Jifunze kanuni za fedha
kama ilivyoainishwa hapo chini.
Fedha inatakiwa uwe na nidhamu nayo katika kutumia
Hii kanuni inatumika kwenye vyanzo vyako vyote vya fedha ili uwe na mafanikio yenye amani
Tuangalie hapa chini hizi kanuniπππ
Fungu la kumi 10%
Akiba 30%
Matumizi 40%
Dharura 10%
Msaada 5%
Sadaka 5%
ππhii kanuni inafanya kazi katika kila hela unayopata kama faida
Mfano : mtu mwenye mshahara wa mil 1 unayoipata kila mwezi baada ya makato
Fungu la kumi 10% (Tithe) hii ni mali ya Mungu si yako!!
πitakuwa ni sh laki 1 unatakiwa uitoe sehemu unayoabudia kila mwezi na kama unabiashara zako faida yake ndani yake toa fungu la kumi
Pia hata kama ni hela unapewa kama zawadi itolee fungu la kumi
πfaida ya hii
πΈinalinda kazi au Biashara unayoifanya zidi ya adui
πΈmagonjwa,ajali , ( vitu vitakavyokufanya utumie hela bila mpangilio),etc yanakuwa mbali nawe
Akiba 30%
πhii unaiweka kwa matumizi yako ya baadae kama kujenga,kusomesha,kulima, investment, etc
πunatenga laki 3 kwa mtu anaepokea mil 1
Matumizi 40%
πhii itatumika kwa matumizi ya kila siku ,chakula ,Maji, etc
πhapa unatenga laki 4 kwa ajili ya matumizi kwa mtu wa mshahara wa mil 1
πnote : hapa ndio hela yako ya kustarehe inatoka
Angalia matumizi yasizidi hela uliyonayo
πwengi wao hapa watu ndio inamfanya awe na vyanzo vingi vya hela ili aweze kufanya starehe awezavyo
πpia hii ndio hela unayotoa kwa ajili ya mbegu (sadaka ya gharama) wanaoifahamu
Dharura 10%
πhii fedha unaitunza kwa ajili ya vitu usivyotarajia kama msiba, ndugu kuumwa au kukwama etc
πunatunza laki 1 kwa mtu wa mshahara wa mil 1
Msaada 5%
πhii inawahusu watoto yatima, wajane na wasiojiweza kama vilema
πunatoa elfu 50 kwa mtu wa mshahara wa mil 1
πunaigawa kama unamagroup yote hayo
Sadaka 5%
πhii unatoa elfu 50 kwa mtu wa mshahara wa mil 1
πigawe mara NNE coz mwezi una jumapili 4 ambayo utapata ni elfu 12500 ivyo basi kila jumapili peleka sadaka elfu 12500
Note:
πKitu chochote kinachoitwa sadaka kiombee kabla hujakitoa kama siku 2 au 3 ndio uitoe
sadaka
πnakama unahitaji kitu mfano Nguo peleka nguo kwa waitaji uone utakavyopata Nguo
Nyingi
πchukua mfano Bakhresa na Mengi wanavyojitolea mbona hawaishiwi, siri yao iko kwenye nidhamu hii ya pesa!!
Jaribu na wewe anza hata na kidogo kidogo kuwa na nidhamu na fedha uone nayo itakavyokuheshimu
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE