Dalili, athari, kinga na tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB)

Kifua kikuu ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya bacteria na kuenezwa kwa njia ya hewa. Mtu mwenye maambukizi ya kifua kifua kikuu akikohoa, kupiga chafya au kutema mate ovyo husambaza vijidudu hewa, huweza kumwabukiza mtu mwingine kama atakuwa hajaanza kutumia dozi ya kifua kikuu.

Dalili za kifua kikuu.

 1. Kukohoa kwa muda wa wiki mbili au zaidi
 2. Maumivu ya kifua
 3. Homa za usiku
 4. Kutoka jasho kwa wingi usiku
 5. Kupungua uzito
 6. Kukohoa damu
 7. Kukosa hamu ya chakula na mwili kuwa dhaifu

Athari za kifua kikuu.

 1. Ugonjwa huweza kuenea kwenye viungo vingine vya mwili.
 2. Watu wengine hupoteza maisha iwapo hawatapata tiba sahihi mapema.
 3. Watu wengine huambukizwa ugonjwa katika muda mfupi.
 4. Wagonjwa wa kifua kikuu hawazezi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendelea.
 5. Matibabu ya kifua kikuu huchua muda mrefu na ni gharama kubwa.

Kinga za ugonjwa wa kifua kikuu.

Ugonjwa huu unakingwa kwa chanjo ya kifua kikuu kwa kitaalamu (BCG) ambayo hutolewa mara tu mtoto anapozaliwa.

Ili kupunguza uwezekano wa kupata kifua kikuu zingatia yafuatayo;
 1. Kujenga na kuishi kwenye nyumba zinazoruhusu mzunguko kwa hewa ya kutosha (ziwe na madirisha makubwa ya kutosha)
 2. Epuka kukaa kwenye msongamano wa watu wengi
 3. Watoto wanyonyeshwe maziwa ya mama pekee kwa miezi sita na umlikiza kwa vyakula vyenye virutubisho ili kumjengea kinga imara
 4. Kula vyakula vyenye lishe bora
 5. Kutotema mate na makohozi ovyo ili kuziua usambaaji wa bacteria wasababishao Kifua kikuu.

Ratiba ya chanjo.

Chanjo ya kifua kikuu hutolewa baada ya mtoto kuzaliwa au anapofika kliniki kwa mara ya kwanza
Iwapo kovu kwa mtoto halijajitokeza chanjo irudiwe katika kipindi cha miezi 3.

Tiba ya kifua kikuu (TB)

Ugonjwa wa kifua kikuu unatibika. Matibabu yake huchukua muda mrefu wa miezi 6 hadi 8 na ni ya gharama kubwa.

Inashauriwa mgonjwa awahi matibabu mapema kwenye vituo vya kutolewa huduma za kinga.

Ugonjwa wa kifua kikuu ni hatari, hata hivyo unakingwa kwa chanjo.

Mzazi au mlezi hakikisha kila mtoto anapozaliwa anapata chanjo ya kuzuia kifua kuu

“Kumbuka chanjo ya kifua kikuu (BCG) Itamkinga mtoto dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu”.

Enjoyed? Rate this Article by click a Star Above and then Drop your Comment Below
OR Chat Live with AckySHINE here
Read and Write Comments
Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Shopping Cart