Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Ni asilimia ipi ya Watanzani ambao wameambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Nchini Tanzania ni 7% ya watu wenye umri kati ya miaka 15-49 wana maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Hii i ii inamaanisha kuwa kati ya watu 100 wa umri huu 7 wao wameambukizwa na Virusi vya UKIMWI.
Kila mkoa una watu walioambukizwa kwa kiwango tofauti, mikoa mingine i ikiwa na kiwango cha juu . Jedwali lilioambatanishwa hapa linaonyesha Mkoa wa Mbeya, Iringa na Dar es Salaam kuathirika zaidi na i idadi kubwa ya watu waliopima na kuonekana kuwa na virusi vya UKIMWI.

Mama mwenye virusi vya UKIMWI na UKIMWI, anaweza kuzaa mtoto?

Na anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni au wakati wa kumnyonyesha?
Ndiyo, mama mwenye virusi vya UKIMWI na UKIMWI anaweza kubeba mimba kama mwanamke mwingine yeyote. Ila ni muhimu kukumbuka kwamba kuna uwezekano wa mtoto kuambukizwa na Virusi vya UKIMWI.

Lakini siyo watoto wote waliozaliwa na mama mwenye maambukizi watabeba virusi. Kuwa moto ataambukizwa au hataambukizwa i itategemea na i idadi ya virusi ambavyo viko kwenye damu ya mama na sababu nyingine. Tafiti zimeonyesha kwamba watoto wawili kati ya watoto watatu waliozaliwa na akina mama wenye maambukizi ya Virusi huambukizwa na hivyo virusi.
Pamoja na hayo, mama mwenye virusi vya UKIMWI anaweza kumwambukiza mtoto wake wakati wa kumnyoshesha kwa sababu ya kuwepo virusi kwenye maziwa ya mama. Akina mama walio na maambukizi ya UKIMWI na UKIMWI wanashauriwa kuacha kuzaa na kutumia njia za uzazi wa mpango

Je, nikitoa au kupata damu hospitalini, itakuwepo hatari ya kupata virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Katika swali hili lazima tutofautishe kati ya kutoa damu na kuwekewa damu. Kutoa damu hakuleti hatari, kama mtaalamu wa afya aliyechoma sindano kwa ajili ya kutoa damu anatumia sindano na vifaa vilivyochemshwa.
Kwa kawaida hakuna matatizo kuongezwa damu, kwa sababu damu i inapimwa kabla ya kumuongeza mgonjwa hospitalini. Iwapo damu i imepimwa na sindano zilizochemshwa zimetumika hakuna ubaya wowote katika kuongezwa damu.

Je, nikila na mtu mwenye Virusi vya UKIMWI, nitaambukizwa na virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Hapana, ukila na mtu mwenyemaambukizi ya Virusi vya UKIMWI huwezi kuambukizwa Virusi vya UKIMWI wala UKIMWI, isipokuwa pale ambapo wote wawili mna vidonda mdomoni na mnachangia kijiko kimoja. Lakini uwezekano huu ni mdogo sana, kiasi tunachoweza kusema kwamba huwezi kuambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI ukila sahani moja na mtu aliyeambukizwa na virusi.
Lakini, kufuatana na kanuni za afya, ni vizuri zaidi kila mtu atumie vifaa vyake na baada ya kuvitumia avioshe kikamilifu.

Je, ninaweza kuambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwa kuumwa na mbu?

Hapana, mbu na wadudu wengine hawawezi i kukuambukiza virusi vya UKIMWI kutokana na mfumo wa mii li yao. Virusi vya UKIMWI haviwezi kuishi kwenye mii li yao, kwa sababu siyo mazingira vinavyoyapenda. Virusi vya UKIMWI vinajilisha na kuzaliana katika chembechembe nyeupe za damu, lakini chembechembe za aina hii hazipo katika mwili wa mbu. Kwa hiyo, virusi vya UKIMWI vinakufa mara baada ya mbu kufyonza damu na akingโ€˜ata mtu mwingine baadaye hakuna hatari ya kuambukizwa.
Thibitisho jingine la ukweli huu ni kwamba sisi sote tungekuwa tumebeba virusi vya UKIMWI kama mbu angelikuwa anaambukiza kwa sababu sisi sote tunaishi katika mazingira yenye mbu na karibu na watu wengine.

Shopping Cart