Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Ushauri kwa mtu aliyebakwa

Jambo la kwanza jaribu kumwondoa hofu mwathiriwa na
muliwaze maana amepata jambo la kutisha. Na iwapo mtu
amejeruhiwa sana mpeleke katika kituo cha huduma za afya
kilicho karibu mara moja. Vinginevyo ongozana na rafiki
yako kwenda kituo cha Polisi na kutoa taarifa kuhusu jambo
lililotokea. Polisi watampa fomu ambayo ataipeleka kwa mtoa
huduma. Ni muhimu usijioshe kwa maji kabla hujachunguzwa na
mtaalamu wa afya kwani kufanya hivyo kutaondoa ushahidi wa
kubakwa.
Kwa kuwa kupitia utaratibu huu
inakuwa vigumu mwathiriwa
anahitaji msaada wa karibu
na uangalizi. Mzazi au rafiki
anahitajiwa aongozane naye
na kumsaidia, kwa mfano
kuhakikisha kuwa katika kituo
cha polisi msichana ahojiwe na
polisi wa kike.
Mtu aliyebakwa anahitaji
kusaidiwa kihisia ili aweze
kusahau mawazo na jambo
liliomtokea. Kwa mwathirika, ni
muhimu apewe ushauri nasaha
ili aendelee kujihisi kwamba yeye bado yupo kama mtu wa
kawaida. Ni muhimu pia kuzishughulikia habari za mwathiriwa
kwa siri. Usimweleze kila mtu kilichotokea. Waeleze wale tu
ambao unafikiri wanaweza kusaidia kama daktari, mwalimu au
mzazi. Usiulize maswali ya kwa nini maana inaweza ikaonekana
ni kosa la mwathiriwa. Badala yake zungumza na huyo mtu kwa
utaratibu, polepole, peke yake na mpe uangalifu wa kutosha.
Hakikisha kwamba hutoi lawama yoyote kwa mwathiriwa.
Kubakwa kamwe siyo kosa la mwathiriwa.

Ukeketaji ni nini?

Katika baadhi za jamii viungo vya uzazi vya nje vya msichana,
yaani kisimi au sehemu ya ndani na nje ya mashavu ya uke
yanakatwa na kuondolewa kabisa. Huu ndiyo ukeketaji au
kutahiriwa kwa mwanamke.
Wakati mwingine uekeketaji hufanyika katika umri wa miezi ya
mwanzo ya maisha ya mtoto wa kike. Mara kwa mara kutahiriwa
kwa wanawake hufanyika wakati msichana anapofikia utu uzima
au kuadhimisha na kuvuka kutoka utoto kuingia utu uzima.
Mara nyingine ukeketaji ni sehemu ya unyago na kuadhimia kwa
msichana kujifunza jinsi ya kuwa mtu mzima.
Kuna aina mbalimbali za ukeketaji:
1 Sehemu ya ngozi inayofunika kisimi huwa inaondolewa.
Mara nyingine kisimi au eneo lake hukatwa pia. Watu
wengi huita aina hii sunna.
2 Kisimi pamoja na sehemu za mashavu ya ndani
hutolewa.
3 Sehemu yote au baadhi ya viungo vya nje hutolewa na
uke hufungwa kwa kushona. Hii huacha sehemu ndogo
ya tundu ambapo mkojo na damu ya mwezi (hedhi)
hupita. Aina hii huitwa mfyato (Infibulation).
4 Aina yeyote ya kuchezea kwa lengo la kuharibu
sehemu yoyote ya viungo vya nje kama vile kutia vitu
vyenye madhara kwenye uke, kurefusha mashavu au
kisimi kwa kuvivuta au kutoboatoboa.

Watu wafanye nini iwapo wamelazimishwa kufunga ndoa na mtu wasiyemtaka?

Iwapo mtu amelazimishwa
kuingia katika hali ya ndoa
(kuoa/kuolewa) na msichana/
mvulana ambaye hampendi,
hatua ya kwanza ni kukataa
ndoa hiyo na kuonyesha wazi
wazi. Jadiliana suala hili na
wazazi wako. Waeleze kwa
heshima kwa nini hukubaliani
na ndoa hiyo.

Kwa kawaida wazazi wanape-nda mambo mema kwa watoto wao.
Kwa hiyo kuwepo na uhusiano mzuri kati ya wazazi na watoto
kunaweza kukapangilia mambo yakaenda vizuri.
Iwapo jaribio la kuzungumza na wazazi wako halikufaulu,
unaweza ukazungumza na mtu mwingine unayemwamini ambaye
atakubali kuzungumza na wazazi wako. Kumbuka kwamba iwapo
bado unalazimishwa kufunga ndoa, unaweza kutoa taarifa polisi
kwa kuwa sheria ya Tanzania hairuhusu kulazimisha ndoa.

Sheria zinazohusiana na ndoa za kulazimishwa

Sheria ya msingi ya ndoa nchini Tanzania ni Sheria ya ndoa ya
Bunge, iliyopitishwa mwaka 1971. Sheria hii inakataza ndoa za
kulazimisha. Inatambua ndoa kama ni muungano kati ya mume
na mke ambao kwa hiari yao wameamua kuishi kama mume na
mke. Sheria hiyo inasema kwamba iwapo ndoa haikuwa ya hiari,
basi hiyo siyo ndoa. Sheria pia imefafanua utoaji wa adhabu
kwa watu wote wanaoshawishi au wanaolazimisha pande hizo
mbili kuingia katika ndoa bila hiari yao. Kwa hiyo mwathiriwa wa
ndoa ya kulazimishwa anatakiwa kutoa taarifa juu ya wale wote
waliomlazimisha katika ndoa kwa polisi ambaye atawashitaki
kwa kuwa hili ni kosa la jinai.

Haki zinazokiukwa iwapo mvulana au msichana wamelazimishwa kuoa au kuolewa

Nani na lini unaoa ni maamuzi yako binafsi wewe mwenyewe,
hata kama rafiki na wazazi wanakushauri juu ya jambo hilo.
Kumlazimisha mtoto kuoa au kuolewa ni kumchukulia mtu uhuru
wa anavyopenda kuishi. Haki ya kuchagua kuoa, ama kuolewa
au kuanzisha familia yako huwa imegeukwa. Haki hii ni sehemu
ya makubaliano ya kimataifa na sehemu ya programu na hatua
ya Umoja wa Mataifa tangu mkutano wa Cairo 1994. Sheria
ya ndoa, Tanzania13 inasisitiza kwamba hakuna ndoa halali,
isipokuwa ipate ridhaa na iwe ya uhuru na hiari kutoka pande
zote za wanaokusudia kuoana. Ndoa yoyote ambapo pande
zimehusika hazikubaliani ndoa hiyo si halali.

Wakati mtoto amelazimishwa kuingia katika maisha ya ndoa bado
hayupo tayari na ndoa hiyo itakuwa inavunja haki za msichana
kama haki ya elimu.14 Msichana ana haki kupata elimu, msichana
ana haki kupata elimu. Haki ya kuoa inakamilika kwa msichana
kuwa na umri sahihi, naye kuwafanya maamuzi/uchaguzi wake
mwenyewe, kuanzisha familia. Kwa hiyo inaingilia kuvunja haki
ya msingi ya mtoto ya kumtoa shule kabla ya kumaliza elimu ya
msingi, ambayo ni shuruti kwa watoto wote, hapa Tanzania.

Shopping Cart