Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Njia ya kutambua kama umeambukizwa Virusi vya UKIMWI (VVU)?

Njia pekee ya kujitambua kama umepata maambukizo ya
VVU ni kufanya kipimo cha damu (HIV-test). Vipimo hivi
vinapatikana katika vituo vya afya na pia kupitia vituo maalumu
vya ushauri nasaha vya kupima kama vile vya Angaza, huduma
hizi zimesambaa nchi nzima. Kipimo hiki huchukua kiasi kidogo
cha damu na kawaida majibu hupatikana baada ya muda mfupi.
Mshauri nasaha ataongea na wewe na kukuelimisha zaidi kuhusu
kipimo na maana ya majibu.

Kwa nini watu wanaamini kuwa Albino hawana maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (VVU)?

Imani hiyo si kweli kabisa. Inawezekana ni kupotoshwa kwa
makusudi wa ukweli kuhusu jambo hilo kunakofanywa na watu
wachache katika jamii ili kuendeleza matendo yao maovu. Watu
wanaweza kufuata imani potofu na zisizo na msingi wowote ili
kukwepa ukweli kuhusu VVU na UKIMWI. Kwa mfano; imani
kuwa mtu anaweza kupona UKIMWI kwa kufanya mapenzi na
bikira, mlemavu au Albino ni za uongo na hazina msingi wowote.
VVU huambukizwa kupitia majimaji ya mwili, na njia kuu ya
maambukizo ni kujamiiana bila kinga. Njia pekee za kuzuia
maambukizo ni kuacha kabisa kufanya ngono, kuwa na mpenzi
mmoja muaminifu au kutumia kondomu.Watu wanaoeneza imani hizi
potofu wanatafuta njia mbadala ya kuhalalisha tabia zao mbaya.

Wewe pia kama Albino unatakiwa kupambana na imani hizo
potofu kwani zinalenga kueneza madhara kwa watu wanaoishi
na ualbino.

Je, serikali imechukua hatua gani kudhibiti hali hii ya mauaji ya Albino? Tutaishi vipi?

Kifungu cha 14 cha Katiba ya Tanzania kinaeleza kwa ufasaha
kuwa: “Kila mtu ana haki ya kuishi na kulindwa utu wake katika
jamii kwa misingi ya sheria.” Hata Rais Kikwete katika hotuba
zake kwa Taifa za kila mwezi amewahi kukemea mauaji haya
mwaka 2008 kwa kusema; “ mauaji haya ni aibu na fedheha
kubwa kwa jamii yetu” pia “ukatili usio na sababu” na akaendelea
kusema, “ni lazima yakomeshwe mara moja.”
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na taasisi na asasi za
kijamii wanaendelea kutoa mafunzo, taarifa na mazingira
yatakayowawezesha Albino kuishi maisha bora na yenye
mafanikio katika jamii.

Je, zipo sheria zinazolinda watu wenye ulemavu hapa Tanzania?

Ndiyo, zipo sheria
hapa T a n z a n i a
z i n a z o w a l i n d a
watu wenye
ulemavu. Tanzania
ilitia saini na
kuridhia mkataba
wa kimataifa wa
ulinzi, haki na
usawa kwa watu
wenye ulemavu
mwaka 2006. Kwa
kitendo hicho
cha kuridhia
mkataba huo wa
kimataifa Tanzania
imeonyesha nia
yake ya kuwalinda
na kudumisha
haki za watu
wenye ulemavu.
Hata katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
19772 inakataza ubaguzi wa aina yoyote kwa watu wenye
ulemavu.
Zipo sheria nyingi zinazolinda haki na usawa kwa watu wenye
ulemavu ambazo zinahusika na sekta mbalimbali. Kwa mfano;
elimu na mafunzo, ajira3, matunzo4 na ustawi5 kwa ujumla. Ipo
pia sera ya Taifa kuhusu ulemavu ya mwaka 20046. Sera hii
imeweka mazingira muafaka kwa watu wenye ulemavu kupata
haki sawa katika maendeleo ya kijamii, ikiwa ni pamoja na
kupata huduma na mahitaji ya msingi kutoka katika jamii.


Sheria zinazolinda haki za Albino

Hakuna sheria mahususi inayowalenga watu wanaoishi na ualbino
hapa Tanzaina. Ingawaje haki za msingi za Albino zinalindwa
chini ya Katiba
ya nchi pamoja
na Sheria
z i n a z o h u s i k a
na sekta
m b a l i m b a l i .
Sheria hizi
zinakataza na
kukemea aina
zote za ubaguzi
kwa misingi ya;
rangi, kabila,
ulemavu na
kadhalika.
Sera ya Taifa ya ulemavu inabainisha hali ya ulemavu kuwa ni,
“kutokuwa au kupungukiwa na uwezo wa kushiriki kwa usawa
katika shughuli za kawaida za kijamii kutokana na sababu
za mapungufu ya kimwili, akili au kijamii”. Sera hii inatoa
mwongozo wa kutolewa kwa haki na fursa sawa kwa walemavu
kupata mambo na huduma za msingi kama; elimu, taarifa, ajira,
matunzo, huduma za afya, kumudu na kufikia huduma muhimu.
Katika siku za karibuni kumeongezeka vitendo vya kikatili dhidi
ya Albino ambavyo ni pamoja na mauaji ya kikatili na kukatwa
viungo kutokana na imani za kishirikina. Watu wenye ualbino
wanalindwa kisheria kutokana na vitendo hivi kwa kupitia
sheria zilizopo za makosa ya jinai.

Serikali pia imechukua hatua za kudhibiti hali hii isiendelee
kutokea ikiwa ni pamoja na kuanza kuwaandikisha rasmi
(kufanya sensa) watu wenye ualbino, na pia kuanzishwa
kwa ulinzi kwa Albino kupitia jeshi la polisi na jamii kwa ujumla,
kwa mfano; watoto Albino wanapokwenda shule.
Suala la Albino limeendelea kupewa umuhimu mkubwa kitaifa,
ikiwa ni pamoja na mjadala wa kitaifa. Mfano; ujumbe wa mbio
za Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2009 ulilenga kuhamasisha
jamii kuhusu mauaji na vitendo vya kikatili dhidi ya Albino.
Mauaji na vitendo vya kikatili dhidi ya Albino vinavyotokea
sasa hivi pia vimepelekea serikali kuchukua hatua na kuongeza
ulinzi ili kulinda haki za Albino kwa mfano; zimeundwa
mahakama maalumu za kusikiliza makosa hayo ili kuharakisha
upatikanaji wa haki kwa wahusika. Mpaka sasa watuhumiwa
saba wa mauaji ya Albino wamekutwa na hatia na kuhukumiwa
kifo kwa kunyongwa.

Albino anaweza kuwa na maisha ya kawaida na yenye mafanikio katika maisha?

Imani iliyojengeka kwenye jamii kuwa Albino wana uwezo
mdogo si ya kweli. Ipo mifano mingi ya watu walioweza kupata
mafanikio katika maisha ambao pia ni Albino. Wapo ambao ni
walimu, wanasayansi, wanasheria, na wengine wapo kwenye
siasa na uongozi.
Mbunge wa Lindi mjini kupitia chama cha CUF mheshimiwa
Salum Khalifan Barwani.
Mbunge wa viti maalumu wanawake Mheshimiwa. Al-Shymaa
Kway-Geer, muimbaji maarufu wa muziki wa kizazi kipya (bongo
flava) Keisha,
mwanasheria Abdallah Possi na Sizya Migila ambaye ni afisa
utawala wa Taasisi ya Uhasibu ya Taifa ni mifano mizuri
inayoonyesha Albino waliopata mafanikio katika maisha yao.
Mwanamuziki wa kimataifa wa Afro-pop kutoka nchi ya Mali
anayeitwa Salif Keita amefikia mafanikio makubwa sana duniani
kote kuanzia bara la Afrika na Ulaya kiasi cha kuitwa, “Sauti
ya Dhahabu.” Yeye alizaliwa katika familia ya muasisi wa Taifa
la Mali Ndugu Sundiata Keita. Hii pia inadhihirisha kuwa Albino
anaweza kuzaliwa katika familia yoyote kuanzia zile za kifalme
na hata familia maskini za wakulima vijijini.

Shopping Cart