijinsia wakati mwingine unaweza kusababisha ulemavu wa
maisha na mara nyingine hata kifo cha mwathiriwa. Ubakaji
unaweza kusababisha mimba, na uenezaji wa magonjwa hatari
kama Virusi vya Ukimwi.
Watoto wanadhuriwa zaidi na vitendo vya ukatili wa ujinsia
katika miili yao kwa sababu ukubwa wa viungo vyao vya sehemu
za siri ni vidogo kuliko vile vya watu wazima.
Athari za kisaikolojia kwa mwathiriwa pia ni hatari sana. Uonevu
wa ujinsia kwa mwathirika unaweza kusababisha kuchanganyikiwa
na kupata kiwewe na hali ya hatari sana inayoweza kusababisha
mtu akapata kichaa katika miezi ya kwanza. Baada ya uonevu
wa ujinsia na hata baada ya miaka, mwathiriwa bado atakuwa
na kumbukumbu ya maumivu aliyopata na hivyo kukumbuka
katika akili yake. Waathiriwa wengi wa ubakaji wana matatizo
ya kutokuwa na uhusiano mzuri wa kujamiiana, kwani kila mara
atahusisha kujamiiana na alipobakwa. Ndiyo maana waathiriwa
wa ubakaji wanahitaji msaada, uelewa na uvumilivu toka kwa
wazazi wao, wenzi wao na marafiki.

Uhusiano wa ubakaji na uvaaji wa nguo fupi?

Ubakaji kamwe siyo kosa linalomhusu yeye aliyebakwa; ni kosa
linalomuhusu yeye aliyebaka. Unachovaa hakimpi mtu yoyote
haki ya kukubaka wewe. Wengi wanaobakwa huwa mara nyingi
hawakuvaa nguo fupi wakati wanabakwa. Ni maamuzi yako nini
uvae, ingawaje kama nguo unazovaa zinasababisha wengine
kupata mheko kutokana na mavazi yako, ni muhimu ufahamu
kuwa unaweza ukasababisha matatizo juu yako mwenyewe.
Uvaaji wa nguo ambazo jamii
inayokuzunguka hawaziruhusu
inaweza ikasababisha watu
wakakufedhehesha au kukutishia
ubakaji kila mara. Ubakaji ni
mbaya kwa sababu unasababisha
kuvunja haki za bindamu na
kumwacha mwathiriwa na
maumivu kimwili na kisaikolojia.
Katika hali yoyote mtu hana haki
ya kumbaka mwingine.

Shopping Cart