Baini Siri za Kuwa na Afya Bora na Utimamu

Faida 8 za kula pilipili mbuzi

Watu wengi tumekuwa hatufahamu utumiaji wa pipilipili, hasa pilipili mbuzi. Naomba leo tuangalie kwa uchache faida hizo za pilipili mbuzi.

1. Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu.

2. Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene (overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari.

3. Utafiti huo pia umeonyesha kwamba kawaida ya kula Pilipili kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha insulini kwa 60%. baada ya kula chakula.

4. Pilipili husaidia kupunguza maumivu na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili.

5. Pilipili usaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi!

6. Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye tumbo (Stomach Cancer)

7. Pilipili usaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua kiwango na metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.

8. Kula pilipili usaidia kupunguza cholesterol, na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu.

Faida 6 za kula karoti kiafya

Asilimia kubwa tunapenda kutumia karoti katika kuunga katika mboga ya nyama na si kuila karoti kama karoti. wataalamu wanashauri ili uwe na afya bora unatakiwa ule karoti sita kwa wiki au moja kwa siku. Unaweza kula karoti ya kuchemshaa,juisi au mbichi.

Faida ya kula karoti ni kama zifuatazo

1. Karoti husaidia kuimarisha macho kuona vizuri, mfano tatizo la kutoona vizuri usiku, pia inasaidia kuondoa matatizo ya allergy kwenye macho mfano macho kuwasha sababu ya vumbi.

Karoti inarutubisha cells mwilini na kuzifanya zisizeeke haraka. Hii inatokana na uwepo wa Vitamin A ambayo ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa macho kuona.

2. Huifanya ngozi iwe nzui na yenye afya, kama utatumia kurutubisha ngozi yako, ikwangue kwa kutumia grater kiasi unachotaka tia asali mbichi kijiko 1 kikubwa (cha kulia chakula) mafuta ya nzai au olive kijiko kimoja kikubwa na limao kijiko 1 kikubwa changanya vizuri, kisha itumie kusugua mwilini sehemu yoyote unayotaka, ukimaliza acha kama dakika 15 na zaidi kisha oga, itasaidia kuondoa taka katika vinyweleo, kuifanya ngozi iwe laini na kuondoa mikunjo katika ngozi, Kumbuka inatakiwa asali mbichi na siyo asali yoyote.

Karoti husaidia kuondoa sumu na taka mwilini, inaondoa mafuta yasiyotakiwa katika ini (cholesterol) na kuliwezesha lifanye kazi vizui, Kusafisha njia ya haja kubwa na kusaidia kupata choo vizuri (kuzuia constipation).

3. Karoti zinasaidia kufanya fizi na meno kuwa imara na kuchochea uzalishwaji wa mate.

Pia inasaidia kuzuia stroke (kiharusi, baadhi ya watafiti kutoka vyuo vikuu duniani wanasema ulaji wa karoti sita kwa wiki husaidia kutopata stroke.

Pia wamegundua kaoti zinatibu tatizo la kupoteza kumbukumbu kwa wazee.

4. Karoti hupunguza hatari ya kupata Shinikizo la Damu (blood pressure) kwani ulaji wa karoti husaidia mwili kupata madini muhimu ya Potassium ambayo husaidia kutanua mirija ya damu (bllod vessels na kufanya damu kufika katika maeneo husika ya mwili (organs).

5. Karoti pia husasidia kuzuia magonjwa mengine kama vile kisukari (Diabetes), Kiharusi (Stroke), Kansa pamoja na magonjwa ya moyo.

6. Karoti husaidia kuongeza kinga mwilini (immune booster). Kwasababu tabaia asilia ya karoti kuwa na antibacteia pamoja na antiseptic ambazo husaidia kuzuia kinga za mwili. Pia Karoti ina Vitamin C muhimu kwa kusisimua seli nyeupe za damu (white blood cells) ambazo ni sehemu muhimu katika kinga ya mwili.

Faida 25 za kutembea kwa Miguu

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na kuathiri afya zao kwa kiasi kikubwa. Hivi leo watu wanatumia vyombo mbalimbali vya usafiri kwenda karibu kila eneo.

Kwa hakika kutembea kwa miguu kuna manufaa mengi sana kwa ajili ya afya ya mwili, uchumi na maisha yako ya kijamii.

Ikiwa unapenda kuwa bora na mwenye tija zaidi katika nyanja zote, basi fahamu faida za kutembea kwa miguu.

  1. Hukabili maradhi ya moyo kwa kuhamasisha mzunguko mzuri wa damu.
  2. Huimarisha mifupa.
  3. Huondoa au kupunguza hatari ya kupata kiharusi.
  4. Husaidia kupunguza uzito.
  5. Huzuia saratani ya utumbo mpana.
  6. Hukuwezesha kupata vitamini D kutoka kwenye jua.
  7. Hukusaidia kuboresha usawa wa mwili wako (balance).
  8. Hukabili maradhi ya kisukari. Unapotembea unafanya mazoezi yanayoleta uwiano wa urefu na uzito – BMI; jambo litakalokukinga na aina ya pili ya kisukari (Type 2 Diabets).
  9. Hukabili shinikizo la damu.
  10. Huondoa msongo wa mawazo.
  11. Huongeza utayari.
  12. Hukufanya ujifunze mambo mbalimbali kwa kuona.
  13. Hukuokolea gharama za nauli au mafuta.
  14. Hupunguza lehemu mbaya mwilini (cholesterol)
  15. Huimarisha misuli.
  16. Husaidia mmeng’enyo wa chakula kwenda vizuri.
  17. Huwezesha kinga mwili kujiimarisha na kujijenga (kutokana na sababu kuwa kutembea ni aina ya zoezi).
  18. Huboresha uwezo wa kumbukumbu.
  19. Hukujengea mahusiano ya kijamii. Unapotembea utakutana na watu mbalimbali.
  20. Huzuia kuzeeka. Utafiti uliofanyika ulibaini kuwa watu wanaotembea umbali mrefu huishi zaidi.
  21. Hukuweka katika hali nzuri (mood).
  22. Hukusaidia kulala vizuri. Kumbuka mazoezi ni chanzo cha usingizi mzuri.
  23. Huboresha afya ya uzazi hasa kwa wanaume. Kutembea kama zoezi ni njia ya kuwapa wanaume nguvu katika afya ya uzazi.
  24. Huzuia kuharibika kwa mimba. Mazoezi ni muhimu sana kwa mama mjamzito kwa ajili ya afya yake na mtoto; hivyo zoezi rahisi na jepesi kwake ni kutembea.
  25. Huboresha mwonekano wa mwili. Mazoezi ni njia moja wapo ya kuufanya mwili wako uonekane katika umbo zuri. Hivyo kutembea kama aina mojawapo ya zoezi kunaweza kukusaidia sana.

Naamini umeona jinsi ambavyo kutembea kwa miguu kuna manufaa makubwa sana kwenye afya, uchumi na hata mahusiano yako ya kijamii.

Inashauriwa kuhakikisha unatembea kwa miguu angalau dakika 30 kila siku. Kwa njia hii utapata manufaa mengi yaliyotajwa hapo juu.

Faida 14 za kufunga chakula

Watu wengi wanafahamu kuwa kufunga kula ni swala linalohusiana na imani zaidi. Wengi hawafahamu kuwa kufunga kula kuna manufaa ya kiafya pia. Kufunga kula ni tendo lenye historia ndefu sana ambayo kimsingi chimbuko lake ni sababu za kiimani. Hata hivyo shuhuda na tafiti mbalimbali zimedhihirisha kuwa kuna manufaa mengine kemkem ya kufunga kula mbali na yale ya kiimani.

Ikiwa basi unapenda kuongeza maarifa pamoja na kuboresha afya yako, fahamu faida za kufunga kula.

1. Huboresha metaboli

Metaboli ni mchakato ambao mwili hutumia virutubisho kutoka kwenye vyakula ili kujipa nguvu.

Unapofunga kwanza unapumzisha mfumo wako wa umeng’enyaji, pili unaufanya mchakato wa metaboli kwenda vizuri kwani mwili utatumia vyema virutubisho vilivyoko mwilini tayari.

2. Huboresha mzunguko wa damu

Tafiti mbalimbali zinaeleza kuwa kufunga kula hufanya mzunguko wa damu uende vizuri hasa kwa watu wenye aina ya pili ya ugonjwa wa kisukari (Type 2 Diabetes)

3. Husaidia kupunguza uzito

Kufunga kula ni njia mojawapo bora ya kupunguza uzito kwani kwa njia hii mwili hutumia mafuta yaliyoko mwilini ili kujipa nguvu.

4. Hufanya insulini kufanya kazi vizuri

Unapofunga kula mwili huzalisha insulini ili kutawala kiwango cha sukari mwilini kwani hakuna sukari inayoingia. Kwa njia hii insulini itaweza kuzalishwa na kufanya kazi ipasavyo mwilini mwako.

5. Hupunguza shinikizo la damu

Watu wengi wanapofunga hujikuta pia shinikizo la damu likipungua, hii inasababishwa na kupungua kwa kiwango cha chumvi kwenye damu.

Kumbuka chumvi nyingi husababisha shinikizo la damu. Hivyo kufunga ni kupunguza kiasi cha chumvi kinachoingia mwilini.

6. Husaidia kutawala sukari mwilini

Kwa watu wenye kiwango kikubwa cha sukari mwilini, wanaweza kutumia njia ya kufunga ili kukipunguza. Kumbuka unapofunga unapunguza pia kiwango cha sukari kinachoingia mwilini.

7. Hurefusha maisha

Watafiti wa afya wanaeleza kuwa kula sana kunakufanya pia uzeeke mapema. Wanaeleza kuwa kula kidogo kutatawala mchakato wa metaboli, hivyo kuzuia seli kuchakaa mapema.

8. Hukuwezesha kuhisi njaa

Kuna watu huwa wanashindwa kula vizuri kwa sababu huwa hawahisi njaa vyema. Njia moja wapo ya kupata njaa ambayo itakusababisha ule vyema, ni kufunga kula.

9. Huboresha utendaji kazi wa ubongo

Kufunga kula kunachochea uzalishaji wa protini ya brain-derived neurotrophic factor (BDNF) ambayo ni muhimu sana katika ukuaji, afya na utendaji kazi wa seli za fahamu za ubongo (neurons).

10. Huboresha kinga mwili

Kufunga kula hufanya kinga mwili kujiimarisha ili kukabiliana na chochote kinachoweza kutokea.

Hii ni kwa sababu unapofunga unabadili hali ya msingi ya mwili na inabidi kinga mwili kujiimarisha kujianda na lolote linalohusiana na mabadiliko hayo.

11. Huboresha afya na mwonekano wa ngozi

Ingawa lishe bora ni muhimu kwa ajili ya afya ya ngozi, kufunga kula kunaifanya ngozi iwe na mwonekano mzuri.

Ngozi inapokuwa na sukari nyingi, huifanya iwe na mwonekano usiovutia.

Kwa kufunga kula utapunguza kiwango cha sukari kinachoingia mwilini, hivyo kuwa na ngozi yenye mwonekano mzuri.

12. Huwezesha kujizalisha upya kwa seli
Seli hukua na kuchakaa au hata kufa kwenye mwili wa binadamu. Kama ilivyo kwa kinga mwili, utafiti unaonyesha kuwa unapofunga mwili huzalisha seli mpya ili kujiaanda au kukabili badiliko lolote linaloweza kutokea.

13. Huboresha afya ya moyo

Watafiti wa afya wanaeleza kuwa kufunga kula kunasababisha mishipa ya moyo na misuli kufanya kazi vyema.

14. Husaidia Kutawala umbo la mwili na mwonekano

Njia nzuri ya kutawala umbo au mwonekano wako ni kwa kutawala kile unachokula. Hii ndiyo sababu walimbwende au warembo hujizuia sana kula hovyo ili wasije wakaharibu mwonekano wao.

Kwa njia ya kufunga kula utaweza kutawala umbo na mwonekano wa mwili wako kama unataka uwe mnene au mwembamba.

Kumbuka

Hakikisha unafunga kwa kuzingatia kanuni za afya pamoja na hali ya afya ya mwili wako. Kama hujawahi kufunga, unaweza kuanza taratibu au kwa kupunguza kiasi cha mlo wako hadi utakapozoea.
Ikiwa unatatizo la kipekee la afya, ni vyema ukapata ushauri wa daktari kwanza.

Faida 13 za kunywa juisi ya miwa

Unapopita maeneo mengi ya mijini na pembezoni wa miji utakutana na wafanyabiashara wa miwa wanaouza miwa na juisi yake. Wengi hununua juisi ya miwa kwa kuwa hufurahia utamu wake. Lakini umeshajiuliza juisi miwa ina faida gani kiafya?

Kuna faida nyingi za juisi ya miwa. Baadhi ya faida hizo ni kama zifuatazo;
1. Juisi ya miwa ina uwezo mkubwa wa kuipatia miili nguvu kwa haraka na kukata kiu ya maji. Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari “sucrose” ambayo kazi yake kuu ni kutengeneza nguvu mwilini. Kwa hiyo wakati mwingine ukiwa na uchovu, badala ya kunywa vinywaji vya viwandani tafuta juisi ya miwa.

2. Ingawa juisi ya miwa ina utamu lakini inafaa sana kwa watu wenye kisukari. Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari halisi ambayo ina uwezo mdogo wa kuzidisha kiwango cha sukari mwilini au kitaalamu inaitwa “Low Glycemic Index”. Kutokana na hilo juisi ya miwa inashauriwa kutumiwa kama mbadala wa vinywaji vingine vya viwandani. Ni muhimu pia kwa watu wenye kisukari kutumia juisi hii kwa kiasi kidogo au kulingana na ushauri wa Daktari.

3. Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya calcium, magnesium, potassium, chuma na manganese. Madini haya yana uasili wa ualkali ambao husaidia kupunguza uwezekano wa kupata kansa kama vile kansa ya Tezi dume “Prostate cancer” na kansa ya maziwa “Breast Canser”.

4. Juisi ya miwa inasaidia kuongeza kiwango cha protein mwilini na ku-imarisha ufanyaji kazi wa figo.

5. Juisi ya miwa iliyochanganywa na maji ya Nazi husaidia kupunguza maumivu hasa yanayosababishwa na maambukizi ya ngono “STDs” na kidney stones.

6. Juisi ya miwa husaidia kulinda maini yasipate maambukizi. Hii ndo maana Madaktari hushauri matumizi ya juisi ya miwa kwa watu wenye ugonjwa wa Homa ya Manjano.

7. Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya potassium ambayo husaidia kuimarisha mmeng’enyo wa chakula.

8. Husaidia kuzuia maambukizi katika tumbo na utumbo.

9. Vilevile husaidia katika kutibu matatizo ya choo kigumu au kitaalamu inaitwa “constipation”.

10. Uchunguzi unaonyesha juisi ya miwa husaidia kuzuia meno kuoza na matatizo ya kupumua kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha madini. Kwa hiyo kama unafikiria kwenda kwa daktari kung’arisha meno yako, kunywa juisi ya miwa mara kwa mara.

11. Juisi ya miwa husaidia katika kupambana na mabaka mabaka na kung’arisha ngozi.

12. Juisi ya miwa huweza kutumika kama ” face mask na scrub” kwa kuipaka kwenye ngozi na hivyo kusaidia katika kuing’arisha na kuiimarisha uso.

13. Juisi ya miwa ina faida nyingi mwilini, ni muhimu kuhakikisha usafi katika utengenezaji wake.

Kumbuka: Juisi ya miwa isiyokuwa salama inaweza ikawa ni chanzo kikubwa cha magonjwa ya tumbo na kuhara.

Shopping Cart