Madhara yanayotokea kwa unyanyasaji wa jinsia kwa mtu

Unyanyasaji wa ujinsia una matatizo mabaya ya kimwili na
yanayochukua muda mrefu kwa mwathiriwa kupona. Unyanyasaji
wa jinsia mara nyingi humuumiza mwathiriwa, matendo ya
ubakaji, majaribio ya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia kwa mtoto,
na ukeketaji kwa wanawake yanamhusu moja kwa moja mwili
wa mwathiriwa. Mwathiriwa anaweza kupata maumivu makali
wakati wa kitendo, viungo vyake vya uzazi akiwa mwanamume
au mwanamke kuna uwezekano ukapata majeraha wakati wa
ubakaji. Zaidi ya hayo mbakaji anaweza kumuumiza mwathiriwa
katika sehemu nyingie za mwili. Na jambo baya zaidi ukatili
wa kijinsia wakati mwingine unaweza kusababisha ulemavu wa
maisha na mara nyingine hata kifo cha mwathiriwa. Ubakaji
unaweza kusababisha mimba, na uenezaji wa magonjwa hatari
kama Virusi vya Ukimwi.
Watoto wanadhuriwa zaidi na vitendo vya ukatili wa ujinsia
katika miili yao kwa sababu ukubwa wa viungo vyao vya sehemu
za siri ni vidogo kuliko vile vya watu wazima.
Athari za kisaikolojia kwa mwathiriwa pia ni hatari sana. Uonevu
wa ujinsia kwa mwathirika unaweza kusababisha kuchanganyikiwa
na kupata kiwewe na hali ya hatari sana inayoweza kusababisha
mtu akapata kichaa katika miezi ya kwanza. Baada ya uonevu
wa ujinsia na hata baada ya miaka, mwathiriwa bado atakuwa
na kumbukumbu ya maumivu aliyopata na hivyo kukumbuka
katika akili yake. Waathiriwa wengi wa ubakaji wana matatizo
ya kutokuwa na uhusiano mzuri wa kujamiiana, kwani kila mara
atahusisha kujamiiana na alipobakwa. Ndiyo maana waathiriwa
wa ubakaji wanahitaji msaada, uelewa na uvumilivu toka kwa
wazazi wao, wenzi wao na marafiki.

Enjoyed? Drop your Comment Below
OR Chat Live with AckySHINE here
Read and Write Comments
Shopping Cart