Baini Siri za Kuwa na Afya Bora na Utimamu

Faida 10 za kulala mapema kiafya

Mapera ni matunda yanayo patikana kwa wingi lakini mara nyingi huwa hayapendelewi sana kutokana na ugumu wake wakati wa kuyatafuna pamoja na kuwa na mbegu mbegu nyingi. Hata hivyo matunda haya yana faida kubwa sana kwa afya ya mwili wa mwanadamu.

Zifuatazo ni faida kumi za mapera:

1. Utajiri wa Vitamin C.

Mapera yana utajiri mkubwa wa Vitamin C ambayo ni muhimu sana katika mwili wa mwanadamu.

2. Ni kinga nzuri ya kisukari.

Ulaji wa watu wengi unawaweka katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari lakini matumizi ya mapera yatakupunguzia hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari Hii ni kwa sababu mapera yana utajiri mkubwa sana wa Fibre.

Fibre ni muhimu sana katika kupunguza kiasi cha sukari kwenye damu. Vilevile ni muhimu sana katika kuusafisha mfumo wa usahihi.

3. Kuimarisha Uwezo Wa Kuona

Mapera yana utajiri mkubwa sana wa Vitamin A au Retinol ambayo ni muhimu sana katika kusaidia kuona vizuri. Hivyo basi kama ilivyo kwa karoti, mapera yanasaidia sana katika kuongeza na kuimarisha uwezo w a mtu kuona.

4. Kusaidia katika Uzazi

Mapera yana madini yaitwayo Folate ambayo husaidia katika kurutubisha mayai ya uzazi.

5. Kurekebisha Kiwango Cha Shinikizo La Damu

Madini ya Potassium yaliyomo ndani ya mapera yanasaidia katika ku-normalise shinikizo la damu ( Blood Pressure )
Ndizi na mapera vina kiwango cha potassium sawa.

6. Utajiri mkubwa wa Madini Ya Shaba

Mapera yana madini ya shaba ( Trace element copper ) ambayo ni mazuri sana katika ku- maintain ufanyaji kazi wa tezi ziitwazo thyroid.
Tezi za thyroid zisipo fanya kazi vizuri zinaweza kusababisha matatizo mengi ya kiafya kwa mwanadamu.

7. Utajiri wa Madini Ya Manganese

Mapera yana utajiri mkubwa wa madini ya manganese ambayo yanausaidia mwili katika kunyonya ama kupata virutubisho muhimu kutoka kwenye vyakula tunavyo kula.

Chakula tunacho tumia kikitumika vizuri mwilini, tunapata virutubisho vyote muhimu kama vile biotini, vitamin nakadhalika.

8. Kuusadia mwili na akili katika ku-relax.

Mapeara yana utajiri mkubwa wa madini ya magnesium ambayo hufanya kazi ya kuvifanya akili na mwili wa mwanadamu viweze ku relax. Unashauriwa kutumia mapera baada ya kazi nzito. Hii itasaidia katika kuufanya mwili na akili yako kutumika.

9. Mapera ni muhimu katika afya ya akili ya mwanadamu.

Vitamin B3, Vitamin B6 ambazo zinapatikana ndani ya tunda la mpera muhimu katika kuimarisha afya ya akili ya mwanadamu. Mapera yatasaidia kuufanya ubongo wako u relax.

10. Ni muhimu sana katika ngozi ya mwanadamu

Vitamin C, viondoa sumu na karotini ambavyo vyote vinapatikana ndani ya tunda la mpera ni muhimu sana katika kuimarisha afya ya ngozi.

Kama hiyo haitoshi, kokwa la mpera huwa linatumika katika kutengeneza vipodozi na losheni kwa ajili ya matumizi ya mwanadamu.

Faida 10 za kula tende kiafya

Kila wakati unashauriwa na watalam wa afya ya kwamba unatakiwa kula tende kwa wingi ili kupata faida zifuatazo katika mwili wako:

1. Huongeza nguvu kutokana na kuwa na sukari ya asili, unaweza kuchanganya na maziwa na kupata mchanganyiko bora!

2. Huzuia meno kuoza, na ni tiba nzuri kwa wagonjwa wa anemia kutokana na kuwa na madini mengi ya chuma.

3. Hupunguza uwezekano wa kupata Kiharusi (stroke) kwani hazina cholesterol kabisa! Pia zina vitamini na madini kwa wingi.

4. Huongeza uwezo wa Kujamiiana kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha nguvu

5. Hupunguza madhara ya pombe mwilini na kurudisha afya ya mtu.

6. Zina kiasi kikubwa cha kamba kamba ambazo hufanya mtu apate choo kirahisi na laini.

7. Licha ya kuwa tamu, tende haziongezi kiwango cha sukari mwilini, hivyo zinaweza kutumika kama mbadala wa sukari

8. Huimarisha Mifupa na kuondoa maumivu ya mara kwa mara ya mifupa kutokana na kuwa na madini ya chuma na potassium kwa wingi.

9. Tende ina msaada mkubwa kwa mama mjamzito, humuongeza nguvu, na hazina madhara kiafya kwa mtoto. Pia husaidia kupata uzazi salama

10. Ulaji wa tende kwa wingi husaidia kuongeza mwili kwa wale waliokonda kupita kiasi. Hivyo hushauriwi kula tende kupita kiasi kama huhitaji kuongeza mwili.

Dalili, athari, kinga na tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB)

Kifua kikuu ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya bacteria na kuenezwa kwa njia ya hewa. Mtu mwenye maambukizi ya kifua kifua kikuu akikohoa, kupiga chafya au kutema mate ovyo husambaza vijidudu hewa, huweza kumwabukiza mtu mwingine kama atakuwa hajaanza kutumia dozi ya kifua kikuu.

Dalili za kifua kikuu.

  1. Kukohoa kwa muda wa wiki mbili au zaidi
  2. Maumivu ya kifua
  3. Homa za usiku
  4. Kutoka jasho kwa wingi usiku
  5. Kupungua uzito
  6. Kukohoa damu
  7. Kukosa hamu ya chakula na mwili kuwa dhaifu

Athari za kifua kikuu.

  1. Ugonjwa huweza kuenea kwenye viungo vingine vya mwili.
  2. Watu wengine hupoteza maisha iwapo hawatapata tiba sahihi mapema.
  3. Watu wengine huambukizwa ugonjwa katika muda mfupi.
  4. Wagonjwa wa kifua kikuu hawazezi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendelea.
  5. Matibabu ya kifua kikuu huchua muda mrefu na ni gharama kubwa.

Kinga za ugonjwa wa kifua kikuu.

Ugonjwa huu unakingwa kwa chanjo ya kifua kikuu kwa kitaalamu (BCG) ambayo hutolewa mara tu mtoto anapozaliwa.

Ili kupunguza uwezekano wa kupata kifua kikuu zingatia yafuatayo;
  1. Kujenga na kuishi kwenye nyumba zinazoruhusu mzunguko kwa hewa ya kutosha (ziwe na madirisha makubwa ya kutosha)
  2. Epuka kukaa kwenye msongamano wa watu wengi
  3. Watoto wanyonyeshwe maziwa ya mama pekee kwa miezi sita na umlikiza kwa vyakula vyenye virutubisho ili kumjengea kinga imara
  4. Kula vyakula vyenye lishe bora
  5. Kutotema mate na makohozi ovyo ili kuziua usambaaji wa bacteria wasababishao Kifua kikuu.

Ratiba ya chanjo.

Chanjo ya kifua kikuu hutolewa baada ya mtoto kuzaliwa au anapofika kliniki kwa mara ya kwanza
Iwapo kovu kwa mtoto halijajitokeza chanjo irudiwe katika kipindi cha miezi 3.

Tiba ya kifua kikuu (TB)

Ugonjwa wa kifua kikuu unatibika. Matibabu yake huchukua muda mrefu wa miezi 6 hadi 8 na ni ya gharama kubwa.

Inashauriwa mgonjwa awahi matibabu mapema kwenye vituo vya kutolewa huduma za kinga.

Ugonjwa wa kifua kikuu ni hatari, hata hivyo unakingwa kwa chanjo.

Mzazi au mlezi hakikisha kila mtoto anapozaliwa anapata chanjo ya kuzuia kifua kuu

“Kumbuka chanjo ya kifua kikuu (BCG) Itamkinga mtoto dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu”.

Dalili za kuharibika kwa Mimba

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha mama mjamzito mimba yake kuharibika. Sababu kuu huwa ni magonjwa kama vile ugonjwa hatari wa malaria, ugonjwa unaotokana na zinaa kama vile kaswende na kisonono na U.T.I, dawa fulani fulani mfano Albendazole, Misoprostol, Metronidazole na kadhalika.

Lakini pia mjamzito akifanya kazi za kutumia nguvu nyingi anaweza kusababisha mimba yake kuharibika. Lakini kuna sababu nyingi ambazo zinasababisha mimba kutoka huweza kuzuilika kwa kwenda kliniki mapema yaani pale tu unapohisi una mimba hata kama ni wiki mbili na kufuata ushauri wa wataalamu.

Ukweli ni kwamba kuna wanawake wengi mimba zao huharibika na wao hushindwa kugundua mapema na matokeo yake anakaa na mtoto mfu hata miezi kadhaa bila kujua.

Zipo dalili ambazo husababisha mimba kuharibika kama tutakavyoona leo hapa. Dalili hizo ni hizi zifuatazo:

1. Kuwa na maumivu makali tumboni.

Ikiwa mjamzito atakuwa ana maumivu makali ya tumbo wakati ni mjamzito hiyo pia ni dalili mbaya. Kwa kawaida maumivu makali ya tumbo hasa kwa mimba kubwa ya miezi zaidi ya mitano au mimba ndogo kama mwezi mmoja, basi kuna uwezekano mkubwa kondo imeanza kujiondoa kwenye kizazi kwa mimba kubwa au mimba ndogo imeshindwa kuendelea kukua na moja kwa moja hiyo inaweza kuwa dalili ya kuwa mimba imeharibika.

2. Mimba kutokukua

Ikiwa mimba itaacha kuongezeka au kukua ni dalili nyingine ya mimba kuharibika. Kila mtu aliye mjamzito anategemea mimba iwe inakua kila siku na iwe kubwa kulingana na umri unavyozidi kwenda mbele, ikiwa mimba iko vilevile kwa miezi kadhaa, yaani haikui au ukubwa wa tumbo haubadiliki ujue kwamba mimba hiyo imeharibika, ili kupata uhakika wahi hospitali kupimwa.

3. Mtoto kuacha kucheza tumboni.

Ikiwa mtoto ataacha kucheza tumboni ni tatizo kubwa kwani kwa kawaida mtoto huanza kucheza akiwa na wiki ya 18 mpaka 20 kwa wanawake ambao hawajawahi kubeba mimba na wiki ya 16 mpaka 20 kwa wanawake ambao wameshawahi kuzaa. Ikitokea mtoto aliye tumboni ameshawahi kucheza lakini ghafla akawa hachezi au muda huo umepitiliza na bado kimya kuna uwezekano mkubwa ikawa mtoto huyo amefia tumboni, hivyo haraka sana wahi hospitali kumuona daktari.

4. Kutokwa na damu nyingi sehemu za siri.

Mjamzito akitokwa na damu nyingi sehemu za siri ni dalili kwamba mimba imeanza kuachia na mlango wa uzazi umeanza kufunguka, na hiyo inaashiria kwamba kuna mambo mawili yameshatokea kwanza inawezekana mtoto ameshafia tumboni au bado hajafa, lakini kama damu imetoka kwa wingi inaashiria kuwa mtoto huyo aliye tumboni atakufa tu.

5. Kutoka na vipande vya vyama sehemu za siri.

Ikiwa mama mjamzito atakuwa akitokwa na vipande vya nyama sehemu za siri ni dalili mbaya sana. Kutokwa na vipande vya nyama sirini ni kuashiria kwamba kuna mtoto ameharibika tumboni. Hali hiyo ya hatari ikitokea mjamzito anatakiwa asafishwe kuondoa masalio yaliyobaki.

6. Kupotea kwa dalili za ujauzito.

Kupotea kwa dalili za ujauzito ni tatizo lingine baya kwa mama mjamzito. Mara kwa mara mwanamke akiwa na ujauzito anakuwa na dalili nyingi kama vile kuwa na kichefuchefu, kukosa hamu ya kula baadhi ya vyakula, kutapika, kulamba vitu vichachu kama vile limao, ndimu, wengine hula udogo na wengi hubadilika sana tabia, hivyo basi dalili zote hizo za mimba zikisimama ghafla basi ujue mimba imeharibika.

Dalili za homa ya dengu (Dengue fever)

Dengue ni moja kati ya homa kali inayodhoofisha na kuambatana na maumivu makali. Kwa sasa hakuna kinga ya homa ya dengue, njia pekee ya kuepuka ugonjwa huu ni kuzuia kuumwa na mbu anayesambaza homa ya dengue.

Dalili za ugonjwa huu ni;

•Homa kali ya ghafla

•Maumivu makali ya kichwa

•Macho kuuma

•Maumivu ya viungo

•Kichefuchefu

•Kutapika

•Vipele ambavyo hutokea siku nne baada ya homa kuanza

•Kutoka damu puani, kwenye fizi na kuchubuka kirahisi

Mara nyingi dalili huwa sio kali na wengi hudhania ni homa ya mafua au maambikizi mengine ya virusi. Dalili hizi huanza kutokea baada ya wiki mbili, lakini kwa wengi huchukua wiki moja ya kwanza na tayari utaanza kuona dalili za dengue.

Shopping Cart