Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Nikitumia nyembe kali au sindano pamoja na mtu mwenye Virusi vya UKIMWI ninaweza kupata Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Ndiyo, unaweza kuambukizwa ukitumia nyembe kali au sindano kwa kuchangia pamoja na mtu mwenye virusi i vya UKIMWI. Matumizi ya vyombo vyenye makali, kama sindano, visu au nyembe yana hatari. Kama baada ya kutumika damu husalia katika vyombo hivi, na endapo vitatumika bila kutakaswa au kuchemshwa, matumizi yake yanaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa mbalimbali, pamoja na UKIMWI.
Kwa hiyo ni muhimu sana kutochangia vifaa vyenye makali na watu wengine au lazima kuvitakasa na kuchemsha kila baada ya kuvitumia.

Kwa nini nao watu wanaishi kwenye ndoa wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Kuna sababu kuu mbili i kwa wana ndoa kupata maambukizi i ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Kwanza, i inawezekana kuwa mmoja kati yao alikuwa tayari na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kabla ya siku ya kuoana. Kwani hata mtu aliyeambukizwa na Virusi vya UKIMWI anaweza kuonekana mwenye afya nzuri i na kuwa navyo mwilini siku ya harusi. Hii ni pale ambapo awali alifanya ngono na mtu aliyeambukizwa Virusi i ama alivipata kwa kupitia njia nyingine kwa mfano, njia ya damu i siyo salama..
Kama mtu aliwahi kufanya ngono kabla, njia pekee ya kuhakikisha kuwa hana virusi kabla ya kufunga ndoa ni kwenda kupima damu.
Pili, wanandoa hao wanaweza kuambukizwa baada ya kufunga ndoa, pale ambapo mwenzi mmoja atafanya mapenzi na mtu mwingine. Kama mmoja wao au wote wawili watafanya ngono na mpenzi mwingine (mahusiano nje ya ndoa) wanaweza kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Je, nitaweza kupata virusi vya UKIMWI na UKIMWI nikijamiiana na msichana au mvulana wa umri mdogo sana?

Ndiyo, utaweza kuvipata virusi vya UKIMWI. Uwezekano wa kuambukizwa hautegemei umri wa mpenzi wako, lakini unategemea afya yake! Kama huyu msichana au mvulana tayari ameshapata virusi vya UKIMWI na unajamii ana naye utaweza kuambukizwa.
Mara nyingi huwezi kufahamu kama mtu ana virusi vya UKIMWI au hapana, kwa sababu katika hatua ya mwanzo baada ya kuambukizwa hakuna dalili zozote za kuugua.
Vilevile ni tabia mbaya sana kushawishi wasichana au wavulana wadogo kujamii ana. Kwa usalama na faida ya wote, mnashauriwa kuacha mapenzi na wasichana au wavulana wadogo.

Shopping Cart