Kutoa zawadi kwa mtu kwa kubadilishana ili kujamiiana
ni unyanyasaji mbaya. Iwapo mpokeaji wa zawadi hajakubali
kujamiiana na unamlazimisha, mwanamume au mwanamke
kujamiiana hapo hiyo ni unyanyasaji na unamwonea kwa sababu
jambo hilo la kujamiiana lilikuwa halikubaliki kwa mtu yule.
Hapa Tanzania kosa la namna hii hujulikana kama unyanyasaji/
unyonyaji wa ujinsia10 ambapo mtu hufikiria kutumia fedha,
mali au msaada kwa mtoto au wazazi kwa kusudi la kumpata ili
ajamiiane naye.
Uwe mwangalifu unapopewa zawadi, alama za juu shuleni, au
kuajiriwa kwa ajili ya kubadilishana na ngono. Kila mara uliza na
jaribu kuelewa kwa nini zawadi inatolewa kwako.
Usikubali zawadi yoyote au pesa, kama unafikiri kuwa huyo mtu
anayekupa hongo kama zawadi, anakutegemea wewe kujamiiana
naye kwa kubadilishana na hiyo zawadi aliyokupa. Ni jambo
la majaribu kukubali
zawadi au pesa, hasa pale
unapohitaji, lakini fikiri
hatari itakayokupata kwa
kujamiiana kama vile mimba
usiyoitarajia, magonjwa
yaenezwayo kwa njia ya
kujamiiana hata Virusi na
Ukimwi.
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Recent Comments