Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Unyanyasaji wa kijinsia

Kuna aina nyingi za unyanyasaji wa jinsia na unaweza kutokea
kwa wote wanaume na wanawake. Kwa kawaida unajulikana
kama matumizi ya makusudi ya kutumia nguvu na uwezo na
kutishia au kwa hali halisi kinyume cha mtu au kikundi au
jamii ambapo matokeo yake yanaweza kuleta jeraha au kifo,
kuumia kisaikilojia, kutokukua au kudumaa.7 Chini ya sheria za
Tanzania8 unyanyasaji wa kijinsia ni pamoja na maneno, sauti
ishara au maonyesho ya sehemu za mwili kwa makusudi kinyume
na matakwa ya mtu.
Hakuna mtu anayeruhusiwa kujamiiana nawe bila ya ridhaa yako,
maana hii itakuwa ni ubakaji. Kumlazimisha mtu kujamiiana nawe kwa
kubadilishana na zawadi au kumpa kazi ni unyanyasaji wa kijinsia.
Kadhalika hakuna mtu anayeruhusiwa kushika viungo vya siri vya
uzazi, au kukupiga busu bila ya ridhaa yako. Tendo la ukeketaji ni
aina nyingine ya ukatili wa kijinsia.
Aina nyingine za unyanyasaji wa kijinsia ni pamoja na kumwita
mtu majina, kumlazimisha mtu kuvua nguo mbele za watu au
kumlazimisha mtu kujamiiana na mtu mwingine. Fikiria kwamba
unyanyasaji wa kijinsia ni tendo baya kwa haki za binadamu
na unasababisha maumivu kwa wahusika. Tukumbuke kwamba
uhusiano wa kimapenzi na watu waliokaribu nasi kwa mfano baba,
mama, kaka, dada, babu au bibi ni aina nyingine ya unyanyasaji
wa jinsia. Inajulikana kama kujamiiana kwa maharimu β€œincestβ€œ
na inakatazwa kisheria.

Sheria kuhusu kufanya punyeto

Punyeto ni kupapasa au kusugua kiungo cha uzazi ili uweze kupata
starehe. Hakuna kosa kwa tendo hilo, kwa sababu hakuna tatizo
lolote kwa mvulana au msichana. Kwa kawaida watu hufanya hivyo
kwa siri, baadhi ya mila na desturi wanapinga kufanyika kwa
tendo hili hata hivyo hakuna sheria yoyote kuhusu punyeto.

Sheria kuhusu utoaji mimba

Sheria kuhusu utoaji
mimba zinatofautiana
kati ya nchi na nchi. Hapa
Tanzania utoaji mimba
ni kosa la jinai.5 Kosa la
jinai linamchukulia mtu
hatua aliyetoa mimba na
yule aliyemtoa au
kumsaidia kutoa mimba.
Hata hivyo hapa Tanzania
unaruhusiwa kutoa mimba
pale tu inapokwepo sababu
za kuokoa maisha ya mama
mjamzito kama kuna
matatizo ya kiafya au
pale mimba inatokana na
kubakwa.6 Utoaji mimba hufanyika kwa siri.
Ni hatari iwapo utoaji mimba utafanyika bila ya utaalamu. Yule
anayesaidia kutoa mimba anawajibishwa kisheria. Iwapo utoaji
mimba umefanywa na mtu asiye na ujuzi, kwa mama mwenyewe,
au kifaa kilichotumika ni kichafu, au majani au dawa zimewekwa
ukeni, zinaweza kuhatarisha maisha ya mama.
Ni muhimu hata hivyo kujua kuwa wahudumu wengine hutoa
huduma baada ya mimba kuharibika kwa wale wanaohitaji
msichana au mama, kutokana na matatizo ya utoaji mimba au
kuharibika kwa mimba

Mtoa huduma wa afya anaweza kukataa kutibu?

Siyo haki kwa mtoa huduma wa afya kukataa kumtibu.
Kama kijana, una haki sawa ya kutibiwa kama vile mtu yoyote.
Iwapo mtoa huduma anakataa kukutibu wewe, jaribu kuzungumza
naye kuhusu jambo hilo na umuulize sababu za kukataa kukutibu.
Iwapo yeye anashikilia uamuzi wa kutokutibu basi amua ama
unatafuta mhudumu mwingine au zungumza na mkubwa wake
kuhusu tatizo lako. Ni jambo la maana kuzungumza na rafiki
yako au mwone mtu unayemwamini akusaidie kutatua tatizo
lako.

Vituo vingi vya Umma na vya binafsi vya huduma za afya
vinajitahidi kutoa huduma rafiki kwa vijana. Tafuta kituo cha
karibu au shirika linalotoa huduma za afya ya uzazi. Kumbuka,
haki ya afya ambayo pia inabeba haki ya huduma ya afya ya
uzazi, Kimataifa inatambuliwa kupitia ICESCR4 na pia imetiwa
saini na kuridhiwa hapa Tanzania. Hivyo usisite kuulizia huduma
kama hii.

Ni katika umri gani vijana wana haki ya kutumia huduma za afya ya uzazi na njia za uzazi wa mpango?

Hakuna kiwango cha umri kwa kutumia huduma za afya ya uzazi
na njia za uzazi wa mpango. Unatakiwa kuanza kutumia huduma
za afya ya uzazi pale unapoona unazihitaji. Na hasa iwapo
umeamua kujamiiana, unatakiwa uende kwanza kwenye huduma
za afya ya uzazi, na kupata ushauri juu ya ujinsia na masuala
ya afya ya uzazi pamoja na njia mbalimbali za uzazi wa mpango.
Vijana kisheria wamepewa haki ya kutumia njia za uzazi wa
mpango.
Nchini Tanzania kuna sera ya idadi ya watu ya mwaka 1992.2
ambapo kati ya mambo mengine inalenga katika kuandaa
vijana, kabla ya kuingia katika maisha ya ndoa wawe wazazi
wanaowajibika kwa kuinua kiwango cha elimu ya familia.
Sera hii inazungumzia uanzishwaji wa huduma za afya ya uzazi
ambayo itakidhi mahitaji ya vijana na inawahakikishia vijana
kupata huduma za afya ya uzazi kwa urahisi bila pingamizi
katika umri wowote.
Baadhi ya watu wanafikiri kuwa huduma za uzazi wa mpango ni
kwa watu walio kwenye ndoa. Hii si kweli, mtu yoyote anaruhusiwa
kutumia huduma za uzazi wa mpango na kupata njia mbalimbali
za uzazi wa mpango. Vijana3 wanafaidika na kuwa na haki sawa
kama watu wazima walio kwenye ndoa. Huduma za kinga kama
vile ushauri juu ya mafunzo ya afya ya uzazi na vilevile kondomu
ni njia za kuzuia mimba zinapatikana bure katika vituo vya afya
vya serikali hapa Tanzania.

Shopping Cart