SALA YA UHAI KWA MT. YOSEFU

(Sala hii inafaa sana kwa ajili ya kutetea uhai wa watoto wachanga wakiwa tumboni mwa mama zao, dhidi ya utoaji mimba au hatari nyingine dhidi ya uhai wa binadamu)

Ee Mt. Yosefu, wewe ni Mchumba safi na Mpenzi wa Bikira Maria, u Baba Mlishi wa Yesu, mlinzi na mtunzaji wa Familia Takatifu, na wa familia zote. Tuna imani kabisa katika uangalizi wako uliojaa upendo, juu ya uhai mpya, na uaminifu wako kwa familia.

Tunaweka jitihada zetu chini ya ulinzi wa sala zako. Utusaidie daima katika kutetea zawadi ya uhai wa binadamu, ili ukue hadi uzima wa milele ulioahidiwa na kujaliwa kwetu na Mwanao, Ndugu yetu, Yesu Kristu.
Amina.

Jinsi Muda Unavyopotea, Jifunze kitu hapa

Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa miezi 12 au kwa mwaka.

Katika hayo masaa 24 unayoyapata kila siku unayatumiaje katika suala zima la kukufikisha katika ndoto na malengo au mafanikio yako?

Kwa nini kuna matajiri na maskini na wote tunapewa masaa 24???
Tucheki mgawanyo Wa masaa 24 ulivyo….katika masaa 24 unayopewa kwa siku masaa 8 ni ya kazi,masaa 8 ni ya kulala na masaa 8 ni ya kufanya mambo yako mengine.

Tuseme katika Masaa 8 kwa ajili ya mambo yako mengine labda masaa manne yanapotea katika foleni au purukushani za maisha kama kula nk.
Je haya mengine manne yanaenda wapi?Tunayapotezea wapi?
Kwenye mpira?kwenye movie?kwenye TV?kwenye mitandao ya kijamii?kukaa na kuwajadili wengine na mashosti?

Hivi unajua kwa siku una wastani Wa kupoteza masaa manne kwenye masaa yako 24??
Kwa wiki unapoteza masaa 28 hali kadhalika masaa 112 kwa mwezi hupotea.
Kwa mwaka mmoja wenye masaa 8760 una wastani Wa kupoteza masaa 1344 ambayo ni sawa na siku 56 kwa mwaka kwa makadirio ya haraka haraka.

Kwa maana nyingine kwa kutumia hii “concept” kila miezi 12 ya mwaka mzima unapoteza miezi miwili kwa mambo ambayo sio “productive”.
Hii ni sawasawa na kupoteza mwaka mmoja ndani ya miaka 6…kwa maana nyingine kwa “the same concept” ya masaa 4 kwa siku kupotea ni kwamba unapoteza mwaka mmoja kwa mambo ambayo hayakusaidii chochote.

Hebu jiulize hapo ulipo una umri gani?umeshapoteza miaka mingapi kwa mambo ambayo sio productive??
Kama wewe ni mfanyakazi au muajiriwa ukifanya kazi kwa muda Wa miaka 40 au kwa muda Wa miaka 40 unapoteza miaka 6.6.

Je hebu jiulize muda wote huo unaoupoteza kwenye mambo ambayo sio “productive” ungekuwa ni muda ulioutumia vizuri kwa mambo ya uzalishaji mfano kuanza kidogo kidogo kujenga biashara yako sasaivi tungekuwa na mamilionea na mabilionea wangapi?
Ili uweze kujenga biashara ambayo ni “strong” inakuhitaji angalau uijenge kwa muda Wa miaka mitano kwa maana nyingine kwa kutumia masaa manne tu kwa siku ndani ya miaka 40 utakuta tayari wewe ni milionea na baada ya kustaafu ajira usingeanza kuangaishana na pensheni (kwanza ni shilingi ngapi) au kuanza kubembeleza kuomba uongezewe mkataba au kwenda kufanya tena part time employment…..kwa concept hiyo ni mamilionea wangapi tumewapoteza??

Ndio maana katika hii dunia yetu tunayoishi matajiri wote ni 3% na 97% ya watu waliobakia wanawafanyia kazi matajiri.
Matajiri waliweza kuiona hii concept kwa jicho la Tatu na wakaanza kuifanyia kazi and the rest is history.
Huwezi kumkuta tajiri anapoteza muda wake kwa mambo ya kizembe yasiyomuingizia chochote ndio maana matajiri wanazidi kuwa matajiri na maskini wanaendelea kuwa maskini.

Lakini bado muda na nafasi unayo sasa ukiamua na ukianza kuutumia muda wako ulio nao kwa ajili ya kuyatengeneza maisha yako.
Watu wengi hawako tayari kuumia na kujifunza biashara na kuielewa ndani ya miaka mitano itakayowapelekea kuwa matajiri na kuweza kuyafikia malengo na ndoto zao lakini wapo tayari kuajiriwa na kufa maskini ndani ya miaka 40.

Muda mzuri ndio sasa Wa kufanya maamuzi sahihi Wa kuyawekeza masaa manne kwenye biashara ili uje upate matokeo chanya.

Mafundisho kuhusu Neema

Je, tunaweza kuhakikisha neema ya utakaso?
Hapana, hatuwezi kuhakikisha neema ya utakaso kwa kuwa ni tukio ambalo linapita maumbile na kufanyika rohoni, hivyo halifikiwi na hisi zetu. Pengine Mungu anatokeza dalili fulani za badiliko hilo kama vile furaha ya ndani au karama ya nje, lakini hizo hazihitajiki wala hazitoshi kuthibitishia mtu amepata neema hiyo.
“Wengi wataniambia siku ile: Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri: Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu” (Math 7:22-23).
“Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu” (1Kor 13:1-3).

Neema ni nini?
Neema ni kipaji cha roho kinachopita nguvu za viumbe vyote; ndicho kipaji tupewacho na Roho Mtakatifu ili tupate uzima wa milele. (Lk 1:30, Rum 5:2)

Kuna aina ngapi za neema?
Kuna aina mbili za neema
1. Neema ya utakaso
2. Neema ya msaada

Neema ya Utakaso ni nini?
Neema ya Utakaso ni uzima wa Kimungu unaomiminwa na Roho Mtakatifu mioyoni mwetu. (Yoh 1:16, Yoh 3:3-5)

Neema ya Utakaso yapatikanaje?
Neema ya Utakaso yapatikana kwa;
1. Kwanza kwa Sakramenti ya Ubatizo
2. Sakramenti ya Kitubio
3. Kwa majuto kamili (majuto ya mapendo)
4. Yaongezwa kwa kupokea Sakramenti nyingine
5. Kwa Sala
6. Kwa Ibada Takatifu
7. Kwa matendo mema

Neema ya Utakaso yapoteaje?
Neema ya Utakaso yapotea kwa kutenda dhambi kubwa (dhambi ya mauti)

Kuna Faida ya kuwa na Neema ya Utakaso?
Faida ya kuwa na Neema ya Utakaso ni;-
1. Kupendwa na Mungu hapa duniani
2. Na kupokelewa kwake mbinguni baada ya kufa

Neema ya Msaada ni nini?
Neema ya Msaada ni msaada tupatao kwa Roho Mtakatifu kutuongezea nguvu Rohoni tutende mambo mema na tuepuke Mabaya

Neema ya Msaada yapatikanaje?
Neema ya Msaada yapatikana kwa kupokea Sakramenti, kusali, na kutenda mambo ya Ibada (Yoh 15:5, 1Tim 2:4)
Shopping Cart