Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Je, mwanaume anaweza akajua kama amempa msichana mimba siku ileile walipojamiiana?

Hapana, hamna njia ya kufahamu kama amempa msichana mimba siku i ileile wanapojamii ana. Inachukua muda kwa mwili kuonyesha dalili za mimba.
Msichana akitaka kwenda kliniki kupimwa mkojo, kwanza ahesabu tarehe i ipi alikuwa anategemea kupata hedhi yake.
Kama anakosa hedhi katika muda aliotegemea, i itambidi aende kliniki. Mimba i inaonekana kwenye kipimo cha mkojo wakati ambapo mwanamke alitakiwa kwenda mwezini. Msichana akienda kupimwa mkojo kabla, hali halisi kuhusiana na ujauzito haiwezi kutambuliwa.

Dalili za kwanza za msichana au mwanamke kuwa na mimba ni zipi?

Dalili moja i iliyo wazi zaidi ni kukosa hedhi. Mwanamke akijamii ana na mwanaume bila kutumia kinga yoyote na asipopata hedhi katika muda unaotakiwa, mara nyingi i i ina maana kwamba amepata mimba.

The ListPages module does not work recursively.

Dalili nyingine ni kuvimba matiti na chuchu kuchomachoma. Baadhi ya wanawake wanaota mavuzi mengi na wengine wengi rangi ya chuchu i inabadilika kuwa nyeusi. Pia, karibu nusu ya wanawake wajawazito huumwa tumbo na wengine hutapika. Wanawake wengi husikia mkojo mara kwa mara na wengine hujisikia wachovu na kuona kizunguzungu, hasa katika miezi mitatu ya mwanzo. Wakati mwingine wanawake hupenda au huchukia baadhi ya vyakula.

Ili mwanamke awe na uhakika kama ni mjamzito au hapana, akapimwe mkojo kwenye kliniki au hospitalini, mara anapokuwa na wasiwasi

Je, mapacha wanapatikanaje?

Zipo aina mbili za mapacha, wale wanaofanana na wale wasiofanana. Karibu robo ya mapacha wote hufanana. Hii ina maana kwamba wametokana na yai moja lililotungwa mimba ambalo hujigawa katika makundi mawili tofauti ya chembechembe, kila mojawapo hubadilika kuwa kiumbe pekee. Hadi sasa, wataalamu hawaelewi vizuri sababu za yai kujigawa. Mapacha wa aina hii , kwa vile wametokana na yai moja, mara zote huwa na jinsia moja na hufanana sana kimaumbile.
Mapacha wasiofanana hutokea wakati wa yai kupevuka, kokwa za mwanamke hutokea zikawa mayai mawili badala ya moja tu. Mayai yote mawili hurutubishwa na hutungishwa mimba kwa mbegu mbili tofauti za mwanaume. Viumbe viwili hukua wakati mmoja katika mfuko wa uzazi. Mbali ya kukua katika mfuko mmoja wa uzazi na kuwa na umri uleule, mapacha hawa ni sawa sawa na watoto wengine wawili wa wazazi haohao. Wanaweza kuwa wa jinsia na maumbile tofauti kabisa.

Je, kama mwanamke na mwanaume wanapata watoto wa jinsia moja tu, ni kosa la nani?

Hakuna mwenye kosa, kwa sababu jinsia ya mtoto i inategemea na bahati na hamna uwezekano wa kupanga kuzaa aina fulani ya mtoto. Tulivyoona juu ni mwanaume ndiye aliye na aina mbili za mbegu. Aina moja husababisha kutokea mtoto wa kike na aina nyingine mtoto wa kiume. Mwanaume hana uwezo wa kuhakikisha achangie aina ya mbegu gani. Kwa hiyo, hata kama ni mwanaume anayeyakinisha jinsia ya mtoto, hana kosa, kwa sababu hana uwezo wa kuamua achangie mbegu ya aina gani.

Je, unaweza kupanga kuzaa aina ya watoto, yaani wa kiume au wa kike tu?

Mimba i inatungwa wakati yai la kike linaporutubishwa na mbegu za kiume. Kama tulivyoona hapo juu, jinsia ya mtoto i inategemea aina ya mbegu za kiume. Nusu ya mbegu za mwanaume zinatengeneza mtoto wa kiume na nusu ya mbegu zinatengeneza mtoto wa kike. Lakini wanaume hawana uwezo wa kuamua aina ya mbegu i itakayorutubisha yai. Kwa hiyo, haiwezekani kupanga. Jinsia ya mtoto i nategemeana na bahati tu.

Shopping Cart