Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Je, nikiambukizwa virusi vya UKIMWI na UKIMWI nifanye nini?

Jambo la msingi ni kutokukata tamaa na kuwa na matumaini. Mara nyingine i inasaidia kama utakuwa na mazungumzo na watu ambao tayari wanaishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI au marafiki na ndugu unaowaamini. Jaribu kuongea na mwenzi wako i ili kumfahamisha juu ya hali yako ya maambukizi. Yeye pia anaweza kuwa ameambukizwa na angependa kupima. Ni muhimu kuzingatia kanuni muhimu za afya nzuri kama vile kula vyakula vyenye mlo kamili na kujiweka katika hali ya usafi. Kwa mantiki hiyo hiyo ni lazima kuharakisha kutibu maradhi mengine yatakayojitokeza. Watu wanaoishi na virusi i vya UKIMWI wanashauriwa wasitumie pombe wala kuvuta sigara, kwa sababu vyote hivyo huchangia katika kudhoofisha mwili. Kama watafanya ngono, ni lazima watumie kondomu i ili wasiambukize wengine.
Aliyeambukizwa, baada ya miaka kinga ya mwili i wake i itaanza kupungua na atatakiwa kupata dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARV).
Kama mtu aliyeambukizwa na virusi vya UKIMWI atazingatia masharti haya, kuna uwezekano wa kuishi na kufurahia maisha kwa miaka mingi.

Niende wapi kupima kama nina Virusi vya UKIMWI?

Vituo vyenye utaalamu na katika hospitali i au Taasisis kama vile Shirika la Amref au CCBRT wana uwezo wa kutoa ushauri nasaha na vipimo vya kuaminika. Ushauri nasaha unakusaidia wewe kuelewa kipimo hicho ni cha nini, ni majibu gani yanayoweza kupatikana au kutopatikana. Upimaji huu hufanywa kwa siri, ni wewe tu pekee yako unaweza kupewa majibu. Katika miji mingi, vituo vya ANGAZA vipo na pia vituo hivi hutoa huduma rafiki kwa vijana.
Huduma za upimaji hazipatikani kwa urahisi sehemu za vijijini kwa sababu vyombo vinavyotumika katika upimaji ni vya gharama kubwa na vinahitaji umeme na uangalizi mkubwa. Mpaka sasa huduma hizi zinapatikana katika hospitali na kwa baadhi ya mashirika yanayojishughulisha na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Jambo nzuri ni wewe kuuliza habari zaidi katika kituo cha afya kilicho karibu nawe.

Nifanye nini ili kujua kama nina au sina maambukizi ya Virusi vya UKIMWI?

Ipo njia moja ya kuhakikisha kama umeambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI au hapana. Njia hii ni ya kupima damu yako katika vituo vyenye utaalamu wa upimaji.
Ni muhimu kukumbuka kuwa Virusi vya UKIMWI, vinaonekana kwenye damu ya binadamu miezi mitatu baada ya kuambukizwa. Kipindi hiki kati ya kuambukizwa hadi kufikia miezi mitatu kipimo hiki i hakiwezi kuonyesha kama maambukizi ya virusi yapo au hayapo. Kipindi hiki ni cha hatari sana , kwani aliyeambukizwa anaweza kuwaambukiza wengine bila kujua.

Je, nifanye nini ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Hakuna chanjo dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI, Lakini kuna mienendo ya tabia ambayo i itaweza kukusaidia kujikinga na maambukizi ya UKIMWI na UKIMWI. Kutokufanya ngono kabisa ni njia mojawapo ya kujikinga na maambukizi ya UKIMWI na UKIMWI. Kuwa mwaminifu na kuwa na mpenzi i ambaye hajaambukizwa ni njia nyingine ya kujikinga. Lakini hii i ii inahitaji wote muwe katika afya nzuri ( bila maambukizi) wakati mnaanza uhusiano wa kujamii ana kwa mara ya kwanza.
Pia i inashauriwa hima kutafuta matibabu ya magonjwa ya ngono mara pale yatakapojitokeza. Vidonda vinavyosababishwa na magonjwa ya ngono vinasababisha mwingiliano wa maji maji ya ukeni, maji maji ya uumeni na damu wakati wa kujamii ana na kuwezesha Virusi vya UKIMWI kupita kwa urahisi.
Kufuata kanuni za ngono salama ni njia nyingine ya kujikinga ili usiambukizwe na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Ngono salama kwa upande mwingine ni kitendo cha kukaribiana ambacho hakitahusisha uume kuingia ukeni au njia ya haja kubwa. Pia utumiaji wa kondomu kila wakati ngono i itahusisha kuingizwa kwa umme, ukeni au njia ya haja kubwa ni njia nyingine ya kujikinga

Shopping Cart