Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Kwa nini pombe za kienyeji ni hatari kuliko pombe za viwandani?

Pombe zinazotengenezwa kiwandani zinafuata viwango
ambavyo ubora wake umethibitishwa kihalali. Hii inamaanisha
kwamba wataalamu katika kiwanda, huzipima bidhaa hizo
mara kwa mara huangalia usafi wake, kiwango cha kilevi, na
mchanganyiko wa malighafi zinazotumika kutengenezea pombe
hiyo. Madhara ya pombe za kienyeji yanatokana na kutokuwepo
kwa utaratibu kama huo. Mara nyingi vitu kama vile mbolea za
chumvichumvi huongezwa ili kuichachusha haraka. Kwa bahati
mbaya, mara nyingi watu hupata madhara makubwa baada ya
kunywa pombe zilizotengenezwa kienyeji. Wengi hupata upofu
na hata wengine hufa.

Kwa nini hairuhususiwi kuotesha au kuvuta bangi, iwapo kupanda na kuvuta tumbaku kunaruhusiwa?

Sheria ya Tanzania inaeleza dawa zilizo halali na zisizo halali.
Tumbaku imekubalika na jamii kwa muda mrefu, na ni katika
miaka kama hamsini iliyopita ndipo madhara yatakanayo na
nikotini iliyomo kwenye tumbaku yalipoanza kukubalika. Hata
hivyo, hadi sasa tumbaku ni halali, lakini ni bangi kwa upande
mwingine si halali kisheria Tanzania.
Kwa hivyo, kutokana na kwamba nikotini kwenye sigara
ina madhara, basi serikali ilichukua hatua ya kuanza
kuwatahadhadharisha wavutaji na kuwazuia vijana kuvuta sigara.
Kuna sheria mpya Tanzania ambayo inawalazimisha
watengenezaji wa bidhaa za tumbaku kuandika tahadhari
ya afya kwenye bidhaa wanazotengeneza na kuuza. Kuanzia
mwaka 2000 bidhaa za tumbaku zote zililazimika kuwa na onyo
kwamba “Uvutuaji wa sigara ni hatari kwa afya yako.”

Je, Tanzania kuna wataalamu wanaosaidia watu wenye matatizo ya ulevi wa kupindukia?

Ndiyo. Hapa Tanzania kuna kitengo maalumu kinachojishughulisha
na masuala ya akili. Wataalamu mbalimbali hufanya kazi pamoja
kama vile matibabu ya magonjwa ya akili na wanasaikolojia.
Wanaustawi wa jamii ambao wana mbinu za kuelewa kiwango
cha unywaji pombe katika jamii kulingana na tamaduni
mbalimbali ambao pia wana utaalamu wa masuala ya utoaji
ushauri, wanaweza kushirikiana na wataalamu wa afya ambao
hufanya kazi hospitalini na kwenye jamii.

Je, pombe ni moja ya sababu za kuenea kwa Virusi vya UKIMWI na VVU au magonjwa mengine yatokanayo na kujamiiana?

Matumizi mabaya ya pombe ndiyo yanayosababisha kuenea kwa
VVU au magonjwa mengine yatokanayo na kujamiiana. Tabia
ya ulevi ya kupindukia huwaweka watu katika hatari kubwa ya
kupata na kueneza magonjwa haya.
Pombe husababisha watu kusahau hatari ya kuwa na wapenzi
wengi na pia kufanya mapenzi na watu ambao hawafahamu hali
za afya zao. Husahau kujilinda wao wenyewe na wapenzi wao, kwa
kutumia kondomu na kusahau majukumu yao ya familia.

Watu wanaokunywa pombe kupita kiasi hudhoofisha mfumo wa
kinga mwilini, hivyo basi, virusi huingia miilini mwao kirahisi.
Kumbuka, bado hakuna tiba ya UKIMWI. Njia pekee ya kinga
ni kubadili tabia.

Shopping Cart